Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Posho mbili, Spika Sitta, Takukuru na Maadili yake!

Hii inaonyesha kwamba Hosea hana jipya anatumiwa na mafisadi tu kuwatisha Wabunge ili wasiiweke kwenye kiti moto kuhusiana na sakata la Richmond. Hosea wacha uhuni kazi imekushinda bora tu ujiuzulu.
 
Hakuna kipya alichosema kwenye mkutano wake according to some news sources za hapo nyumbani.Cha kusubiri ni maamuzi ya Bunge hiyo Jumatano.Binafsi nisingependa Bunge liwe juu ya sheria lakini timing ya PCCB siyo nzuri kabisa na pia inaleta maswali mengi kuhusu nia na madhumuni yake.Ukweli ni kuwa Serikali haitakuja na majibu ya kuridhisha kwa mara nyingine tena.Mategemeo ya wengi yalikuwa Dr.Hosea atajiuzulu lakini haijatokea.Kiburi hichi si kidogo kwa sababu anajua anashikilia wapi kwenye serikali ya sasa.Nanukuu alichosema..."...there is life after PCCB..."

Kiburi hiki.....sijui!

Mungu atusaidie Tanzania.

mungu alishatusaidia na ujinga wetu,kwani nchi hii haina jeshi la kujenga nchi,maana hawa wote jeuri yao inatokana na ahadi za wahindi za kuwapa maisha, na ndiyo maana viongozi wetu hawatuheshimu maana walishalewa,nani alijuwa kama mkapa angetugeuka. sasa mambo anayofanya kikwete tuliyemuamini kwa asilimia 80 yako sawa? je ni haki kwetu afanyayo?
 
Wabunge waonyesha jeuri
headline_bullet.jpg
Wachukua nyingine mbili mpya jana
headline_bullet.jpg
Sitta asema si haramu, ni takrima
headline_bullet.jpg
Wapuuza vitisho vya Takukuru

