Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kweli hii ni kama kurudisha nchi yetu nyuma!Lakini kama ilivyo kawaida maoni yangu yako pale pale..and thats the CORE...That it is for nobody's ineterest if there is no substantial changes to the constitution of ours!Kama kweli watanzania tunaitakia nchi yetu mema then bila mabadiliko ya kikatiba tunacheza..enzi zile wakiita "makida"Habari ambazo zinaingia mida hii kutoka Dar zinasema kuwa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta baada ya kukutana leo imeamua kuwatimua wakurugenzi wake watatu kwa kile kinachoaminika ni kuvujisha siri za shirika hilo hususan zihusiano na vitendo vya kifisadi.
Habari za ufisadi kwenye shirika hilo zilitemwa kwenye mtandao huu wa JF siku chache zilizopita. Hata hivyo kwa wale "wanaojua" habari hizi hazikutoka kwa afisa yeyote wa juu ndani ya shirika hilo isipokuwa baadhi ya Watanzania ambao wamechoshwa na hujuma na vitendo vya kifisadi.
Kama ufukuzwaji huo utathibitishwa hii itakuwa ni mara nyingine ambapo JF imetumiwa kisingizio cha kufukuza watu ili kutishia watumishi wa umma wasifichue uovu kwenye taasisi za umma na ambazo ni nyeti. Miezi michache iliyopita shirika la ndege la ATC nalo lilitimua watumishi wake watano kwa kisingio cha kuvujisha siri za ununuzi wa dege la Airbus na vitendo vya kifisadi ndani ya shirika hilo.
Wakati huo huo mojawapo ya Vyuo Vikuu vya Tanzania nacho kimemfuta kazi mmoja wa wahadhiri wake waandamizi kwa kile amacho viongozi wa chuo hicho wanadai kuwa ni "pressure" toka juu hasa baaada ya mhadhiri huyo mwishoni mwaka jana kujitokeza hadharani na kumnyoshea kidole cha ufisadi mmojawapo wa mawaziri na kumtaka ajiuzulu.
Kama tabia hii ya "kufukuza fukuza" itaendelea bila kukomeshwa mara moja, Taifa la Tanzania litakuwa limeanzisha utawala wa vitisho na utamaduni wa kuziba habari za vitendo vya kifisadi kwa kutishia retaliation kwa mtu yeyote yule.
Hadi hivi sasa haijajulikana ni kwa kiasi gani sheria ya "Whistleblowing" imefikia na ni lini sheria hiyo itaanza kuwalinda Watanzania ambao wanaibua vitendo vya kifisadi, kuhujumu uchumi, rushwa, na ukiukwaji wa maadili katika sehemu zao za kazi.
Kadampinzani unajidhalilisha!
kada SUBIRI THANKS YANGU NIKIFA KWA HIYO COMM YAKO
Maisha haya labda MUNGU aje kuingilia kati na kuwasaidia hao waliofukuzwa kwa kutoa habari kwa JF!
Weekend njema kwa kila mtu!
Kimsingi kutoa taarifa za kampuni yoyote bila ya kufuata utaratibu uliowekwa na kampuni ni kosa kubwa ktk Kampuni.Kama kweli walifanya hivyo wanastail kuadhibiwa.Lakini kama wanaona wameonewa pale tawini kwao wawasiliane na chama cha wafanyakazi kama sio wanachama waende mahakani wakatetee ulaji wao.Tafuteni wakili ili muwaonyeshe adabu hao waliowafukuza kwa sababu kama mmeonewa wajiandae kuwalipa mamilioni ya shilingi na wasifanye mzaha wakufukuza watu ovyo kama walikua hawana ushahidi wa kutosha.
jamani naomba kueleweshwa, kuna mashirika mawili tofauti, umesema bodi ya shirika la posta, lakini mnaongea kuhusu benki ya posta, haya si mashirika mawili tofauti? kwa sababu mwenyekiti wa bodi ya benki ya posta anaitwa kapelega ambaye ni muajiriwa wa shirika la posta.
little clarification please
Mzee mwana k - Nashangaa kusikia wewe unajua kwamba wametimuliwa ila mimi binafsi naelewa kwamba hawa watu wamepewa likizo ya lazima ili kuendelea kutengenezewa visanga baada ya hapo ndo watimuliwe ila binafsi nadhani kabla ya watu hawa kupoteza kazi zao kwa kutetea mabillion ya walala hoi sisi kama wana JF twaweza kuokoa ajira zao na huyo jamaa kih nanihii huyo akanyea bakuri la Mr Richmond na wenzake,Tanzania ya leo sio ya jana - wote tulivalie njuga jambo hili.
Mnyonge mnyongeni tu ila sasaaaa Hakiiiiiiiiii yake MPENI!!ebo