Postal wamenikatalia kusafirisha nusu kilo ya kahawa mpaka kibali bila kuniambia kibali Cha nini

Postal wamenikatalia kusafirisha nusu kilo ya kahawa mpaka kibali bila kuniambia kibali Cha nini

Kuna urasimu kama hufahamiki ukienda wizara wanakuweka unaulizwa maswali kama uko polisi. Mimi mara ya kwanza nataka kusafirisha ngozi nilihangaika kwanza posta walinimislead walinielekeza wizara ambayo sio. Kufika wizara nikapigoshwa bench aliyenisaidia ni Woiso huyu wa Woiso Original product coz ngozi nilikuwa nimeinunua kwake one call na kibali nikapewa.
Watanzania tumezoea kuhangaishwa ndiyo maana watu wengi wanaona kama mwanzisha thread amekosea. Hana kosa lolote na hao posta ndiyo walitakiwa wawe na maelezo sahihi kwani ndiyo kazi yao. Ona sasa wanamwacha mteja kuhangaika wakati siku zote mteja ni mfalme.
 
Kuna siku nilitaka kutuma sample nusu kilo ya ufuta to Lebanon, DHL wakakataa mpaka niwe na kibali. Nililipa 50k kupata kibali chenywe na receipt sikupewa.
 
Njia rahisi hapo muulize kama kuna mtu anayetoka Bongo kwenda Ujerumani ili umpe ampelekee hand to hand.

Au kama hapo Moshi ofisi za TFDA zipo nenda kawacheki wakupe hicho kibali.
Option ya kwanza ni nzuri na ni cheap
 
Njia rahisi hapo muulize kama kuna mtu anayetoka Bongo kwenda Ujerumani ili umpe ampelekee hand to hand.

Au kama hapo Moshi ofisi za TFDA zipo nenda kawacheki wakupe hicho kibali.
Nipo Dar
 
Mkuu yanj nchi hii kuna urasimu hapo mpaka uende wizara. Hata ukitaka kusafirisha ngozi ya ng'ombe lazima ukachukue kibali wizara ya maliasili.
Ukichukua gogo ukalichonga na kulipaka rangi ukataka ukaliuze nje hapo basi napo kibali
Acha tu mkuu
 
Kibali hichi kinaitwa phytosanitary.
Shipper wengi anasema kina cost sh 60,000-80,000 kwa maelezo wanasema unaweza kukipata pale airport Dar es salaam.
Mwenyewe nilitaka kusafirisha samples za chai.
Baada ya kuona vile nimechoka hapa.
Cheap ni hao post tu. Kwengine ni bei ni kisanga ila lazima ulipie kibali.
 
Kwani jamaa amekupa kias gani Cha euro kumsafirishia kifurushi hicho
 
Posta wamerekebisha jengo lakini huduma sifuri. Japo kwa chakula kama wachangiaji wengine wanavyosema si kitu cha kujitumia kiholela. Kuna taratibu zake. Tatizo ni hao Posta inashangaza sana mambo yao ni ya kijima sana. Mimi nina barua 7 sijawahi kuzipata na sanduku nalilipia kila mwaka bila kulimbikiza. Mpaka leo sijui barua zangu zimepotelea wapi.
 
Kwa Mfano huyo unaemtumia Akikata roho-Magazeti ya Ujerumani yataandikaje habari bila kuitaja Tanzania,Nani anajua kama huyo Rafiki yako!
Labda ungeituma kimagendo na ukishtukiwa Kifungo Kitakuhusu...
 
Mamlaka ya kutoa kibali cha kusafirisha Kahawa yako chini ya Bodi ya Kahawa. Wasiliana nao utapewa maelekezo. Ukipata hicho kibali lazima upate wakala wa forodha ili akutengenezee documents export. Kwa maana hiyo lazima uwe na TIN hata kama sio ya biashara. Itakugharimu lakini ndio utaratibu.

BRANCH MANAGER
TANZANIA COFFEE BOARD
Godown No.1
United Youth Godowns
Off Bandari Road,Kurasini
P.O Box 3437
Dar es salaam
TEL. +255 22 – 2129847
FAX. +255 22 –2111624
EMAIL.
 
Mkuu si kila kitu tulaumu kwamba ni urasimu. Hivyo vibali vinahitajika hata nchi utakakotuma mzigo.
Sasa kama siyo urasimu inawezekanaje mamlaka ya serikali kama Posta eti hawajui taratibu za kufanya ili mtu asafirishe Parcel? Kama mtumishi wa umma hajui je raia wa kawaida itakuwaje?
 
Habari wakuu?

Kuna rafiki yangu aliniomba nimkaangie buni ya kahawa ya Kilimanjaro nimtumie ujerumani,sasa nimeenda pale postal EMS wamesema hawatumi kahawa mpaka kibali na wenyewe hawajui kinapatikana wapi?