Mapambano ya wabunge na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa juu ya upokeaji wa posho mara mbili jana uliingia hatua mpya baada ya kupokea posho hizo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Hatua hiyo si tu inaiweka Takukuru katika mazingira magumu zaidi juu ya hatua zake za kuwahoji wabunge kwa kuchukua posho mara mbili, ile wanayolipwa na Ofisi ya Bunge na za kwenye taasisi nyingine za umma wanakokwenda kufanya kazi, bali inaonyesha wazi kupuuzwa kwa harakati hizo za kuwadhibiti wabunge.
Jana mchana wabunge wakiwa wamekwisha kuhudhuria kikao cha asubuhi cha Bunge na kwa maana hiyo kuhalalisha posho zao kutoka Ofisi ya Bunge, walihudhuria semina iliyoandaliwa na Wizara hiyo ili kujadili muswada wa sheria ya watoto.
Muswada huo unaoratibiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, ulisomwa kwa mara ya kwanza bungeni Julai 31, mwaka huu.
Jana semina hiyo ilifunguliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Philip Marmo, na ilihudhuriwa pia na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margareth Sitta, Manaibu Waziri na watumishi wengine wa Bunge.
Semina hiyo ililenga kuwaelimisha wabunge hao kuhusu muswada huo.
Kabla ya semina hiyo, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu aliwatangazia wabunge kuwepo kwa semina hiyo na kusema ‘itifaki zote zimezingatiwa.’
Sitta alisema kuwa wabunge wamekuwa wakiandamwa kutokana na kulipwa posho nje ya Bunge, lakini akasema hiyo ni takrima na kwamba makundi mengine wakiwemo waandishi wa habari nao wanaipokea.
Wabunge waliohojiwa na Nipashe kuhusu kauli hiyo walisema ina maana pana, lakini yenye kubeba tafsiri ya huduma zote zinazohitajiwa kwa mwalika wa semina, ikiwemo makabrasha na posho.
Akifungua semina hiyo, Marmo alisema inatoa fursa muhimu kwa wabunge kuujua muswada huo kwa undani, hivyo kurahisisha mjadala pindi utakapofikishwa bungeni.
Marmo alisema kwa muda mrefu Tanzania haijakuwa na Sheria ya Watoto, hivyo muswada huo utasaidia kujenga na kufanikisha upatikanaji wa mazingira bora na haki kwa mtoto.
Alisema baada ya kusomwa kwake, muswada huo ulijadiliwa na wadau mbalimbali waliotoa maoni yao ambayo kwa kiasi kikubwa yatafanikisha azma ya kuwezesha kupatikana kwa haki za mtoto.
Wakati huo huo, habari zimetanda mjini hapa kuwa bado Takukuru wanaendelea kuwawinda baadhi ya wabunge machachari ili kuwahoji kabla ya kuwasilishwa bungeni taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu kashfa ya Richmond.
Habari kutoka vyanzo mbalimbali mjini Dodoma, zinaeleza kuwa baadhi ya wabunge ambao wamesimama kidete kuibana serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio ya Richmond wamepelekewa taarifa za kujiandaa kuhojiwa na taasisi hiyo kuhusiana na kupokea posho nje ya vikao vya Bunge.
Mbunge mmoja ameiambia Nipashe kuwa tangu wiki iliyopita alitaarifiwa na Takukuru kuhusu mpango wa kumuita kumhoji, lakini akasema hadi sasa hajaitwa.
Alisema anashangaa hadi sasa kutoitwa na Takukuru, hatua ambayo alisema inalenga kudhoofisha mjadala wa Richmond baada ya kuwasilishwa bungeni Jumatano ijayo. Mbunge mwingine, ambaye naye ameeleza kuwa ataitwa kuhojiwa na Takukuru, alisema kitendo cha kuwaita na kuwahoji siku chache kabla ya kuwasilishwa na kujadiliwa kwa hoja ya Richmond, lengo lake ni kutaka kuwajengea hofu ili wasiweze kushiriki katika mjadala huo.
Baadhi ya wabunge ambao wamethibitisha kuhojiwa na taasisi hiyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, William Shellukindo.
Shellukindo, ambaye ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) na kamati yake wamekuwa mstari wa mbele kuibana serikali itekeleze maazimio ya Bunge kuhusu Richmond hususan azimio linalotaka watendaji waliohusika kuipa zabuni ya kufua umeme wa dharura wa megawati 100 wa kampuni hewa ya Richmond wachukuliwe hatua.
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye aliiongoza Kamati Teule ya Bunge kuchunguza uhalali wa zabuni ya Richmond, aliitwa kuhojiwa na Takukuru, lakini alikataa kufanya hivyo. Alipotakiwa kuthibitisha kuwepo kwa mpango huo, Afisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kapwani, alisema jana jioni kuwa hakuwa katika nafasi ya kulitolea ufafanuzi suala hilo kwa kuwa yuko nje ya ofisi kutokana na ugonjwa.
Mbunge mwingine ambaye amehusishwa na mpango wa kuhojiwa ni Lucas Selelii, Nzega (CCM). Selelii ni mmoja wa wajumbe waliounda Kamati Teule ya Bunge ya kuchunguza zabuni ya Richmond.
Baadhi ya Wabunge na makundi mengine ya jamii wanaichukulia hatua ya Takukuru kuwa ina lengo la kulitisha Bunge ili lisiweze kuibana serikali ili iwachukulie hatua waliohusika na mkataba wa kitapeli ulioligharimu taifa kiasi cha Sh. bilioni 200 kuilipa kampuni ya Richmond na mrithi wake Dowans.
Kutokana na mlolongo wa matukio hayo, baadhi ya watu wanahoji uadilifu wa Takukuru inayoongozwa na Dk. Hoseah kuwahoji wabunge wakati hatma ya utekelezaji wa mapendekezo ya Bunge haijajulikana.
Kashfa ya Richmond ilimlazimisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kujiuzulu Februari mwaka jana pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na mtangulizi wake, Dk. Ibrahim Msabaha.
Pamoja na mambo mengine maazimio ya Bunge yalitaka kuwajibishwa kwa watendaji wa serikali wakiwemo aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi na Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah.

CHANZO: NIPASHE

Aibu tupu. Watu wazima wanashabikia wizi!!!
 
