Unadhani hakuna watu walioombewa magonjwa na wakapona kwa muujiza? Hivi juzi tu mamia ya watu nchi ya Pakistani wameponywa magonjwa katika mkutano wa Injili, kwa akili yako unadhani muislamu raia wa Pakistani anaweza kutunga uongo kuwa ameponywa ugonjwa na Yesu
Suala la uponyaji wa kimiujiza linategemea pia na fundisho/doctrine ya kanisa husika kwamba linatetewa au kusisitizwa kwa kiwango gani, sio kila dhehebu lina msisitizo unaofanana linapokuja suala la uponyaji
Hata katika madhehebu au makanisa yanayohubiri uponyaji, hayakatazi watu kwenda hospitali, mtu anaweza kupata uponyaji wake kwa njia za kisayansi za kitabibu na bado hilo haliondoi ukweli kuwa Mungu ndiye mponyaji kwa sababu hata uwepo wa resources zote za kitabibu ni kutokana upaji wa Mungu huyo huyo.
Hata huyo kiongozi aliyeenda hospitali pia bila shaka amemwomba Mungu amponye na bado anaendelea kumwomba Mungu amponye, suala la namna gani atapokea uponyaji wake hilo hatuwezi kumpangia Mungu wala kulazimisha Imani ya mgonjwa
Sisi watanzania tuna matatizo mengi;
1) Umaskini unafanya wasionacho washindwe kumudu gharama za matibabu
2) Ujinga unafanya watu washindwe kuweka uwiano sawa kati ya sayansi na miujiza ya Mungu
3) Utapeli unafanya wengine wajipachike uchungaji na kuendesha huduma za kiroho kinyume na biblia
4) Chuki za kidini/kimadhehebu na Ujinga pia vinafanya kukosoa kila kitu bila kuchanganua mambo kama inavyopaswa