Posta yatimua wakurugenzi.. kisa JF!

Posta yatimua wakurugenzi.. kisa JF!

Habari ambazo zinaingia mida hii kutoka Dar zinasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta baada ya kukutana leo imeamua kuwatimua wakurugenzi wake watatu kwa kile kinachoaminika ni kuvujisha siri za shirika hilo hususan zihusiano na vitendo vya kifisadi.

Habari za ufisadi kwenye shirika hilo zilitemwa kwenye mtandao huu wa JF siku chache zilizopita. Hata hivyo kwa wale "wanaojua" habari hizi hazikutoka kwa afisa yeyote wa juu ndani ya shirika hilo isipokuwa baadhi ya Watanzania ambao wamechoshwa na hujuma na vitendo vya kifisadi.

Kama ufukuzwaji huo utathibitishwa hii itakuwa ni mara nyingine ambapo JF imetumiwa kisingizio cha kufukuza watu ili kutishia watumishi wa umma wasifichue uovu kwenye taasisi za umma na ambazo ni nyeti. Miezi michache iliyopita shirika la ndege la ATC nalo lilitimua watumishi wake watano kwa kisingio cha kuvujisha siri za ununuzi wa dege la Airbus na vitendo vya kifisadi ndani ya shirika hilo.

Wakati huo huo mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Tanzania nacho kimemfuta kazi mmoja wa wahadhiri wake waandamizi kwa kile amacho viongozi wa chuo hicho wanadai kuwa ni "pressure" toka juu hasa baaada ya mhadhiri huyo mwishoni mwaka jana kujitokeza hadharani na kumnyoshea kidole cha ufisadi mmojawapo wa mawaziri na kumtaka ajiuzulu.

Kama tabia hii ya "kufukuza fukuza" itaendelea bila kukomeshwa mara moja, Taifa la Tanzania litakuwa limeanzisha utawala wa vitisho na utamaduni wa kuziba habari za vitendo vya kifisadi kwa kutishia retaliation kwa mtu yeyote yule.

Hadi hivi sasa haijajulikana ni kwa kiasi gani sheria ya "Whistleblowing" imefikia na ni lini sheria hiyo itaanza kuwalinda Watanzania ambao wanaibua vitendo vya kifisadi, kuhujumu uchumi, rushwa, na ukiukwaji wa maadili katika sehemu zao za kazi.
Kweli hii ni kama kurudisha nchi yetu nyuma!Lakini kama ilivyo kawaida maoni yangu yako pale pale..and thats the CORE...That it is for nobody's ineterest if there is no substantial changes to the constitution of ours!Kama kweli watanzania tunaitakia nchi yetu mema then bila mabadiliko ya kikatiba tunacheza..enzi zile wakiita "makida"
 
kada SUBIRI THANKS YANGU NIKIFA KWA HIYO COMM YAKO
 
Ni vigumu kumjua mvujishaji habari kwani hakuna mtu anayeweza kujiweka wazi kuwa mimi nasema hivi hasa ktk level hiyo inayoongelewa.

Kama kuwapiga chini inawezekana kwa kukisia kuwa fulani na fulani wanajua issue hii na hawajalambishwa(mgawo) chochote ktk deal hizi za kifisadi ,basi wao ndio watakuwa wametuchoma/wamesema.
 
Jambo la muhimu ni kutekelezwa kwa mapendekezo yaliyotolewa na wafichua uovu. Nadhani Mhe. pinda amepata mahali pazuri pa kuanzia kwani kufukuza Wakurugenzi eti wamevujisha siri ni ufisadi pia. Nilitegemea wafukuzwe waliotuhumiwa ili kupisha uchunguzi.
 
Maisha haya labda MUNGU aje kuingilia kati na kuwasaidia hao waliofukuzwa kwa kutoa habari kwa JF!

Weekend njema kwa kila mtu!

Mwafrika wa kike.

