Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

Posho za wabunge zapanda kimyakimya!

Taarifa za posho za wabunge kuongezwa kwa asilimia 150 kutoka sh. 70,000 hadi 200,000/= kumenistua sana, na nadhani kumewastua pia walalahoi wengi nchini. Haiingii akilini kuona 'wawakilishi' wetu hao wakipendekeza , kupitisha na kujilipa maslahi ya kufuru kama hayo, bila mapendekezo hayo kupitiwa na kukubaliwa na chombo huru kama ilivyo kwa watumishi wengine wa sekta ya umma. Na kibaya zaidi tendo hilo la fedheha linafanyika huku kukiwa na madai ya muda mrefu ya wafanyakazi nchini ya kutaka viwango vya mishahara viboreshwe kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi na mfumuko wa bei, lakini wamekuwa wakizimwa kila uchao.

Kwangu mimi kitendo hicho nakitafsiri kuwa ni ufisadi uliotukuka na unaonyesha jinsi 'wawakilishi wetu' wanavyoshupalia kuyawakilisha matumbo yao wakiwa mjengoni kuliko kuwakilisha matakwa ya waliowachagua, pamoja na usanii wao wa kujifanya kulia kilio cha mamba wakijidai kupayuka kutetea wananchi! kumbe ni unafiki na uzandiki mkubwa ambao hautasahaulika kwa kipindi kirefu.

Hivi inashindikanaje kuweka mamlaka ya kudhibiti matakwa ya hao waheshimiwa ambao, wamegoma hata kuruhusu stahili zao kukatwa kodi halali za serikali kama ambavyo wafanyakazi wa mihimili mingine ya dola. Wao ni nani hasa na wana tofauti gani na wengine! Kibaya zaidi wao ni wepesi wa kujitwika madaraka hata ya ukaguzi katika taasisi nyingine za serikali zinavyotumia fedha za umma kupitia kamati mbalimbali za bunge!?. Vinginevyo hii dhana na Check and balance kwa Bunge ikoje?
 
Vidole vikiungua unaokoa vya kwako, nao pia wanajikakamua na ugumu wa maisha ila wanakosea maana hawangalii waliowaweka mahali walipo sasa, ni sawa na Jk alivyowasahau waliomuweka madarakani ndio maana Loawasa ilibidi amukumbushe juzi
 
Taarifa za posho za wabunge kuongezwa kwa asilimia 150 kutoka sh. 70,000 hadi 200,000/= kumenistua sana, na nadhani kumewastua pia walalahoi wengi nchini. Haiingii akilini kuona 'wawakilishi' wetu hao wakipendekeza , kupitisha na kujilipa maslahi ya kufuru kama hayo, bila mapendekezo hayo kupitiwa na kukubaliwa na chombo huru kama ilivyo kwa watumishi wengine wa sekta ya umma. Na kibaya zaidi tendo hilo la fedheha linafanyika huku kukiwa na madai ya muda mrefu ya wafanyakazi nchini ya kutaka viwango vya mishahara viboreshwe kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi na mfumuko wa bei, lakini wamekuwa wakizimwa kila uchao.

Kwangu mimi kitendo hicho nakitafsiri kuwa ni ufisadi uliotukuka na unaonyesha jinsi 'wawakilishi wetu' wanavyoshupalia kuyawakilisha matumbo yao wakiwa mjengoni kuliko kuwakilisha matakwa ya waliowachagua, pamoja na usanii wao wa kujifanya kulia kilio cha mamba wakijidai kupayuka kutetea wananchi! kumbe ni unafiki na uzandiki mkubwa ambao hautasahaulika kwa kipindi kirefu.

Hivi inashindikanaje kuweka mamlaka ya kudhibiti matakwa ya hao waheshimiwa ambao, wamegoma hata kuruhusu stahili zao kukatwa kodi halali za serikali kama ambavyo wafanyakazi wa mihimili mingine ya dola. Wao ni nani hasa na wana tofauti gani na wengine! Kibaya zaidi wao ni wepesi wa kujitwika madaraka hata ya ukaguzi katika taasisi nyingine za serikali zinavyotumia fedha za umma kupitia kamati mbalimbali za bunge!?. Vinginevyo hii dhana na Check and balance kwa Bunge ikoje?
Wazo ni zuri,ila pa kuanzia wapi?

Rais si ndo anawalipa hao kwa niaba ya wananchi?

Wabunge hawawezi kujipunguzia mishahara,ni wachache wenye moyo huo na hawawezi kushinda kwa hiyo hoja bungeni.

