Pope Leo XIV agunduliwa kuwa na cancer ya pafu

The Dictator

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
4,475
Reaction score
12,281
1176886_0.jpeg.webp

Vatican imethibitisha rasmi kuwa Papa Leo XIV amegunduliwa kuwa na saratani ya pafu (lung cancer) kufuatia upasuaji uliofanyika Jumanne, Oktoba 13, 2026.

Wakati wa upasuaji huo, madaktari walifanikiwa kuondoa sehemu ya chini ya pafu lake la kulia (lower lobe) baada ya vipimo kudhibitisha uwepo wa uvimbe wenye seli za saratani.

Taarifa kutoka Vatican ilieleza kuwa upasuaji ulifanyika kwa mafanikio makubwa bila kuwa na matatizo yoyote.

::- Siku chache zilizopita, Papa Leo alitangaza kwa waumini kuwa alikutwa na uvimbe mdogo kwenye pafu lake wakati wa uchunguzi wa kawaida wa afya, jambo lililopelekea kupangwa kwa upasuaji huo wa kuondoa uvimbe huo.
 
View attachment 3690224

Mwenyezi Mungu amjaalie nafuu ya mapema na hatimae uponyaji wa changamoto hiyo ya kiafya, Amen 🙏
 
Vatican imethibitisha rasmi kuwa Papa Leo XIV amegunduliwa kuwa na saratani ya pafu (lung cancer) kufuatia upasuaji uliofanyika Jumanne, Oktoba 13, 2026.
Umenikumbusha filamu ya the Godfather, hua wanakuaga na vita kubwa sana hawa watu, vita ya ndani na vita ya nje zote kwa pamoja.

Lakini kisayansi inasemekana kwamba kansa ya mapafu kwa asilimia kubwa hutokana na uvutaji wa sigara sababu 80% ya vifo vya watu wenye kansa ya mapafu chanzo ni uvutaji wa sigara, ukiondoa vyanzo vingine km kuvuta kemikali zenye sumu, uchafuzi wa hali ya hewa na uchaafuzi wa mazingira kwa ujumla km kuchoma kemikali zenye sumu, nk, hii maana yake nini? Hii maana yake ni kwamba papa alikua anauvuta moshi mweupe.

Pole sana ijapokua ni ugonjwa mmoja hatari sana na unaua watu wengi dunia nzima ila ukiupata na ukagundulika ukiwa kwenye hatua za awali unatibika kabisa na mgonjwa anapona.
 
Mungu mponyaji na mlinzi wetu, tunaomba amjalie afya njema mtumishi wake.
 
Hongera kwao wazungu kwa maendeleo makubwa ya matibabu.
Ingekuwa huku kwetu!!!

Hata hivyo sijui makadinali pale Vatican sana kula nini, ni wachache sana ambao hawaumwi!
Umri umeenda, lazima waumwe. Hiyo ni kawaida.
 
Huyu ni mkuu wa kanisa, hajaombewa uvimbe uyeyuke, wameitwa madaktari, wakachunguza. Sasa wewe unayedhani ni kondoo kuliko Papa ukipata uvimbe nenda kakemewe ili uvimbe uyeyuke.
Hayo mambo ya kuombea uvimbe uyeyuke ni huku nchi maskini ambapo watu hawamudu pesa za matibabu na pia hawajaelimika,watu wangekuwa wanamudu matibabu,hakuna mtu angeenda kuombewa uvimbe uyeyuke.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh

Mkuu, kuna watu wapo brain washed uwezo wa kutibu malaria anao ila analeta mchungaji aombee mpaka mtu anazidiwa ndo akili inamkaa sawa.
 
Anakuwa brainwashed kutokana na mazingira aliyopo/aliyokulia. Mtu anakua toka yuko mtoto anapewa stori za uchawi na kulogwa lazima aombewe hata kama ana malaria .
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Anakuwa brainwashed kutokana na mazingira aliyopo/aliyokulia. Mtu anakua toka yuko mtoto anapewa stori za uchawi na kulogwa lazima aombewe hata kama ana malaria .
Yes, ni moja ya sababu.
 
Huyu ni mkuu wa kanisa, hajaombewa uvimbe uyeyuke, wameitwa madaktari, wakachunguza. Sasa wewe unayedhani ni kondoo kuliko Papa ukipata uvimbe nenda kakemewe ili uvimbe uyeyuke.
Kuombe ni kwa waafrika tu mkuu.
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Huyu ni mkuu wa kanisa, hajaombewa uvimbe uyeyuke, wameitwa madaktari, wakachunguza. Sasa wewe unayedhani ni kondoo kuliko Papa ukipata uvimbe nenda kakemewe ili uvimbe uyeyuke.
Unadhani hakuna watu walioombewa magonjwa na wakapona kwa muujiza? Hivi juzi tu mamia ya watu nchi ya Pakistani wameponywa magonjwa katika mkutano wa Injili, kwa akili yako unadhani muislamu raia wa Pakistani anaweza kutunga uongo kuwa ameponywa ugonjwa na Yesu

Suala la uponyaji wa kimiujiza linategemea pia na fundisho/doctrine ya kanisa husika kwamba linatetewa au kusisitizwa kwa kiwango gani, sio kila dhehebu lina msisitizo unaofanana linapokuja suala la uponyaji

Hata katika madhehebu au makanisa yanayohubiri uponyaji, hayakatazi watu kwenda hospitali, mtu anaweza kupata uponyaji wake kwa njia za kisayansi za kitabibu na bado hilo haliondoi ukweli kuwa Mungu ndiye mponyaji kwa sababu hata uwepo wa resources zote za kitabibu ni kutokana upaji wa Mungu huyo huyo.

Hata huyo kiongozi aliyeenda hospitali pia bila shaka amemwomba Mungu amponye na bado anaendelea kumwomba Mungu amponye, suala la namna gani atapokea uponyaji wake hilo hatuwezi kumpangia Mungu wala kulazimisha Imani ya mgonjwa

Sisi watanzania tuna matatizo mengi;
1) Umaskini unafanya wasionacho washindwe kumudu gharama za matibabu
2) Ujinga unafanya watu washindwe kuweka uwiano sawa kati ya sayansi na miujiza ya Mungu
3) Utapeli unafanya wengine wajipachike uchungaji na kuendesha huduma za kiroho kinyume na biblia
4) Chuki za kidini/kimadhehebu na Ujinga pia vinafanya kukosoa kila kitu bila kuchanganua mambo kama inavyopaswa
 
Huyu ni mkuu wa kanisa, hajaombewa uvimbe uyeyuke, wameitwa madaktari, wakachunguza. Sasa wewe unayedhani ni kondoo kuliko Papa ukipata uvimbe nenda kakemewe ili uvimbe uyeyuke.
Papa hawezi kuwa kondoo😅 yeye ndio mchungaji wa hao kondoo mazuzu😅
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom