Mi nshawahi kukuta vinywaji.Hata polisi kuna kaunta ila hakuna vinywaji
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mi nshawahi kukuta vinywaji.Hata polisi kuna kaunta ila hakuna vinywaji
Hata iweje maumivu haya ambukizi!...
Umefanya utafiti wa kutosha na ukajiridhisha kwamba kweli hayaambukizi?
(Joni) dogo wa darasa la kwanza kafika shule akaanza kulalamika kwa mwalimu wake wa darasa kwamba la kwanza si saizi yake na anataka arushwe hadi darasa la tatu kwa maana anaamini ana akili kumzidi hata dada yake ambaye yuko darasa la tatu. Ticha wa darasa kuona dogo kazidi kupiga kelele na kusumbua akamchukua akaenda naye kwa mwalimu mkuu. Ticha wa darasa: Huyu mtoto hata simuelewi, darasani anapiga kelele kwamba anataka apelekwe na darasa la tatu kwamba la kwanza si saizi ya akili zake.
Ticha mkuu akapigwa: Ngoja nimuulize maswali ya la tatu akishindwa arudi darasani na akae atulie vinginevyo acheze na bakora. We mtoto, tatu mara tatu ngapi?
Joni: Tisa mwalimu.
Ticha mkuu: Tisa mara 4?
Joni: 36
Basi ticha mkuu akamkandamiza dogo maswali kibao ya darasa la tatu dogo akawa anapatia.
Ticha mkuu: mwalimu mi naona kijana yuko sawa, hebu mpeleke tu darasa la tatu, fanyeni utaratibu wa kumuingiza kwenye atendensi ya darasa la tatu.
Ticha wa darasa: sawa mwalimu ila ngoja nimuulize maswali zaidi. Joni ni kitu gani ambacho ng'ombe anavyo vinne na mimi ninavyo viwili?
Joni: Miguu
Ticha: Kitu gani unacho ndani ya kaptula yako ya shule ambacho mimi sina? (Ticha mkuu akashtuka kuhusu hilo swali)
Joni: Mifuko
Ticha: Kitu gani mbwa anakifanya halafu binadamu anakikanyaga?
Joni: Kujisaidia haja kubwa njiani. (ticha mkuu mdomo ukawa uko wazi anashangaa)
Ticha: Kitu gani ukikiingiza ndani kinakuwa kigumu na cha rangi kama nyekundu au pink lakini kikitoka kinakuwa kilaini na kinanata nata? (Ticha mkuu jicho likamtoka lakini kabla hajamzuia dogo kujibu dogo akatoa jibu)
Joni: Big G.
Ticha: Kitu gani mwanaume anakifanya akiwa amesimama, mwanamke akiwa amekaa na mbwa akiwa kasimama kwa miguu mitatu?
Joni: Kujisaidia haja ndogo.
Ticha mkuu akaanza kutetemeka.
Ticha: Neno gani linaanza na herufi K na linaishia na herufi A ambalo huleta raha sana watu wakilitamka?
Joni: KULA
Ticha mkuu akavuta pumzi ndefu halafu akazishusha akasema: Mwalimu naona mpeleke Joni darasa la tano. Maswali yote sita ya mwisho mimi mwenyewe nimekosea majibu yake.
Takwimu zinaonyesha kwamba, 8 kati ya kila watu 10 wanaojamba hujifanya si wao na kuuliza "Jamani nani tena kachafua hewa?"
Huwa naenjoy sana kusoma yaliyoandikwa nyuma ya daladala hasa ninapokuwa kwenye foleni. Misemo maarufu
ya kwenye daladala.
1.Yatima hadeki
2.Utamu wa chips mimba
3.Ukitaka kujua ugumu wa kudai kopesha ukweni
4. Usiyempenda kaja
5. Kobe hapimwi joto
6. Acha kazi uone kaz kupata kaz
7. Ukichezea koki utalowa
8. Heshima pesa kipara kovu tu!
9. Mtumbwi hauna saitmira.
9. Silaha pesa bastola mzigo
10. Hata uoge mjini huendi
11. Chezea mshahara usichezee kazi.
12. Ukiona manyoya ujue kishaliwa
13. Ikisimama Panda
14. Pombe pombe tuu kunywea bar mbwebwe
15. Njia ya chooni haioti nyasi
16. Likizo ya maskini ugonjwa
17. When i grow up i want to be a scania
18. Hata bibi alikuwa binti
19. Kisigino hakikai mbele
20. Kama mapenz pesa kaolewe na benki
21. Hata barabara ina matuta lakin huwez panda viazi
22. Mavi hayana miba lakin ukikanyaga lazma uchechemee
23. Paka haishi kwa msela
24. Ukipendwa ujue kuna boya kaachwa
25. Tako nalo lina nywele lakin hazinyolewi
26. Mchana nzi ucku mbu
27. Ucmshangae funza kukata viuno ndio mwendo wake
28. Kama umelipenda(gari) bonyeza nyota liwe lako
29. Supermarket hawauzi mkaa
30. We nisubiri mi nakungoja.
31. Zetu dagaa kuku tamaa
32. Hata uwe na heshima vipi huwezi kumpokea askari bunduki.
Lakini kumbuka ..... Kujenga nyumba kwa wakwe ni sawa na kujenga nyumba kwenye hifadhi ya barabara.
Ha ha ha ha watu sijui mnafikiria nini