Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
NGORONGORO CONSERVATION AREA AUTHORITY (NCAA)
JOB OPPORTUNITY
1.CONSERVATOR OF NGORONGORO
Salary and Remunaration:
SG 17 (NCAA Salary Grade), i.e. TZS 4,285,000/= X 121,000/= 4,500,000/= per month.
Halafu mnataka WABUNGE wabaki hivohivo?
Huko mbali sasa, hapa ofisini kuna baadhi ya watu wanalipwa hadi dollar 10,000 kwa mwezi na bado nyumba wanalipiwa, usafiri wanalipiwa na watoto wanasomeshewa, huwa natamani hata kulia sasa hao wanataka tena waongezewe hayo mapesa, mmmh sijui tutaishia wapi huko, si tutakuwa tunawazalishia wachache tu???
HII NI HATARI.....KATIBA IJAYO IELEZA NAMNA WABUNGE WATAKAVYOLIPWA MISHAHARA NA POSHO , C KUJIPANGIA KAMA WANAVYOFANYA SASA'''':lol::lol:
Wapandishe posho na huku kwingine ili na sisi tufaidi matunda ya uhuru kwa sababu kama ni kazi sote tunafanyasasa unafikiri tutafanyaje? Vita au?
Huko kungine ni jitihada zenu tu. Wizara ya Nishati na Madini ni serikali kwa 100%. Umeona maposho ya kufa mtu yanavyolipwa kule? Turudishe SCOPO. Watu wanahomola kikatili sana kwenye taasisi za UMMA.Wapandishe posho na huku kwingine ili na sisi tufaidi matunda ya uhuru kwa sababu kama ni kazi sote tunafanya
Waandishi wa habari waende mbali zaidi ya Wabunge. Waende EWURA, TPDC, TPA, SUMATRA, DAWASA, DAWASCO( pamoja na kuwa Dar haina maji), TANESCO( pamoja na umeme wa kugawana), TCRA,....Huko mbali sasa, hapa ofisini kuna baadhi ya watu wanalipwa hadi dollar 10,000 kwa mwezi na bado nyumba wanalipiwa, usafiri wanalipiwa na watoto wanasomeshewa, huwa natamani hata kulia sasa hao wanataka tena waongezewe hayo mapesa, mmmh sijui tutaishia wapi huko, si tutakuwa tunawazalishia wachache tu???
Nimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Msimamo wangu: Kupandisha posho za wabunge ni ukichaa na kutojali Hali ya Nchi
by zittokabweNimeshtushwa sana na taarifa za kupandishwa kwa posho za vikao kwa Wabunge. Nimeshtushwa zaidi kwamba Posho hizi zimeanza kulipwa katika mkutano wa Bunge uliopita kabla hata Rais hajaamua maana maslahi yote ya Wabunge huamuliwa na Rais Baada ya kupokea mapendekezo ya Bunge kupitia Tume ya Bunge.
Wabunge wote watambue kwamba kuamua kujipandishia posho zao bila kuzingatia Hali ya maisha ya mwananchi wa kawaida ni usaliti usio na mfano. Mbunge yeyote ambaye anabariki Jambo hili au anaishi hewani haoni tabunza wananchi au ni mwizi tu na anaona Ubunge ni Kama nafasi ya kujitajirisha binafsi.
Kwa Wabunge wa Chadema, wajue uamuzi kuhusu posho ni uamuzi wa chama na ni uamuzi wa kisera. Mbunge yeyote wa Chadema anayepokea posho za vikao anakwenda kinyume na maamuzi ya sera za chama tulizoahidi wananchi wakati wa uchaguzi. Nimemwomba Katibu Mkuu wa chama kuitisha kikao maalumu cha Kamati Kuu ya chama kujadili suala hili.
Toka tarehe 8 juni mwaka 2011 nilikataa kupokea posho za vikao. Popote ninapohudhuria vikao huomba Risiti ya fedha ninazokataa. Baadhi ya Wabunge Kama Januari Makamba wamekataa posho na hata kwenye semina ya kamati ya nishati alikataa na tumeona kwenye vyombo vya habari jina lake likiwa limekatwa ilhali viongozi wakubwa kabisa wamechukua posho.
Nampongeza kijana mwenzangu kwa uzalendo huu. Nawataka wabunge wengine wenye Moyo wa dhati kukataa sio tu ongezeko hili la posho Bali posho yote ya vikao. Kwa nini mbunge akubali kulipwa kwa kukaa?
Tazama nchi hii, juzi serikali ilipokea Msaada wa tshs 20bn kwa ajili ya Sensa ya mwakani wakati wabunge wanalipwa 28bn Kama posho za kukaa tu.
Tanzania inaagiza gesi ya matumizi ya nyumbani kutoka nje kwa kutumia mamilioni ya dola za kimarekani. Kuwanda cha kutengeneza LPG kinagharimu tshs 35bn tu, Wabunge peek Yao kwa mwaka wanatumia 28bn kwa posho za kukaa tu achilia mbali mishahara na marupurupu mengine.
Ipo siku Watanzania watatupiga mawe kwa usaliti huu dhidi yao.
Hii issue ya posho sasa ni mtaji wa kisiasa kwa ccm wameongeza ili wapate pa kuwasema wapinzani kama wewe si mgeni wa siasa za bongo nafikiri utakumbuka ruzuku za vyama vya siasa zinavyoleta mitafaruku kwenye vyama hivyo. Sasa hivi ccm inajaribu kila mbinu kuinyamazisha pipoz na hapa kwenye posho wanatekeleza hilo nafikiri utayakumbuka yaliyoipata nccr mageuzi miaka ile.Here u can clearly see how human being we are full of psychological biases, we want to see things in way that please us and not in reality.
Hii mada kwa kuwa cdm nao wamelamba posho utaona washabiki wa cdm wanajaribu kuikwepa, wengine wanasingizia eti ccm ndo wamepitisha.
Mbowe alidanganyia shangingi kuwa atarudisha kumbe wapi bana.
Zitto ur right, iko siku watu watauona unafiki huu wa hali ya juu.
Tumepata tulicholipia! Si mliwachagua wenyewe sasa mwalalama nini?Wizi mtupu huu!! Nadhani tulifute Bunge, kwanza halina tija yeyote zaidi ya kufuja fedha zetu...