Dkt Hoseah ameongea na waandishi wa habari leo na miongoni mwa mambo aliyoyaelezea ni kwamba ahukumiwe kwa haki na sio kwa hisia. Pia alisema kwamba haonei mtu na anafanya kazi kwa mujibu wa sheria. Alidai pia kwamba tuhuma dhidi ya wabunge kulipwa posho mbili kwa kazi moja zimetoka Bungeni! Hoseah alisema ombi la kufanywa uchunguzi huo ni la Bunge lenyewe kupitia barua ya Februari 26, 2008, ambayo ilimtaja yeye kwa jina ikimtaka afanye uchunguzi huo na kuhoji: "Kwa hiyo Bunge lenyewe linaweza kuandika barua kutaka kuwalenga watu fulani?"

Dk Hoseah alifafanua kwamba, tayari suala hilo la kuwajibishwa liko mamlaka ya juu (rais), hivyo ni vema wakasubiri maamuzi na kusisitiza kwamba, "uchunguzi huo utaendelea kwa hiyo waheshimiwa wabunge, wazee wangu toeni ushirikiano ili suala hili lisije kutufikisha pabaya, nchi hii ni ya amani".
Mkuu huyo alitumia mkutano huo kufafanua pia kwamba, uchunguzi huo haukumlenga mtu yeyote ambaye ni mjumbe wa kamati iliyochunguza kashfa ya Richmond, akisema: "Kwanini, mbona Mheshimiwa Zitto (Kabwe) tumemhoji, yeye alikuwa kamati ya Richmond?"

Kumbukumbu za Bunge (Hansard), kuhusu Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini ya Agosti mosi, kujibu taarifa ya serikali iliyotolewa Julai 25, inasema: "Mheshimiwa Spika, Azimio Na. 20, Serikali iendeshe uchunguzi maalum ili kubaini ukweli kama taarifa rasmi ya Takukuru iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine.

"Na kama jalada halisi linalohusu kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa jingine kwa lengo la kuficha ukweli. Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Serikali: Kamati ya Vyombo vya Dola imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na suala hili.

"Na imebainika kuwa, si kweli kuwa taarifa rasmi ya Takukuru iliyotoa matokea ya uchunguzi kuhusu mchakato wa suala la Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine kwa lengo la kuficha ukweli.

"Vile vile, taarifa ya kamati ya vyombo vya dola inaonyesha baada ya upelelezi na uchunguzi wa kina kufanyika wameridhika kuwa jalada halisi la Richmond lililokuwa BRELA halikuharibiwa na wala hakukuwa na jalada lingine lililowekwa kuficha ukweli wa jambo hili."

"...Maoni ya Kamati; Kamati inaridhika na taarifa hiyo."
Hoseah akitumia azimio hilo, alisema alibahatika kusoma kwa makini taarifa zote za kamati kuanzia ya kwanza na hiyo ya pili na kuhoji : "Sasa nijiuzulu kwa kosa lipi, watu mnihukumu kwa haki, au unataka kuchukua nafasi yangu (alimuuliza mwandishi wa gazeti hili)?"
(Source: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15735).
 
kosa lako ni kushindwa kuishauri serikali kwamba kesi ya posho mara mbili etc ni jukumu la polisi na kiutawala zaidi kuliko kuwa la rushwa. hivyo ungewarudishia faili lao na barua zao ziende kunako husika.
na zaidi ya hapo hata sisi takukuru hua tunalipa hiyo posho kwa waandishi wa habari na wabunge na wadau wengine wanapo hudhuria warasha/kongamano /na semina zetu bila kusahau mikutano yetu iwe ya ndani au ya nje.
zaidi ya hapo tunatuhumiwa na wabunge kwa kuisafisha richomond, sasa wakati huu huh tukiwachunguza haita onekana tunatenda haki.
 
hosea maji shingoni tena ole sendeka alisema takukuru walifanya semina na wao wakagawa posho hizo hizo kwa wabunge walioshiriki, leo hii wanachunguza posho hiyohiyo waliotoa
 
kosa lako ni kushindwa kuishauri serikali kwamba kesi ya posho mara mbili etc ni jukumu la polisi na kiutawala zaidi kuliko kuwa la rushwa. hivyo ungewarudishia faili lao na barua zao ziende kunako husika

Nafikiri kosa alilozungumzia ni linalohusiana na Richmond! Chungulia post #1 tena utaelewa!
 
hosea maji shingoni tena ole sendeka alisema takukuru walifanya semina na wao wakagawa posho hizo hizo kwa wabunge walioshiriki, leo hii wanachunguza posho hiyohiyo waliotoa

Kosa la wabunge waliokwapua posho mbili kwa kazi moja kinyume na sheria ni kutokutoa taarifa kwa TAKUKURU kwamba tayari walishapokea posho kwa hiyo wasingestahili kulipwa tena!
 
