Ni takribani miezi miwili na nusu tangu Bunge letu tukufu la Jamhuri ya Muungano liliopotisha Bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2021/2022 ambapo na mambo mengine lilipisha watendaji wa kata kulipwa posho za madaraka na Halmashauri na malipo hayo yakawekwa kwenye mabaadiliko (Ammendement) ya sheria ya fedha ya 2021/2022, bado kiza kikuu kimetanda kwenye ulipwaji wa shtaiki hizo kwa watendaji wa kata.
Mpaka sasa Halamshauri zilizolipa stahiki hizo kwa miezi ya July na August hazifiki hata 25 katika jumla ya Halmashauri karibia 184 zilizopo nchi nzima.
Watendaji wanapofuatilia huwa wanapewa majibu yasiyoridhisha yanayoonesha kwamba wakurugenzi wanamdharau Mh. Waziri wa TAMISEMI aliyeagiza stahiki hizo ziwe zinalipwa kabala ya Tarehe 25 ya kila mwezi. Wapo wanaojibu wanasubiri waraka , wapo wanaosema kwamba waziri hana uwezo nwa kuwafanya chochote hata wasipolipa na wapo wanaosema kwamba waziri hana ubavu wa kuwapangia namna ya kulipa siku na tarehe na hakuna cha kuwafanya.
Watendaji wamekata tamaa na hata morali ya kazi imeshuka sana kwani wao ndio wanaosimamia ukusanywaji wa mapato ya Halmashauri kwa jasho na damuna kwa mateso makubwa kwani hawana usafiri hali inayowafanya kukusanya mapato kwa kutumia usafiri wa kukodi kama vile pikipiki, lakini wakurugenzi kwa makusudi baadhi yao wameamua kuzikalia stahiki hizo ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya Bunge.
Maombi ya watendaji wa kata ni kwamba ni wakati sasa stahiki hizo zikalipwa moja kwa moja kutoka hazina na sio kupitia Halmashauri kwani Wakurugenzi wameonesha wazi hawana nia na hawataki kulipa stahiki hizo ambazo ni haki za watendaji wa kata.
Suala hili bila ya Mh. Rais Samiah Suluhu kuingilia kati hakika linaenda kuzorotehsa ufanishi wa kazi na kuwavunja moyo wa na matumaini kwa watumishi wa kwenye kada ya utendaji wa kata nnchi nzima.