Kwa upande wa Rais,yeye hana shida kwasababu hiyo nikama anatoa hongo ambayo ni ndirect ama imehalalishwa na katiba.

Bunge ni mojawapo ya silaha kubwa tu ya rais haswa ukitilia maanani kuwa chama chake ndicho chenye majority,hivyo upinzani ni kama wana bahati kuwemo humo na kulipwa kama CCM wanavyolipwa.

Kwa hiyo kwanza jaribu kufikiri pa kuanzia...
 
Jamani wabunge ni waheshimiwa sana - hakuna tofauti na miungu wadogo. Hakuna ubaya hata hiyo sitting allowance ingefika 500,000 kwa siku. Na nawaambia kabla ya 2015 itafika kiwango hicho.
 
HUU Ni UNYAMA!! HII HAIKUBALIKI! HUU NI UKATILI! HUU NI UJAMBAZI!! MBUNGE HAWEZI KULIPWA SHS 330,000 kwa siku kama posho, achilia mbali mshahara million 12 kwa mwezi kama mshahara na marupurupu mengine!! WATANZANIA WAKE UP!!
 
HALAFU ISITOSHE ASILIMIA KUBWA YA WABUNGE KICHWANI HAKUNA KITU! TuNAWAONAGA JINSI WANAVYO CHANGIAGA PUMBA KWENYE VIKAO VYA BUNGE.
 
am fedup na hili li-gvt letu. jamani can u imagine posho inapanda kwa 130,000/= wakati profesional teachers hadi leo hawajalipwa malimbikizo yao kwa madai kuwa serikali haina pesa. jamani hivi kweli inaingia akilini. Eti maisha ya dodoma yapo juu! ina maana yapo juu kwa hao waheshimiwa tu wanaokuja kwa msimu ila kwa wakazi wa dodoma yapo chini. inaudhi sana jamani.
 
Ok, Wameongeza posho kutokana na kupanda kwa ghalama za maisha, lakini tatizo langu kwa nini wameongeza kwenye sitting allowance?! Sitting allowances zina uhusiano gani na kupanda kwa ghalama za maisha?! Nadhani ka kuongeza wangepandisha kwenye Substance Allowance ambayo inajumuisha chakula na makazi!! Kwa mtazamo wangu wameamua kuongeza sitting allowance ili wabunge wanaozipinga wasiweze kupata, na kama wangeongeza kwenye substance allowance wabunge wote wangestahili kuzipokea..
 
Hapa ndio mtakapotia akili kama nyie kweli ni great thinkers muone kuwa CHAMA CHA SILAHA a.k.a magwanda au chama cha kikabila cha wachaga! HAKINA MAANA ! wote wapo katika KULIGANDAMIZA taifa hili! wote pale bungeni wapo kwa maslahi yao na si ya wananchi wa Tanzania.

Nawashangaa wanaowashabikia hawa watu ! kama kweli wanaona uchungu huo wanaijitia nao basi wangekuwa ni wa kwanza kupinga hizi posho na wakatuachia sisi magamba tuonekane wabaya! wote baba mmoja mama mmoja! na inaonesha dhahiri kwamba watu hawa WANATAFUTA UMAARUFU WA BURE ! ...kazi kwenu great thinkers! ... nyie mwasusa wenzenu walaa!

“So do not weaken and do not grieve, for you will indeed be superior if you are truly believers.” [Al-Quran 3:139]

Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema walivyokuwa wakipinga posho hizo wakati zilivyokuwa Sh70,000 waandishi wa habari walichukua suala hilo kama ajenda ya Chadema, hivyo kupandishwa kwa posho hizo ni matokeo ya watu kuwapuuza walivyokuwa wakizipinga.

Huyu Mbowe ni mnaafik mkubwa, sio yeye aloulizwa siku ile TBC kipindi kilichorushwa live asubuhi kuhusu posho zao kuweka kama collateral BAnk kwa mikopo walochukuwa? na List ilikuwepo akaanza kukwepa na kusema "mtangazaji kama serikali ilivosema, tuungane wote kujenga serikali yetu na hili jambo la posho ni dogo sana" HUKU William Lukuvi akigeuza geuza kiti chake kumkebehi Mbowe kwa kula M A T A P S H I yake! wote kama nilivosema awali kuwa wapo kwa maslahi yao wenyewe na moreover wanatafuta umaarufu kwa kupitia migongo ya walalahoi wenye shida! nawashangaa wanaomuunga mkono mpuuzi huyu!

“So do not weaken and do not grieve, for you will indeed be superior if you are truly believers.”
[Al-Quran 3:139]
 
Back
Top Bottom