Kesho itakapotolewa ripoti ya serikali katika kutekeleza maazimio yaliyotolewa na Kamati Teule ya Richmond kitaeleweka kwamba sakata hili lina mweleko gani!
 
Dkt Hoseah ameongea na waandishi wa habari leo na miongoni mwa mambo aliyoyaelezea ni kwamba ahukumiwe kwa haki na sio kwa hisia. Pia alisema kwamba haonei mtu na anafanya kazi kwa mujibu wa sheria. Alidai pia kwamba tuhuma dhidi ya wabunge kulipwa posho mbili kwa kazi moja zimetoka Bungeni! Hoseah alisema ombi la kufanywa uchunguzi huo ni la Bunge lenyewe kupitia barua ya Februari 26, 2008, ambayo ilimtaja yeye kwa jina ikimtaka afanye uchunguzi huo na kuhoji: "Kwa hiyo Bunge lenyewe linaweza kuandika barua kutaka kuwalenga watu fulani?"

Dk Hoseah alifafanua kwamba, tayari suala hilo la kuwajibishwa liko mamlaka ya juu (rais), hivyo ni vema wakasubiri maamuzi na kusisitiza kwamba, "uchunguzi huo utaendelea kwa hiyo waheshimiwa wabunge, wazee wangu toeni ushirikiano ili suala hili lisije kutufikisha pabaya, nchi hii ni ya amani".
Mkuu huyo alitumia mkutano huo kufafanua pia kwamba, uchunguzi huo haukumlenga mtu yeyote ambaye ni mjumbe wa kamati iliyochunguza kashfa ya Richmond, akisema: "Kwanini, mbona Mheshimiwa Zitto (Kabwe) tumemhoji, yeye alikuwa kamati ya Richmond?"

Kumbukumbu za Bunge (Hansard), kuhusu Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini ya Agosti mosi, kujibu taarifa ya serikali iliyotolewa Julai 25, inasema: "Mheshimiwa Spika, Azimio Na. 20, Serikali iendeshe uchunguzi maalum ili kubaini ukweli kama taarifa rasmi ya Takukuru iliyotoa matokeo ya uchunguzi kuhusu mchakato wa Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine.

"Na kama jalada halisi linalohusu kampuni ya Richmond lililokuwa BRELA liliharibiwa na kuwekwa jingine kwa lengo la kuficha ukweli. Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Serikali: Kamati ya Vyombo vya Dola imekamilisha uchunguzi wake kuhusiana na suala hili.

"Na imebainika kuwa, si kweli kuwa taarifa rasmi ya Takukuru iliyotoa matokea ya uchunguzi kuhusu mchakato wa suala la Richmond ilikataliwa na kuharibiwa na kutolewa nyingine kwa lengo la kuficha ukweli.

"Vile vile, taarifa ya kamati ya vyombo vya dola inaonyesha baada ya upelelezi na uchunguzi wa kina kufanyika wameridhika kuwa jalada halisi la Richmond lililokuwa BRELA halikuharibiwa na wala hakukuwa na jalada lingine lililowekwa kuficha ukweli wa jambo hili."

"...Maoni ya Kamati; Kamati inaridhika na taarifa hiyo."
Hoseah akitumia azimio hilo, alisema alibahatika kusoma kwa makini taarifa zote za kamati kuanzia ya kwanza na hiyo ya pili na kuhoji : "Sasa nijiuzulu kwa kosa lipi, watu mnihukumu kwa haki, au unataka kuchukua nafasi yangu (alimuuliza mwandishi wa gazeti hili)?"
(Source: http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=15735).

Hawa watu nadhani wanatuchezea akili. Kwani baada ya kutolewa maazimio yale 23 ya bunge, serikali ilitakiwa kufanya uchunguzi tena au kuyatekeleza?

Kwa mfano kama azimio lilisema Hosea awajibishwe, serikali ilikuwa tena na nafasi ya kuchunguza upya kuhusu kosa la Hosea au ilitakiwa kumpa haki yake ya kumwachisha wadhifa wake?

