Postal wamenikatalia kusafirisha nusu kilo ya kahawa mpaka kibali bila kuniambia kibali Cha nini

fareed uziel

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
657
Reaction score
710
Habari wakuu?

Kuna rafiki yangu aliniomba nimkaangie buni ya kahawa ya Kilimanjaro nimtumie ujerumani,sasa nimeenda pale postal EMS wamesema hawatumi kahawa mpaka kibali na wenyewe hawajui kinapatikana wapi.

Msaada wakuu kama kuna mtu anakijua hicho kibali Cha Nini na kinapatikana wapi anisaidie maana hii kahawa nisipoituma rafiki yangu atajua nimekula pesa yake bila kuamini changamoto iliyonikumba.

Dhl bei juu nimeshindwa.

IMG20220319084731.jpg
IMG20220319084956.jpg
 
Zamani nafikiri kibali cha kusafirisha vyakula na vifaa tiba pamoja na madawa kilikuwa kinatolewa na TFDA siku hizi nafikiri wanafanya hivyo TBS.
 
Habari wakuu?

Kuna rafiki yangu aliniomba nimkaangie buni ya kahawa ya Kilimanjaro nimtumie,sasa nimeenda pale postal EMS wamesema hawatumi kahawa mpaka kibali na wenyewe hawajui kinapatikana wapi?

Msaada wakuu kama kuna mtu anakijua hicho kibali Cha Nini na kinapatikana wapi anisaidie maana hii kahawa nisipoituma rafiki yangu atajua nimekula pesa yake bila kuamini changamoto iliyonikumba.

Dhl bei juu nimeshindwa
View attachment 2206242View attachment 2206243
Mkuu naamini wapeleka nje ya nchi. Kama niko sawa, basi kuna taratibu unazopaswa kufuata ili upate vibali (Mimi si mjuvi). Kuna baadhi ya nchi kama Australia ukipeleka vitu kama hivyo wanaviharibu vikitua tu nchi zao. Kuna sababu nyingi, mojawapo ni kuepuka magonjwa ya mazao na pia kusimamia ubora wa vyakula vyao. Ulipaswa ujishushe upate maelekezo hapo Posta. Usije ukawa ulinyanyua kibega, wakaamua kukuacha. Rudi tena, wao watakupa maelezo mazuri.
 
Hapana mkuu,hua sio mjuaji mkuu na hata nilivoandika huu Uzi sikulaumu mtu yoyote nataka nijue tu utaratibu maana pale wahudumu niliowakuta siku Ile walikua hawana uhakika na hawajui hizo process Kwa undani
 
Mkuu naamini wapeleka nje ya nchi. Kama niko sawa, basi kuna taratibu unazopaswa kufuata ili upate vibali (Mimi si mjuvi). Kuna baadhi ya nchi kama Australia ukipeleka vitu kama hivyo wanaviharibu vikitua tu nchi zao. Kuna sababu nyingi, mojawapo ni kuepuka magonjwa ya mazao na pia kusimamia ubora wa vyakula vyao. Ulipaswa ujishushe upate maelekezo hapo Posta. Usije ukawa ulinyanyua kibega, wakaamua kukuacha. Rudi tena, wao watakupa maelezo mazuri.
Umeongea kitu cha maana akifanyie kazi
 
Habari wakuu?

Kuna rafiki yangu aliniomba nimkaangie buni ya kahawa ya Kilimanjaro nimtumie,sasa nimeenda pale postal EMS wamesema hawatumi kahawa mpaka kibali na wenyewe hawajui kinapatikana wapi?

Msaada wakuu kama kuna mtu anakijua hicho kibali Cha Nini na kinapatikana wapi anisaidie maana hii kahawa nisipoituma rafiki yangu atajua nimekula pesa yake bila kuamini changamoto iliyonikumba.

Dhl bei juu nimeshindwa
View attachment 2206242View attachment 2206243
Mkuu yanj nchi hii kuna urasimu hapo mpaka uende wizara. Hata ukitaka kusafirisha ngozi ya ng'ombe lazima ukachukue kibali wizara ya maliasili.
Ukichukua gogo ukalichonga na kulipaka rangi ukataka ukaliuze nje hapo basi napo kibali
 
Mkuu si kila kitu tulaumu kwamba ni urasimu. Hivyo vibali vinahitajika hata nchi utakakotuma mzigo.
 
Kuna kipindi kipo dstv, cbs reality, new Zealand na Australia wana restrictions nyingi sana za aina za vyakula either vya kupika au raw. Ni ngumu sana kuingiza vyakula kwao, wanaogopa kuingiza maradhi kupitia vyakula, dawa kupitia vyakula..lakini pia ustawi wa mazingira yao.

So, ni muhimu sana kupata Kigali kwanza..kama sio tfda (wana jina jipya), basi tbs au wote kwa pamoja.
 
Mimi sidhani kama huo ni urasimu, hizo ni taratibu za kisheria. Urasimu ni pale mtu anataka kutuma mzigo, ila anacheleweshewa kibali kwa sababu zisizoeleweka.
 
Naangaliaga hicho kipindi, wale hawacheki na mtu wapo seriously.
 
Mkuu si kila kitu tulaumu kwamba ni urasimu. Hivyo vibali vinahitajika hata nchi utakakotuma mzigo.
Mkuu ngozi wanakupa vibali viwili kimoja kinahusiana na mambo ya afya, kingine sijui nyara. Ngozi ya ng'ombe mkuu kumbe ukitaka uza nje inakuwa kama nyara
 
Mimi sidhani kama huo ni urasimu, hizo ni taratibu za kisheria. Urasimu ni pale mtu anataka kutuma mzigo, ila anacheleweshewa kibali kwa sababu zisizoeleweka.
Kuna urasimu kama hufahamiki ukienda wizara wanakuweka unaulizwa maswali kama uko polisi. Mimi mara ya kwanza nataka kusafirisha ngozi nilihangaika kwanza posta walinimislead walinielekeza wizara ambayo sio. Kufika wizara nikapigoshwa bench aliyenisaidia ni Woiso huyu wa Woiso Original product coz ngozi nilikuwa nimeinunua kwake one call na kibali nikapewa.
 
aise unaweza kusababisha taharuki,kichwa chako cha habari ungeandika unataka kusafirisha nje ya nchi
 
Mimi sidhani kama huo ni urasimu, hizo ni taratibu za kisheria. Urasimu ni pale mtu anataka kutuma mzigo, ila anacheleweshewa kibali kwa sababu zisizoeleweka.
Ni urasimu. Wabongo tumezoea kuzungushwa zungushwa na tunadhani ukitaka kupata huduma yoyote ni lazima utaabike kwanza. Ni hivi: hao watu wa posta walitakiwa kumpa maelezo timilifu. Ilitakiwa wawe na website yenye maelezo ambayo hao wahudumu wangemwelekeza akaangalie. Shirika la posta linahudumia wateja mbali mbali na nina uhakika kuna watu wengi wanatuma vifurushi wa aina nyingi nje ya nchi ikiwepo vyakula. Kwa nini wasiwe na maelezo sahihi? fareed uziel anahangaika kwa sababu hakupewa maelezo.
 
Back
Top Bottom