KERO POSHO ya KUJIKIMU: Halmashauri ya USHETU, Shinyanga, Imewalipa waajiriwa wapya pesa PUNGUFU

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Baada ya Serikali kutoa fedha kwa ajiri ya malipo ya posho za kujikimu kwa waajiriwa wapya wa mwaka 2026.
Hali imekuwa tofauti katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu, mkoani Shinyanga.
Ambapo watumishi wapya walio chini ya Idara ya Afya na Lishe wamelipwa pesa pungufu tofauti na miongozo ya serikali inavyotaka.

Baada ya malipo hayo kufanyika tarehe 01/07/2026, watumishi wengi walishangaa kukuta pesa iliyowekwa kwenye account zao ni tofauti na muongozo wa fedha za kujikimu.
WEngi wamelipwa kati ya tsh 500, 000 hadi tsh 680,000. Haijarishi Elimu yako ni shahada, stashahada au cheti.

Hali hii ni tofauti na halmashauri nyingine ambapo wengi wamelipwa kati ya shilingi 900,000 na 1, 000,000tsh.
Viongozi wa idara ya afya na Lishe walipoombwa kutoa ufafanuzi walikwepa kwa kuwaambia watumishi waandike barua kujieleza ni wapi walipopunjwa.
Hii imeonekana ni njia ya kuwafanya watumishi hawa wakate tamaa kufuatilia fedha zao.
Kwani barua zinaweza kuchukua muda mrefu sana kujibiwa.

Tunaomba Serikali itusaidie sisi watumishi tuweze kupata fedha zetu zote kama inavyotakiwa.

Tunaomba pia serikali ichunguze halmashauri hii ya Ushetu kwani kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu hasahasa kwenye fedha za kujikimu.
Na watumishi wanapolalamika wanapokoea vitisho kuwa watahamishiwa kwenye maeneo ya vijijini.

TUNASHUKURU.
 
Weka namba ya Mkurugenzi wa Ushetu hapa..Uje ushuhudie ukuu wa Serikali ya JF au unataka usaidiwe na Serikali ya CCM?!!!
 
Huo muongozo unasema ulipwe shilingi ngapi kwa ajili ya posho ya kujikimu kwa certificate, diploma na degree??
 
Back
Top Bottom