Na kama Hosea hakukosea, pia Mwanyika au mdendaji yeyote serikali hakufanya kosa, basi nani alifanya makosa yote kuhusu Richmond? Na kwa nini EL na wenzake walisusa na kuachia nafasi zao na kusababisha baraza zima la mawaziri kufa kifo cha mende?

Naona ni usanii tu ndo unaendelea.
 
Nasikia mh. huyu kaitwa Dodoma jana,nadhani leo kuna jambo litatokea-tungoje na tusubiri.leteni data zaidi ya safari yake huko Dodoma.
 
hosea maji shingoni tena ole sendeka alisema takukuru walifanya semina na wao wakagawa posho hizo hizo kwa wabunge walioshiriki, leo hii wanachunguza posho hiyohiyo waliotoa

Nadhani hukusikiliza press conference ya Dr. Hosea. Kwa kweli katoa maelezo mazuri sana ya kujibu hoja zote walizotoa wabunge. Imeonyesha wazi kuwa Spika na Wabunge ni wapotoshaji wakubwa. Tatizo ni wabunge kulipwa posho mbili na sio kulipwa posho moja.

Ufafanuzi alioutowa:-

1. Posho walizotoa Takukuru kwa wabunge hazi kutolewa mara mbili. Ofisi ya Bunge haikuwalipa posho wabunge ku attend seminar hiyo. Kwa hiyo ni Takukuru tu ndio iliyowalipa.

2. Posho zinazochunguzwa na Takukuru ni zile zinazolipwa kwa Kamati za Bunge ambazo kwanza hulipwa na Bunge na baadae Kamati zikienda kufanya uchunguzi na mahojiano na wizara na mashirika hudai tena posho hizo hizo. Hii si takrima bali ni makosa.

3. Kwa sheria za Takukuru, kupokea pesa bila kuzitolea jasho ni rushwa.

4. Wabunge hawana kinga katika makosa ya rushwa. Wanayo kinga katika mambo yanayohusu shughuli zao za Bunge na matamshi wanayotowa Bungeni.

5. Ni Bunge ndio lilimuonba Hosea kufanya uchunguzi huo.

6. Yeye hanyimwi usingizi kama wabunge watampigia kura ya kutokuwa na imani naye. Yeye yuko pale kuwahudumia watanzania kwa kufanya kazi yake kwa uadilifu.

7. Wabunge waiachie Takukuru ifanye kazi yake.

8. Takukuru haikuwadhalilisha wabunge kwani yenyewe haikutangaza wabunge iliyowahoji bali ni wabunge wenyewe ndio walikimbilia kutangaza katika vyombo vya habari.

9. Hakuna Mtanzania yeyote aliye juu ya sheria.

Mimi personally nampongeza sana Dr. Hosea kwa ujasiri wake wa kuwa na msimamo. I am sure wabunge wamepata shock, walidhani wangeweza kumtingisha kwa kumtisha na sakata la Richmond lakini kumbe jamaa hatetereki. Kwa vipimo vyangu amefanikiwa kuvunja hoja zote za Sitta na wabunge.
 
Lakini kupokea posho na rushwa wapi na wapi? Mimi nina wasiwasi ilikuwa ni jitihada za kuwa-discredit akina mwakyembe kabla ya kujadiliwa kwa ropiti ya Richmond. Labda kama "rushwa" imepewa maana pana zaidi.
 
Nadhani hukusikiliza press conference ya Dr. Hosea. Kwa kweli katoa maelezo mazuri sana ya kujibu hoja zote walizotoa wabunge. Imeonyesha wazi kuwa Spika na Wabunge ni wapotoshaji wakubwa. Tatizo ni wabunge kulipwa posho mbili na sio kulipwa posho moja.

Ufafanuzi alioutowa:-

1. Posho walizotoa Takukuru kwa wabunge hazi kutolewa mara mbili. Ofisi ya Bunge haikuwalipa posho wabunge ku attend seminar hiyo. Kwa hiyo ni Takukuru tu ndio iliyowalipa.

