Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabisa hiyo naongelea pale uwanja wa shule Tabora town school 1981 hiviMkuu wewe lazima utakuwa ni mhenga...
Uko sahihi ni miaka hiyo nakumbuka ilidondoka ndege ya kivita pale uwanja wa taifa wa zamani Dar, ilikuwa parade sikukuu ya mashujaa,alikuwepo pale...Kabisa hiyo naongelea pale uwanja wa shule Tabora town school 1981 hivi
Huyu power Mabula nilishuhudia show zake early 80s,gari landrover alilolizuia kwa kamba liliendeshwa na baba yangu,nikiwa nashuhudia.
Kuna Siku nilimuona urambo, true ameokoka
Uncle Juju mbona mimi hujanihadithia kumhusu.I knew him personally and I always have a story to tell about him.
You can hit me up whenever is convenient for you and I'll be glad to share it with you.
He is the source of my lifelong passion.
Uncle Juju mbona mimi hujanihadithia kumhusu.
Mshkaji wako yupo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] leo nimempa wali maharage kakataa anauliza "mama mbona hakuna mchuzi" nilicheka sana.Niambie kwanza....mshikaji wangu yupo au hayupo? [emoji3][emoji6]
Mutu na mutu abongisaa kilikuwa kibwagizo chakeBila kumsahau Profesa EYESO! (A.S.O) na mazingaombwe yake, miaka ya '80s alizungukia karibu shule zote za wakati huo
Nakumbuka enzi hizo kulikuwa na vipindi vya michezo ya kwenye radio, kama vile, Mahoka (Na kicheko chake, mama mbavu zangu x2 eh eh eh eh eheeeeeeeeeeeeeeeeeH AAAH) na Pwagu na Pwaguzi...!
Kuna mchezo mmoja wa Pwagu na Pwaguzi, walianzisha mradi wa zahanati ya kungoa meno huku wakiwa hawana mafunzo yoyote ya udaktari wa meno, nje ya ofisi yao waliweka bango kubwa likionesha kuwa wao ni wataalamu wa kungoa meno.
Mteja akifika anapokewa mapokezi na mwenzake Pwaguzi, baada ya kulipia pesa ya matibabu anakwenda chumbani aliko Pwagu na kuanza kungolewa meno kwa kutumia koleo za mafundi baiskeli, Ah ah ah ah.
Issue inakuja kwenye kuulizia fedha ambazo mteja alitoa, Pwaguzi siku zote alikuwa anamdhurumu mwenzake, uwa anadai kuwa zilishapotea katika purukushani za kukimbia...!
Nakumbuka kuna mradi mwingine, walikuwa wanakusanya damu za mbuzi, na kuzipeleka Hospitali, eti wanadai wanatoa msaada kwenye benki ya damu, ah ah ah ah. Hawa jamaa walikuwa mwisho.
Nawakumbuka magwiji wa michezo ya kuigiza yaani maselebu wa ukweli, kama Marehemu Mzee Hamis Tajiri (Janja au Meneja Mikupuo), Marehemu Bi Tunu Mrisho (Mama Haambiliki), Mwanaheri Ngandu, Justin Kilumbi, Ali Manjunju (Ngosha), Marehemu Mzee Batholomeo Milulu (Masawe) na Marehemu Mzee Ibrahim Raha (Mzee Jongo) Mzee Fundi Said (Kipara) na wenginewe nimewasahau.
Power mabula enzi zake. Ila kwa story za waliomwona wanasema alikuwa hadi lori linamkanyaga.Aisee huyu jamaa alivuma sana miaka ya 80 but sadly I never got to see him. Kulikuwepo na story kibao kuhusu uwezo wake wa nguvu za misuri, mambo kibao yaliongelewa, mfano:
-- Alikuwa anaweza kunywa kreti nzima ya soda kwa mkupuo...
King'ast mpaja wako kwenye avatar unaonyesha wewe si mbibi ni mdadanilimuona mara kadhaa kwenye maonesho wakati nikiwa primary skul. ni kweli alikuwa anafanya hayo yote yaliyotajwa,ilikuwa inaogopesha aisee.mara ya mwisho niliskia habari zake kuwa aliokoka na akatolewa mapepo mengi.
Ilisemekana alikuwa anatumia nguvu za giza na hizo kreti za soda walikuwa wanakunywa majini (sijamuona live baada ya kuokoka).ila naskia aliacha mazingaombwe.umenikumbusha mbali sana
Enzi hizo za mazingaombwe kulikua na
Power Mabula-akivuta gari kwa meno
Profesa Eyesu yeye hana ubabe
Weka makaratasi kwenye chungu inageuka dolale🙃😆😆😁
Hawa watu wako wapi?
Wakongwe jazieni hapo