Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Hapana X-P hakua mtu wa msoma alikua msukuma, naskia alikuja kuokoka yeye na mwingine alikua anaitwa power Mwasekaga kitu kama hicho.
Hawa jamaa walitakiwa wawekwe kwenye kipindi cha Believe it or No cha AXN.
inshu sio kuwa msukuma kwani ata Mkoa wa Mara maeneo ya Bunda wapo wasukuma wazawa wengi tu.Ni vyema ungesema ni msukuma wa wapi?
nbpower MABULA ni msukuma wa shinyanga.
 
Kama haya matukio ni ya miaka ya 90 basi kupata picha ni ngumu aisee.. kipindi hicho kupiga picha ni anasa teh
ni kweli ,lakini baadhi ya matukio walichukuliwa cameraman toka studio kupiga picha kwenye matukio aya.
 
Dah nimetafutaga sana historia ya huyu power mabula..tulikuwaga tukiimba enzi hizo "Kababa ninyanyue nyanyu...nyanyuaaaaa,,kababa nibebeeebebe .....beeba""
kababa yeeeeh yeeeeeee,kababa yiii yiiiii

Ilikua raha sana,Mara ya mwisho nlimuonaga Makumira Sec alifunga unywele wake kwenye pikipiki aina ya honda,akaweka ngita hakika pikipiki haikusogea...na mambo mengine mengi...daah
 
Dah nimetafutaga sana historia ya huyu power mabula..tulikuwaga tukiimba enzi hizo "Kababa ninyanyue nyanyu...nyanyuaaaaa,,kababa nibebeeebebe .....beeba""
kababa yeeeeh yeeeeeee,kababa yiii yiiiii

Ilikua raha sana,Mara ya mwisho nlimuonaga Makumira Sec alifunga unywele wake kwenye pikipiki aina ya honda,akaweka ngita hakika pikipiki haikusogea...na mambo mengine mengi...daah
Unachanganya mambo aise...Mabula ni mwingine na huyo anayeimba ni mwingine, huyo aliitwa KABABA YEE...mwisho wa siku asilimia themanini ya show mnaimbishwa na vitendo ni asilimia ishirini tu....jamaa alikuwa clever sana...alikuwa mwembaba, nadhani kuliko Mapower wote wa wakati wake....na kama sikosei alikuwa mwenyeji wa Tanga.

Mwingine alikuwa anaitwa Power MWANAKULIA JITULISHIBALO.
 
Kizazi cha whatsapp na instagram kimepitwa sana na mambo mazuri, huyu power mabula alikuwa rafiki yake sana marehem mzee wangu kwa sababu alikuwa mara nyingi akipiga show pale bush kwetu lazima aje kuchukua Stout yetu, najua vijana wa leo hata Toyota stout hamzijui,
Kuliwepo na jamaa anajiita kaburu bota dah huyu nilikuwa namuogopa kupita maelezo, siku akipiga show usiku silali
 
Na shule zilikuwa zinawaruhusu kuja mashureni.. Basi akija kengere inagongwa mnaenda mstalini anawaonyesha mambo mawili anawambia tuonane baadae
Hapo alikuwa anakupa washawasha,kam home jirani.mwenyewe utakwenda kulia upate shilingi kumi
 
Thread kama hii ni nzuri sana, unakumbuka matukio na enzi za wakati huo, namkumbuka pia Power Jabir Computer a.k.a Kababayee ulikuwa ukiambiwa atakuja shuleni chunga sana kalamu na vitabu, mtu akikuibia anaviuza japo apate shilingi 5 ya kuingilia kwenye maonesho na nyimbo zake zile ''misumri nilalielalie'' watu ''lalia''

Acha kabisa kwa sisi kipindi hicho mwaka 93 na vipindi vya mchana vinavunjwa kabisa watu tukirudia ni full mazingaombwe namkumbuka sana huyu jamaa na kibao chake cha misumari.
 
power Mabula nilikutana nae kijiji kimoja kinaitwa Songe wilayani Kilindi 2006,hivi sasa ni mchungaji wa kanisa la Moses Kulola
 
Aisee huyu jamaa alivuma sana miaka ya 80 but sadly I never got to see him. Kulikuwepo na story kibao kuhusu uwezo wake wa nguvu za misuri, mambo kibao yaliongelewa, mfano:

-- Alikuwa anaweza kunywa kreti nzima ya soda kwa mkupuo
-- Alikuwa anaweza kutegesha kifua na tairi la nyuma la trekta kupita bila kuumia
-- Alikuwa anaweza kuvuta lorry lenye shehena kubwa kwa kutumia nywele
-- n.k.

Were these just a bunch of childish myths kutufanya tukimbie mchakamchaka na kuwahi namba shuleni or was there a grain of truth in them? Tafadhali sana naomba wale waliobahatika kuyaona maonesho ya jamaa watupatie ushuhuda hapa.

Pia naomba kuuliza, je yuko wapi siku hizi, kuna mwenye picha? Bado yupo, au..??
Akhsanteni!!
hakukua na ulazima wa kutia hicho kizungu chako cha kukariri kwenye movie
 
Kunywa soda crate aliweza ila Mara ya mwisho alikuwa mgonjwa Wa kisukari na ile michezo yake haikumwingizia sana pesa kama alivyodhani akawa fulltime michezo hiyo .Mara ya mwisho alienda huko mpanda vijijini akawa mkulima aliyechoka. Nguvu bila busara ni hasara. Aliuchosha mwili kwa malipo kiduchu. Pole take. Hata wengine walikuwemo mfano( Tai kichaa, power bernardo nk) .bora asingeacha jeshi maana jeshini alikula Burr na michezo ikiwa kama burdani. Pia angestaafu hata Leo angekuwa na pensheni. Nguvu zilimdanganya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Basata na wizara ya mwakyembe wana history ya diamond na kina amber ruty tu.ukiwa na baraza na wizara ya utamaduni alafu hata siku moja hawakai kuwaza kuandaa hata tamasha LA kuenzi celebrated wetu na kumbukumbuk zao na kutoa tuzo kwa mchango wao jua fikra zao zimetekwa na usasa mwingi.
 
Back
Top Bottom