2. Posho zinazochunguzwa na Takukuru ni zile zinazolipwa kwa Kamati za Bunge ambazo kwanza hulipwa na Bunge na baadae Kamati zikienda kufanya uchunguzi na mahojiano na wizara na mashirika hudai tena posho hizo hizo. Hii si takrima bali ni makosa.

3. Kwa sheria za Takukuru, kupokea pesa bila kuzitolea jasho ni rushwa.

4. Wabunge hawana kinga katika makosa ya rushwa. Wanayo kinga katika mambo yanayohusu shughuli zao za Bunge na matamshi wanayotowa Bungeni.

5. Ni Bunge ndio lilimuonba Hosea kufanya uchunguzi huo.

6. Yeye hanyimwi usingizi kama wabunge watampigia kura ya kutokuwa na imani naye. Yeye yuko pale kuwahudumia watanzania kwa kufanya kazi yake kwa uadilifu.

7. Wabunge waiachie Takukuru ifanye kazi yake.

8. Takukuru haikuwadhalilisha wabunge kwani yenyewe haikutangaza wabunge iliyowahoji bali ni wabunge wenyewe ndio walikimbilia kutangaza katika vyombo vya habari.

9. Hakuna Mtanzania yeyote aliye juu ya sheria.

Mimi personally nampongeza sana Dr. Hosea kwa ujasiri wake wa kuwa na msimamo. I am sure wabunge wamepata shock, walidhani wangeweza kumtingisha kwa kumtisha na sakata la Richmond lakini kumbe jamaa hatetereki. Kwa vipimo vyangu amefanikiwa kuvunja hoja zote za Sitta na wabunge.

"Nani hajui kama wewe pesa za mafisadi zimekufikia?.Suala la kupokea posho mara 2 limeanza leo?.Basi wachunguze tangia bunge limeanza. Na je yale maazimio 23 akiwemo Osea kujihuzulu imekuaje kugongona na ilo la posho za wabunge, kwani osea amekuwa mkuu wa takukuru leo, alikuwa wapi siku zote?.Wewe ni mmojawapo wa mafisadi.
 
naunga mkono hatua za TAKUKURU kuwachunguza wanaopokea posho mara mbili..hakuna ubabaishaji hapa kama umepokea posho mara mbili na ukijua kwa dhati umekwisha pokea posho mara ya kwanza huo ni wizi...haina definition nyingine zaidi ya hiyo...huo ni wizi tu..simple mwakyembe na wenzako kubalini kuhojiwa acheni makelele hayatawasaidia otherwise no sooner we will clasify you all as wafa maji.
 
"Nani hajui kama wewe pesa za mafisadi zimekufikia?.Suala la kupokea posho mara 2 limeanza leo?.Basi wachunguze tangia bunge limeanza. Na je yale maazimio 23 akiwemo Osea kujihuzulu imekuaje kugongona na ilo la posho za wabunge, kwani osea amekuwa mkuu wa takukuru leo, alikuwa wapi siku zote?.Wewe ni mmojawapo wa mafisadi.

mawazo ya kizamani sana haya...
 
.

Mimi personally nampongeza sana Dr. Hosea kwa ujasiri wake wa kuwa na msimamo. I am sure wabunge wamepata shock, walidhani wangeweza kumtingisha kwa kumtisha na sakata la Richmond lakini kumbe jamaa hatetereki. Kwa vipimo vyangu amefanikiwa kuvunja hoja zote za Sitta na wabunge.

Mimi pia abiria wa basi lako... Wabunge wamechemsha big time!
 
Nadhani hukusikiliza press conference ya Dr. Hosea. Kwa kweli katoa maelezo mazuri sana ya kujibu hoja zote walizotoa wabunge. Imeonyesha wazi kuwa Spika na Wabunge ni wapotoshaji wakubwa. Tatizo ni wabunge kulipwa posho mbili na sio kulipwa posho moja.

Ufafanuzi alioutowa:-

1. Posho walizotoa Takukuru kwa wabunge hazi kutolewa mara mbili. Ofisi ya Bunge haikuwalipa posho wabunge ku attend seminar hiyo. Kwa hiyo ni Takukuru tu ndio iliyowalipa.

