Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

power kapalata anasema baada ya mganga wao kufariki 1993 ndio ukawa mwisho wa ile michezo ya kakanyagwa na trekta kwenye mkono na hauvunjiki ikabaki michezo ya kutunisha misuli tu, na mazingaombwe ya hapa na pale. For ref. power kapalata anafanya kazi ni dereva wa bus za sumry high class sumbawanga-mbeya-sumbawanga.
 
binafsi nimemsikia tuu..simjui hata anafananaje?

Miaka kama 20 hivi iliyopita kulikuwa ni 'fashion' Fulaninchini mwetu ambapo walikuwepo watu watunisha misuli. Mabonge ya watu akina Power mabula, Power Sangandele na kadhalika. Walikuwa na vifua vipana na nguvu nyingi au kubwa. Walikuwa na uwezo wa kuvuta magari kwa meno au mtu kupigilia misumari kwenye mbao zilizotandazwa vifuani mwao. Kila weekend kulikuwa na matangazo magazetini (UHURU, DAILY NEWS na MFANYAKAZI) kwamba weekend hii Power Mabula (na wengineo wengi) atakuwa mahali fulani akionyesha mavitu yake ya nguvu. Basi watu walikuwa wanafurika kweli kweli. Yaani hao ma-'power' walikuwa ni shida. Mara wabebe mifuko arobaini ya cement vifuani mwao sijui mara wafanye hiki na kile mradi tu ilikuwa ni burudani ya aina yake kama ilivyokuwa kwa akina CHENGA kucheza na mijoka.
 
natamani siku nisikie stor za pawa mabula
kwa uchache ni msukuma mmoja wa miraba minne aliyekuwa ana nguvu sanaa.akivaa guo lilishonwa kwa ngozi.ana unywele mmoja mreefu mpaka matakoni ambao wakati mwingine kwayo aliutumia kuvuta gari au pikipiki.
kuna wakati waliweka jiwe kuubwa sana kifuani pake na kulipasua lote na nyundo juu ya kifua hicho aliweza kunywa chumba sita au saba za orange squash kwa wakati ule.kuna wakati akivuta pikipiki kwa meno.kwa haakika lilikuwa ni jitu lenye nguvu,niliwahi mshuhudia akibeba matofali manne kwa meno.
yeye mwenyewe alikuwa akisema alizaliwa kipindi cha mvua kubwa mashambani bibi yake akamlea kwa kumfunika kwa ngozi ya chatu.nadhani kidogo nitakuwa nimekugusa kidogo.
 
muraa
alikua anapangua risasi kwa mkono ina maana alikua mchawi?
vile vitu vilikuwa na mahusiano na uchawi mababu walikuwa na dawa zao za ajabu sana kwa wasambaa kuna kitu inaitwa[ muku]ukichanjiwa ukapigana ni hatari sana,au kubeba mzigo mzito
 
Umenikumbusha enzi za mapawa na maprofesa (wanamazingaombwe). Power Mabula was one of my favourite, kulikuwa na power mwingine anaitwa Power Ngeta, huyu akija tulikuwa tunaimba "Power! Ngeta! Super! Kibongeeee!" Sijui yuko wapi naye huyu.

Kuna dogo tulikuwa tuko naye darasani alikuwa ni fundi wa kutengeneza mihuri (inayogongwa mkononi kama unatoka nje mara moja na utarudi), basi wale maprofesa wakija dogo naye anatengeza na kutugongea mikononi watu wanaotaka kuingia bila kulipia. Baadae ukitoka unampa shilingi 5 au unamnunulia vipande vya mihogo. Tulikuwa tunainjoi sana maisha yale.
wimbo ulikuwa unaimbwa hivi,
Power.....ngeta.......super......kibonge( rudia×4)
 
tulikuwa tuna wa ranks hivi.
1.power MABULA
2.power gronda
3.power ngeta.
4.power silasi

hiyo ndiyo top 4 ,walikuwa ni hatari tupu watu hawa.
Najua wengi hamkushuhudia pambano Kali kabisa LA kihistoria kati ya power MABULA vs power groda,,,ilikuwa hatari tupu.
 