Msaada wakuu kama kuna mtu anakijua hicho kibali Cha Nini na kinapatikana wapi anisaidie maana hii kahawa nisipoituma rafiki yangu atajua nimekula pesa yake bila kuamini changamoto iliyonikumba.

Dhl bei juu nimeshindwa
View attachment 2206242View attachment 2206243
Mkuu njia rahisi ni DHL ijapokuwa ni gharama kubwa ila uhakika mkubwa wa mzigo wako kupokelewa.
Nilituma sample za viungo ujermani mwaka jana nilituma kg 4.5 ya sample mbalimbali kwa uwiano wa 500 g
Iriki,karafuu,kahawa,pilipili kichaa,tangawizi,manjano,mdarasini na lozera
Nililipa laki 3 na 90 DHL.
Walikataa kutuma sample ya nta na asali tu maana inahitaji vibali maliasili.
Baada ya kuuliza mbona bei kubwa DHL walinieleza kuwa bei inajumuisha ukaguzi Tanzania na Germany ukipokelewa.
Ndugu, Jitahidi umeulekeze unae mtumia hiyo sample either alipie au fumba macho uende DHL uepuke usumbufu vnginevyo kutafuta vibali utatumia hela nying zaidi,pia unae mtumia akuone professional.
Business needs investment
 
Kuna siku nilitaka kutuma sample nusu kilo ya ufuta to Lebanon, DHL wakakataa mpaka niwe na kibali. Nililipa 50k kupata kibali chenywe na receipt sikupewa.
Unaona sasa! Ndiyo urasimu wenyewe huo!!
 
Kuna siku nilitaka kutuma sample nusu kilo ya ufuta to Lebanon, DHL wakakataa mpaka niwe na kibali. Nililipa 50k kupata kibali chenywe na receipt sikupewa.
Nchi hii longolongo nyingi
Jelous tu
Wanataka mabilionea wawe wale wale tu

Ova
 
Nchi hii longolongo nyingi
Jelous tu
Wanataka mabilionea wawe wale wale tu

Ova
Nilipata mchongo wa kuchukuwa damu ya ng'ombe kwenye machinjio Nairobi niipike kulekule ndio niingize Tanzania kutengeneza chakula, nilipoenda wizara ya mifugo kuulizia utaratibu wa kibali na shughuri yenyewe ikaishia hapo ikabidi niache bonge la biashara.

Maana nilivyoambiwa sample inaenda hadi kwa mkemia mkuu wa serikali kabla ya kibali nikawa sishangai kwa nini Watanzania ni maskini tena mafukara kabisa.
 
Mamlaka ya kutoa kibali cha kusafirisha Kahawa yako chini ya Bodi ya Kahawa. Wasiliana nao utapewa maelekezo. Ukipata hicho kibali lazima upate wakala wa forodha ili akutengenezee documents export. Kwa maana hiyo lazima uwe na TIN hata kama sio ya biashara. Itakugharimu lakini ndio utaratibu.

BRANCH MANAGER
TANZANIA COFFEE BOARD
Godown No.1
United Youth Godowns
Off Bandari Road,Kurasini
P.O Box 3437
Dar es salaam
TEL. +255 22 – 2129847
FAX. +255 22 –2111624
EMAIL.
😂😂😂Dah wewe ndio umenikatisha tamaa kabisa,yaani hata sitamani tena
 
Nilipata mchongo wa kuchukuwa damu ya ng'ombe kwenye machinjio Nairobi niipike kulekule ndio niingize Tanzania kutengeneza chakula, nilipoenda wizara ya mifugo kuulizia utaratibu wa kibali na shughuri yenyewe ikaishia hapo ikabidi niache bonge la biashara.

Maana nilivyoambiwa sample inaenda hadi kwa mkemia mkuu wa serikali kabla ya kibali nikawa sishangai kwa nini Watanzania ni maskini tena mafukara kabisa.
Dah pole sana .....

Lakini mchongo huo ungewapitia watu fulani,wao wangefanya

Nchi hii tunarudishana wenyewe nyuma,mabilionea watabakia hao hao
Wenye asili ya kiarabu na kihindi tu

Ova
 
Option ya kwanza ni cheap lakini risky.

Hebu fikiria umepewa mzigo wa kahawa iliyokaangwa umpelekee mtu ujerumani.

Unafika ujerumani watu wa narcotics wanaupima wanakuambia hiyo kahawa iko coated na cocaine.

Wema wako ndiyo kosa lako
Hahahahaaaa naua
 
Sasa kama siyo urasimu inawezekanaje mamlaka ya serikali kama Posta eti hawajui taratibu za kufanya ili mtu asafirishe Parcel? Kama mtumishi wa umma hajui je raia wa kawaida itakuwaje?
Yaani nilichoka nilivojibiwa,yaani Tena hapo baada ya kuuliza zaidi ya watu watatu kwenye Ile sehemu maana anayeshughulika mizigo akaniambie emu nenda kaulize dirisha like pale,na huyo akanielekeza kwingine ndio nikapata jibu hilo
 
Back
Top Bottom