Ni kwa taratibu gani ya kisheria TAkukuru wanatakiwa kutoa posho kwa wabunge?
2. Posho zinazochunguzwa na Takukuru ni zile zinazolipwa kwa Kamati za Bunge ambazo kwanza hulipwa na Bunge na baadae Kamati zikienda kufanya uchunguzi na mahojiano na wizara na mashirika hudai tena posho hizo hizo. Hii si takrima bali ni makosa.

hawa wanaotoa hizi posho kwa wabunge ni kina nani? wanazitoa wapi na katika fungu gani? Na kwanini wakidaiwa na wabunge wasigome?

3. Kwa sheria za Takukuru, kupokea pesa bila kuzitolea jasho ni rushwa.

Hiyo sheria imepitwa na wakati, mtu akikupa zawadi atakuwa amekupa rushwa? Basi wengi wetu humu tuna hatia ya kupokea zawadi!

4. Wabunge hawana kinga katika makosa ya rushwa. Wanayo kinga katika mambo yanayohusu shughuli zao za Bunge na matamshi wanayotowa Bungeni.

Wabunge wakiwa bungeni hakuna mahakama inayoruhusiwa kuwachunguza au kufanya uchunguzi wowote bila idhini ya Spika. Siyo kuombwa na Katibu wa Bunge. Bunge likikaa hakuna chombo cha dola kinachoweza kuleta hata summons ya kumuita mbunge yoyote. Sasa TAKUKURU wamepata wapi nguvu ya kuwaita wabunge kutoka kwenye kikao cha bunge kwenda kufanya uchunguzi wao? Soma sheria ya Haki, Madaraka na Kinga ya Bunge Ibara 5 na ya 11!

5. Ni Bunge ndio lilimuonba Hosea kufanya uchunguzi huo.

Hata kama hilo ni kweli, wanapoanza uchunguzi wao wanatakiwa watoe taarifa kwa Spika. Sheria inasema hilo haliwezekani "without Speaker's leave"!

6. Yeye hanyimwi usingizi kama wabunge watampigia kura ya kutokuwa na imani naye. Yeye yuko pale kuwahudumia watanzania kwa kufanya kazi yake kwa uadilifu.

Wabunge hawahitaji kumpigia kura yeye kwani hawamthibitishi uteuzi wake. WAbunge wataipigia kura serikali! Yaani, kutokuwa na imani na waziri mkuu. Sasa JK itabidi achague kumtosa Hosea au serikali yake iporomoke tena sababu ya kiburi cha watu wanaofikiri wako juu ya sheria.

7. Wabunge waiachie Takukuru ifanye kazi yake.

Hilo ni kweli, lakini ifanye kazi yake kisheria. Na hilo ni kusitisha uchunguzi wao sasa hivi, kuomba kibali kwa Spika wanapomtaka mbunge yoyote kutoa ushirikiano wakati kikao cha bunge kinaendelea. Nje ya hapo, wao ndio wamejinyanyua juu ya sheria.

8. Takukuru haikuwadhalilisha wabunge kwani yenyewe haikutangaza wabunge iliyowahoji bali ni wabunge wenyewe ndio walikimbilia kutangaza katika vyombo vya habari.

Imewadhalilisha wabunge kwa kufanya uchunguzi wakati kikao cha bunge kinaendelea bila ruhusa ya Spika.

9. Hakuna Mtanzania yeyote aliye juu ya sheria.

Na hilo linamjumuisha Hosea na Pinda. Kama ingekuwa kweli wanatawala kwa sheria Pinda alitakiwa kujiuzulu siku ile alipotoa ruhusa ya watu kujichukulia sheria mkononi utadhani hiyo sheria ni mapendekezo ya aina fulani.

Mimi personally nampongeza sana Dr. Hosea kwa ujasiri wake wa kuwa na msimamo.

Misimamo mingine siyo ya kupongeza ni ya kubeza. Msimamo wa kudai ana madaraka ambayo hana siyo msimamo wa kupongezwa.

I am sure wabunge wamepata shock, walidhani wangeweza kumtingisha kwa kumtisha na sakata la Richmond lakini kumbe jamaa hatetereki. Kwa vipimo vyangu amefanikiwa kuvunja hoja zote za Sitta na wabunge.

Wabunge wakikubali kushindwa mbele ya TAKUKURU na wakapigishwa magoti then the parliament has officially become irrelevant!. Hosea hawezi kutunishia misuli bunge akabakia alivyo!
 
Back
Top Bottom