Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Power Mabula: Mtu aliyetikisa enzi zake!

Pawa Mabula asili yake kanda ya ziwa. Aliweza kuzuia trekta lisitembee kwa nyele zake na aliweza kuvuta watu wazima walioshiba 20 kwa meno yake. Tairi ya trekta iliweza kupita juu ya tumbo lake akiwa amelala bila kumdhulu. Kilo 100 yeye alizinyenyua kwa meno yake. Miaka ya 1990 kuelekea 2000 alipigana pia mieleka, mpinzani wake mkubwa akiwa Pawa Ngoro.

Nilisikia eti Pawa Mabula ameokoka na ni mchungaji hivi ni kweli?
 
hahahahaha huyu jamaa ni muongo.ati alikuwa akipangua risasi kwa mkono.... hahaha

Lazima ukatae, nasikulazimishi uamini, aliyenisimulia ni baba yangu na walikuwa kikosi kimoja mstari wa mbele na mzee ndo alikuwa kiongozi wake.
 
Lazima ukatae, nasikulazimishi uamini, aliyenisimulia ni baba yangu na walikuwa kikosi kimoja mstari wa mbele na mzee ndo alikuwa kiongozi wake.

aim sorry to say this ... "baba yako alikudanganya"
 
hivi alienda wapi huyu baba?
nakumbukua enzi zile pale Jamhuri stadium Dom alivyokuwa anakunywa orange squash kama 10 hivi bila kuchanganya na maji akitoka hapo ananyanyua kilos kibao
 
binafsi nimemsikia tuu..simjui hata anafananaje?

Alikuwa ni wa kutoka mkoa wa Tabora enzi zake alikuwa ana nguvu sana lakini tatizo lake alikuwa anakunywa sana orange squash ni kinywaji ambacho ni lazima uchanganye na maji lakini yeye alikuwa anapiga dry bila Ku dilute mpaka chupa sita. Hiyo ilimpelekea kupata kisukari na kudhoofika sana, amefariki sasa mungu amuweke pema
 
Pawa Mabula asili yake kanda ya ziwa. Aliweza kuzuia trekta lisitembee kwa nyele zake na aliweza kuvuta watu wazima walioshiba 20 kwa meno yake. Tairi ya trekta iliweza kupita juu ya tumbo lake akiwa amelala bila kumdhulu. Kilo 100 yeye alizinyenyua kwa meno yake. Miaka ya 1990 kuelekea 2000 alipigana pia mieleka, mpinzani wake mkubwa akiwa Pawa Ngoro.

Nakumbuka enzi hizo alipigana na jamaa mmoja kwa jina Gandi alikuwa mwembamba sana lakini alikuwa mgomvi sana na humpati kwa ngumi na akikupiga kichwa huamki. Zilipigwa na Mabula kila akimpiga anakwepa Gandi akaigama kwenye behewa Mabula alitupa ngumi gandi akakwepa behewa lilibonyea and that's fact
 
Amefariki kama sikosei, alikuwa afisa waJWTZ, wakati wa vita ya Uganda alikuwa kikosi kimoja na baba yangu anasema alikuwa na uwezo wa kupangua risasi za adui kwa mikono, baada ya vita alikuja nyumbani kwetu mara mbili lakini nilikuwa nakimbia kwa kumuogopa.

huyu ni nani???? Kama pawa mabula hapana... Ninamfaham labda vizuri kidogo, kuna mdau kaongea kuhusu uwezo wake.. Kwa kuongezea pawa mabula nimemuona zaidi ya mara 20 nadhani, ni mtu wa Shinyanga ambako nimezaliwa na kukulia kidogo.. Alikuwa na uwezo wa kuvuta semi kwa meno.. Na nguvu za ajabu.. Yupo hai na naskia anaishi Arusha ila ameacha hayo mambo na ameokoka kwa sasa..
 
Alikuwa ni wa kutoka mkoa wa Tabora enzi zake alikuwa ana nguvu sana lakini tatizo lake alikuwa anakunywa sana orange squash ni kinywaji ambacho ni lazima uchanganye na maji lakini yeye alikuwa anapiga dry bila Ku dilute mpaka chupa sita. Hiyo ilimpelekea kupata kisukari na kudhoofika sana, amefariki sasa mungu amuweke pema

apumzike kwa amani
 
Huu Uzi umenikumbusha mbali sana. Power mabula kipindi Fulani alikuja shuleni kwetu. Kiingilio kwenda kumuona ilikuwa shillingi tano. Unfortunately sikuwa na hela. Kwa hiyo kengere ilivyopigwa saa Tisa tuko parade wale wenye hela wakaenda ukumbini kumuona Power Mabula. Wale tusiokuwa Na kitu tukaambiwa tuelekee nyumbani. That's how I missed to see this guy alive vuma kuliko maelezo.

In all tumetoka mbali. When I look back kwamba I could not afford five shillings to see something I really wanted, nasema Mungu ni mwema. May this generation be inspired by our hardships we went through to make this world a better place and improve the wellbeing of humanity in general.
 
natamani siku nisikie stor za pawa mabula
1, kwa sasa power mabula ni mchungaji katika kanisa la (TAG) Usharika wa morogoro, pia power mabula au kwa jina lake halisi james mabula, alikuwa ni mmojawapo kati ya watia nia 11 kuwania kuteuliwa na chadema ili kupeperusha bendera ya cdm katika jimbo la morogoro mjini lakini akaanguka ktk kura za ndani za mchujo.

2, kitambo kidogo nikisoma blog ya fullshangwe, john bukuku akiwa safarini tokea sumbawanga kuja dar, alibahatika kuka siti ya mbele na dereva huyu power kapalata wakipiga stori ndipo alipomuuliza kwa nini unaitwa power?, akamjibu; "miaka ya nyuma, mimi, power mabula,na mapower wote tz nzima, tulikuwa na mganga wetu mmoja pale muze,sumbawanga. akiitwa pascal kamoja, huyu mzee alikuwa na nguvu za miujiza ya ajabu sijapata kuona! kabla ya kuingia kwenye michezo yt, alitupa dawa ya kunywa na ya kupaka. ukiingia kwemye mchezo unakuwa na nguvu za simba, alipofariki 1993 ndio ikawa mwisho!.
 
Namkumbuka sana huyu jamaa kwani alivuma sana miaka ile.
aliokoka miaka ya 95/96 na alikuwa anapita kuhubiri na kuelezea namna alivyokuwa anatumia nguvu za giza kufanikisha mambo yake.
hadi sasa bado yupo kwenye wokovu.
Jina la Bwana lihimidiwe.
Nilimjua huyu mabula wakati nina miaka 5 au 6 au saba. Miaka ya themanini
 
Very interesting, nimewahi kumshuhudia miaka ya 1982/3 nikiwa primary Singida mjini huyu bwana alikuwa mwanajeshi, alikuwa na uwezo wa kuvuta magari mawili kwa kuyazuia yasiondoke kwa kutumia mikono yake, magari yakiwa yanakwenda pande tofauti yeye akiwa katikati na kweli magari yalikuwa hayaondoki. Yalikukuwa yakiishia kuunguruma tu bila kufanikiwa kuondoka!!
Heshima mkuu. Enzi hizo ulikua primary?
 
Back
Top Bottom