Siku za leo MUNGU anatumia watu kutenda mambo,na watu ndo sisi kwa hiyo kazi buti tuendeleee.
Nakumbuka ule mkanda wa Nigeria uitwayo THE PRICE uliochezwa na Pastor KENNY,Kuna maneno ya kutia hamasa alisema "COUNT IT JOY WHEN YOU FALL INTO DIVERSY TEMPTATIONS,KNOWING THAT THE TRYING OF YOU FAITH PRODUCES PATIENCE/STEADFASNESS".Tuko duniani na hatuwezi kukwepa changamoto nyingi hasa ktk kufichua uovu uliokithiri ktk haya mashirika ya umma.

Kila kitu chema duniani mara nyingi hupitia changamoto mbalimbali ili kiweze kuthibitika,na mageuzi siku zote yana gharama yake,yanaweza kukugharimu uhai wako,kazi yako,pesa na hata kukufanya uwe maskini.

Nakumbuka mwalimu J.K.Nyerere wakati anapigania uhuru wa TANGANYIKA,Aliwekewa pia masharti mawili na wakoloni ya kuchagua SIASA AU UALIMU ili wamdhoofishe ktk harakati zake za kudai uhuru,lakini hakukata tamaa na leo ni reference yetu ktk mambo mbalimbali ya maendeleo na uongozi ktk nchi hii.

Kweli lazima isemwe.Nchi na mashirika ya umma yanafukarishwa na watu wachache wasioitakia mema nchi hii.

Pia wakurugenzi waliopata masahibu,msikate tamaa,maisha ya mtu dira yake yote anayo muumba.Tumieni taaluma yenu,tafuteni kazi kwingine tuendeleze Taifa letu.
 
Kimsingi kutoa taarifa za kampuni yoyote bila ya kufuata utaratibu uliowekwa na kampuni ni kosa kubwa ktk Kampuni.Kama kweli walifanya hivyo wanastail kuadhibiwa.Lakini kama wanaona wameonewa pale tawini kwao wawasiliane na chama cha wafanyakazi kama sio wanachama waende mahakani wakatetee ulaji wao.Tafuteni wakili ili muwaonyeshe adabu hao waliowafukuza kwa sababu kama mmeonewa wajiandae kuwalipa mamilioni ya shilingi na wasifanye mzaha wakufukuza watu ovyo kama walikua hawana ushahidi wa kutosha.
 
Nadhani pia tungeiga mfano wa wenzetu wa nchi zilizoendelea kwa ku introduce 'whistle blowing policies' sehemu za kazi.
 
Habari ambazo zinaingia mida hii kutoka Dar zinasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta baada ya kukutana leo imeamua kuwatimua wakurugenzi wake watatu kwa kile kinachoaminika ni kuvujisha siri za shirika hilo hususan zihusiano na vitendo vya kifisadi.

jamani naomba kueleweshwa, kuna mashirika mawili tofauti, umesema bodi ya shirika la posta, lakini mnaongea kuhusu benki ya posta, haya si mashirika mawili tofauti? kwa sababu mwenyekiti wa bodi ya benki ya posta anaitwa kapelega ambaye ni muajiriwa wa shirika la posta.
little clarification please
 
Hapo ni rahisi Kukamata wapumbavu...
walio fukuzwa kazi warudishwe kazini haraka sana...na wewe ulie fukuza watu kazi acha kazi mara moja...
 
Kimsingi kutoa taarifa za kampuni yoyote bila ya kufuata utaratibu uliowekwa na kampuni ni kosa kubwa ktk Kampuni.Kama kweli walifanya hivyo wanastail kuadhibiwa.Lakini kama wanaona wameonewa pale tawini kwao wawasiliane na chama cha wafanyakazi kama sio wanachama waende mahakani wakatetee ulaji wao.Tafuteni wakili ili muwaonyeshe adabu hao waliowafukuza kwa sababu kama mmeonewa wajiandae kuwalipa mamilioni ya shilingi na wasifanye mzaha wakufukuza watu ovyo kama walikua hawana ushahidi wa kutosha.

