Posts na nyuzi nyingi mtandaoni za wanaume kuongelea jinsi ya kuishi na wanawake inadhihirisha jinsi gani kutojiamini kwa wanaume kunavyoongezeka

Posts na nyuzi nyingi mtandaoni za wanaume kuongelea jinsi ya kuishi na wanawake inadhihirisha jinsi gani kutojiamini kwa wanaume kunavyoongezeka

Matongee

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2023
Posts
1,056
Reaction score
2,729
Mwanzoni yalikuwa yakizungumziwa mambo machache tu hasa hili la kutosomesha mpenzi/mchumba. Kulikuwa hakuna post wala nyuzi nyingi za kuwaandama wanawake. Ila kwa kinachoendelea ni dhahiri nguvu ya mwanamke inaongezeka huku ya mwanaume ikipungua. Vijana hawajiamini kabisa wanapokuwa kwenye mahusiano na wanawake. Siku hizi hadi vijembe wanaume wanapost baada ya kuachana.

Vitabu vitakatifu vimeandika wazi kwamba tuishi na wanawake kwa akili na hakuna sehemu vitabu vimetoa mwongozo kwamba tuishi nao vipi. Ndugu Smart911 anasemaga HAYANA MWONGOZO. Mitandao imekua sehemu ya vijana wa kiume kupoteza muda kuongelea jinsi ya kuwa na mwanamke. Kimsingi ni kama usengenyaji fulani hivi. Utasikia "usioe single maza", "usimpe attention", "mwanamke usimwonyeshe upendo", "mwanamke usimpe hela", "mwanamke asijue kuhusu shughuli zako", na kauli nyingi sana za kutojiamini.

Ninashauri vijana tutumie akili zetu tulizojaliwa kuongoza wanawake zetu na sio kuja mtandaoni kuwasengenya. Mwanaume kamili hawezi poteza muda kuongelea mwanamke wake. Kama hakufai na harekebishiki piga chini. Inatakiwa tusikie makelele ya mwanamke baada ya kuachana na sio mwanaume unaingia mtandaoni kupost vijembe.
Screenshot_20240703-123602_X.jpg
 
Unaogopa Nini kama kipochi chake kaamua kukianika Kwa mtu mwingine

Mwache maana ni maamuzi yake wewe tafuta chimbo jingine hamisha makazi Kila mtu afurahie kivyake uumbaji wa
 
Jando na unyago vimehamia mitandaoni, vijana wa kike na kiume hawana mafunzo muhimu ya mahusiano, huenda hata wewe huelewi lolote ndio maana umeandika hii thread.
Umetumia vizuri yako ya kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 18.
 
Sio hofu , hii ni platform ya kuandika na kusoma kwa hiyo kuna uelimishaji kuhusu mahusiano ! Hii ni elimu ya Jinsia na ni muhimu ( japo sio zote ) na ukiona jinsia moja inaandika sana ujue inapitia changamoto au jinsia isiyoandika inaweza kuwa wanakufa na Tai shingoni.

Kuna watoto wanabalehe humu wanajifunza
Kuna watu wazima hata hawana suluhisho huko vyumbani.
Kuna watu wanajiua kwa ajili ya wanawake au wanaume ! Inaweza isitusaidie watu 599k tulio JF ila ikamuokoa mwana mmoja.
 
Sisi ni kama maji. Utake utatuongelea, usitake bado ni vile vile.
 
Muongozo wake ndo hiyo akili basiiii
 
Back
Top Bottom