Mwanzoni yalikuwa yakizungumziwa mambo machache tu hasa hili la kutosomesha mpenzi/mchumba. Kulikuwa hakuna post wala nyuzi nyingi za kuwaandama wanawake. Ila kwa kinachoendelea ni dhahiri nguvu ya mwanamke inaongezeka huku ya mwanaume ikipungua. Vijana hawajiamini kabisa wanapokuwa kwenye mahusiano na wanawake. Siku hizi hadi vijembe wanaume wanapost baada ya kuachana.
Vitabu vitakatifu vimeandika wazi kwamba tuishi na wanawake kwa akili na hakuna sehemu vitabu vimetoa mwongozo kwamba tuishi nao vipi. Ndugu Smart911 anasemaga HAYANA MWONGOZO. Mitandao imekua sehemu ya vijana wa kiume kupoteza muda kuongelea jinsi ya kuwa na mwanamke. Kimsingi ni kama usengenyaji fulani hivi. Utasikia "usioe single maza", "usimpe attention", "mwanamke usimwonyeshe upendo", "mwanamke usimpe hela", "mwanamke asijue kuhusu shughuli zako", na kauli nyingi sana za kutojiamini.
Ninashauri vijana tutumie akili zetu tulizojaliwa kuongoza wanawake zetu na sio kuja mtandaoni kuwasengenya. Mwanaume kamili hawezi poteza muda kuongelea mwanamke wake. Kama hakufai na harekebishiki piga chini. Inatakiwa tusikie makelele ya mwanamke baada ya kuachana na sio mwanaume unaingia mtandaoni kupost vijembe.