This is only possible in a country which follows the rule of law and not a country which is run like a private company like ours.

Wengi humu wanaoinsist on procedures wanajua fika, the difficulties involved. Kama waziri MKUU anasema kwamba kupambana na mafisadi ni kazi ngumu kwa vile ni matajiri..wakati anawajua fika..what do you expect? Its a shame on all of us tunaofikiri kwamba we have a right to be more Tanzanians than our fellow men and women languishing in poverty!

Utakuwa ni ujinga na unafiki kutegemea kwamba wanaotenda maovu serikalini watayaexpose wenyewe! NEVER.
 
jamani naomba kueleweshwa, kuna mashirika mawili tofauti, umesema bodi ya shirika la posta, lakini mnaongea kuhusu benki ya posta, haya si mashirika mawili tofauti? kwa sababu mwenyekiti wa bodi ya benki ya posta anaitwa kapelega ambaye ni muajiriwa wa shirika la posta.
little clarification please

B.Kapelega ni Vice Chairman wa Board of Directors wa TPB lakini ni muajiriwa wa TPC, kazi yake huko ni Diretor wa Operations.Shirika linaloongelewa hapa ni TPB.
Mwenyekiti wa Bodi ya TPC ni Yona Killaghane ambaye ni Managing Director wa TPDC.
 
Mzee mwana k - Nashangaa kusikia wewe unajua kwamba wametimuliwa ila mimi binafsi naelewa kwamba hawa watu wamepewa likizo ya lazima ili kuendelea kutengenezewa visanga baada ya hapo ndo watimuliwe ila binafsi nadhani kabla ya watu hawa kupoteza kazi zao kwa kutetea mabillion ya walala hoi sisi kama wana JF twaweza kuokoa ajira zao na huyo jamaa kih nanihii huyo akanyea bakuri la Mr Richmond na wenzake,Tanzania ya leo sio ya jana - wote tulivalie njuga jambo hili.

Mnyonge mnyongeni tu ila sasaaaa Hakiiiiiiiiii yake MPENI!!ebo
 
Bodi za wakurungenzi zinatakiwa kubadili mtazamo wake sasa, badala ya kutimuwa wanaodaiwa kuvujisha siri napendekeza wawasimamishe wanaotuhumiwa na JF, na kuanzisha upelelezi wa kina kuthibitisha au kuwasafisha hapo watawini.

Balali alipo watimua Delloite wakaja Ernest & Young wakatoa uozo zaidi, ikawa issue kubwa zaidi.

wakati umefika ambapo waliopo bondeni wasirudi nyumbani, walioko darini wasishuke kuwachukua walio chini, maana muda wa kulindana umeisha.

Enyi wakurugenzi, shitukeni!
 
Mzee mwana k - Nashangaa kusikia wewe unajua kwamba wametimuliwa ila mimi binafsi naelewa kwamba hawa watu wamepewa likizo ya lazima ili kuendelea kutengenezewa visanga baada ya hapo ndo watimuliwe ila binafsi nadhani kabla ya watu hawa kupoteza kazi zao kwa kutetea mabillion ya walala hoi sisi kama wana JF twaweza kuokoa ajira zao na huyo jamaa kih nanihii huyo akanyea bakuri la Mr Richmond na wenzake,Tanzania ya leo sio ya jana - wote tulivalie njuga jambo hili.

Mnyonge mnyongeni tu ila sasaaaa Hakiiiiiiiiii yake MPENI!!ebo

.....na hilo ndiyo lilikuwa lengo kuu la mwanzisha thread hii ukisoma huko mwanzo.... by the way, karibu jamvini...

SteveD.
 
Kutoka katika chanzo cha habari cha kuaminika- ukweli ni kwamba so far NO ONE has been fired!. Lakini kuna tetesi kwamba baadhi ya management staff watakuwa suspended, watapewa barua za kusimamishwa kazi next week.
 
Back
Top Bottom