Taarifa za posho za wabunge kuongezwa kwa asilimia 150 kutoka sh. 70,000 hadi 200,000/= kumenistua sana, na nadhani kumewastua pia walalahoi wengi nchini. Haiingii akilini kuona 'wawakilishi' wetu hao wakipendekeza , kupitisha na kujilipa maslahi ya kufuru kama hayo, bila mapendekezo hayo kupitiwa na kukubaliwa na chombo huru kama ilivyo kwa watumishi wengine wa sekta ya umma. Na kibaya zaidi tendo hilo la fedheha linafanyika huku kukiwa na madai ya muda mrefu ya wafanyakazi nchini ya kutaka viwango vya mishahara viboreshwe kwa kuzingatia hali halisi ya uchumi na mfumuko wa bei, lakini wamekuwa wakizimwa kila uchao.
Kwangu mimi kitendo hicho nakitafsiri kuwa ni ufisadi uliotukuka na unaonyesha jinsi 'wawakilishi wetu' wanavyoshupalia kuyawakilisha matumbo yao wakiwa mjengoni kuliko kuwakilisha matakwa ya waliowachagua, pamoja na usanii wao wa kujifanya kulia kilio cha mamba wakijidai kupayuka kutetea wananchi! kumbe ni unafiki na uzandiki mkubwa ambao hautasahaulika kwa kipindi kirefu.
Hivi inashindikanaje kuweka mamlaka ya kudhibiti matakwa ya hao waheshimiwa ambao, wamegoma hata kuruhusu stahili zao kukatwa kodi halali za serikali kama ambavyo wafanyakazi wa mihimili mingine ya dola. Wao ni nani hasa na wana tofauti gani na wengine! Kibaya zaidi wao ni wepesi wa kujitwika madaraka hata ya ukaguzi katika taasisi nyingine za serikali zinavyotumia fedha za umma kupitia kamati mbalimbali za bunge!?. Vinginevyo hii dhana na Check and balance kwa Bunge ikoje?