Duh mmenikumbusha kitambo sana wadau.Kuna mmoja pia alikuwa anaitwa power ngeta,cjui naye yupo wapi nowadays?Mwingine wa mazingaombwe aliitwa prof.machafuko.Huyu jamaa alikuwa na usanii balaa.Miaka ya 1990's nikiwa primary school alikuja kufanya show iliyofanyikia darasani.Ile naingia tu ndani nikaona yai la kuku lipo kwenye mbao za darini.Prof. alipoanza shows zake,moja ilihusu kuonekana kwa yai.Kweli,baada ya muda kufanya tukio fulani,ghafla akasema litatokea yai humu ndani,duh.Akatuonesha lile yai nililoliona wakati naingia kabla show haijaanza.Nilipigwa butwaa but ilibidi nitoke nje nikacheke coz nilikuwa naogopa kufanyiwa kitu mbaya nikichekea ndani.
 
Na shule zilikuwa zinawaruhusu kuja mashureni.. Basi akija kengere inagongwa mnaenda mstalini anawaonyesha mambo mawili anawambia tuonane baadae
 
tulikuwa tuna wa ranks hivi.
1.power MABULA
2.power gronda
3.power ngeta.
4.power silasi

hiyo ndiyo top 4 ,walikuwa ni hatari tupu watu hawa.
Najua wengi hamkushuhudia pambano Kali kabisa LA kihistoria kati ya power MABULA vs power groda,,,ilikuwa hatari tupu.
mkuu power ten by ten hujamuweka hapo ila kati ya wote maarufu ni MABULA hivi bado yupo hai?
 
Huu Uzi umenikumbusha mbali sana. Power mabula kipindi Fulani alikuja shuleni kwetu. Kiingilio kwenda kumuona ilikuwa shillingi tano. Unfortunately sikuwa na hela. Kwa hiyo kengere ilivyopigwa saa Tisa tuko parade wale wenye hela wakaenda ukumbini kumuona Power Mabula. Wale tusiokuwa Na kitu tukaambiwa tuelekee nyumbani. That's how I missed to see this guy alive vuma kuliko maelezo.

In all tumetoka mbali. When I look back kwamba I could not afford five shillings to see something I really wanted, nasema Mungu ni mwema. May this generation be inspired by our hardships we went through to make this world a better place and improve the wellbeing of humanity in general.
Amen Mkuu, Mungu ni Mkuu Sana.
 
Ni kweli huyo jamaa, alikuwa na nguvu kweli kweli, nasikia alikuwa ni mtu wa Musoma, Mara uko...! Hayo ni mambo ambayo kweli alikuwa anafanya, na alikuwa ana uwezo wa kunywa chupa za orange squash mpaka mbili bila ya kuzimua.

Si hivyo tu, alikuwa anauwezo wa kuzuia piki piki kwa kutumia nywele na wakati mwingine meno. Na hata kuzuiya gari kwa kutumia nywele zake. Na alikuwa akivunjiwa jiwe kubwa kifuani kwake.

Pia kulikuwa na mwingine anaitwa power Bernard, na wakaja mwishoni mwishoni kina power Bukuku, ila wengine nimewasahau.

Gonga hapa mkuu, kuna uzi kama huyo.

Power-mabula-moris-nyunyusa-na-mwinamila-tz-imewaenzi-vipi.html
MABULA hakuwa wa Mara alikuwa wa shinyanga,ila amefanya maonyesho mengi sana Mkoa wa Mara.
Power gronda ndiye mtu wa Mara.
 
Power Ngeeeeta Supeeeer kibongeee......nimekumbuka mbali sana aiseeee
Alikuwa hatari ila kiboko alikuwa power MABULA.
Kuna siku iliandaliwa mpambano kati ya power MABULA vs power gronda ilikuwa ni hatari tupu.
 
Back
Top Bottom