Power of Attorney ina umuhimu gani?

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Habari wakuu,

Power of Attorney ni kitu ambacho nimekuwa nakutana nacho mara kwa mara. Ni kitu ambacho kwa maoni yangu, si cha kawaida sana Tanzania kama ilivyo nchi za wenzetu. Inawezekana ni desturi yetu au inawezekana pia ni kwasababu wengi wetu hatuna uelewa wa kutosha kuhusu jambo hilo.

Kwa mujibu wa mtandao: A Power of Attorney is a legal agreement between two people in which one person is able to act on behalf of the other person.

Kwa nilivyoelewa (nakaribisha marekebisho) ni kumruhusu mtu mwingine kufanya maamuzi kwa niaba yako ikiwa huwezi kufanya hivyo mwenyewe.

Nina maswali kadhaa katika hili, naomba wanasheria na wanaoifahamu sheria mnisaidie:

1. Ikitokea nahitaji Power of Attorney, naanzia wapi? Yaani process nzima hadi naipata imekaaje?

2. Kama mtu ana Power of Attorney, anaweza kufanya maamuzi ya mwisho ikiwa mhusika au walio karibu naye hawakubaliani nae?

3. Ni vigezo gani huzingatiwa ili kumpa mtu Power of Attorney? Ni lazima mtu huyo awe mtaalamu wa sheria?

4. Hii Power of Attorney ina umuhimu gani especially kwa watu wa kawaida?

Ni hayo tu, asanteni kwa ushirikiano.
 
Power of attorney ni kama tu msimamizi wa mirathi majukumu yake, ukijua jukumu la msimamizi wa mirathi utajua nini maana ya power of attorney
 
Doh!!! Acha tu mkuu tuendelee kuwalipia mihuri yao, ile ni sawa na stamp tu ile ya posta,ipo kwa sababu ilikuwepo.
 
Influenza

Kimsingi na kitaaluma ktk sheria power of attorney ama 'nguvu ya wakili' si kitu kigeni na kinatumika karibu kila siku kwa shughuli za uwakilishi wa kisheria.

Mfano hai. Kaka yake Tundu Lisu Alute Mughwai Lisu alipewa 'power of Attorney' kushitaki kwa niaba ya Lisu ambaye hayupo nchini na akafanya hivyo ktk kesi iliyofunguliwa Dodoma dhidi ya spika na mwanasheria mkuu ikuhusu kupigwa kuvuliwa ubunge wa Lisu.

Ieleweke kwamba, power of attorney inaweza ikampa ama ikamkasimisha mamlaka ya jumla ya mtu kuwakilisha mtu mwingine kwenye jambo lolote la kisheria yaani tunaita, 'general power of attorney' ama mtu akapewa mamlaka mahususi tu kuwakilisha mtu mwingine kisheria hii tunaita, 'special power of attorney'.


1. Ikitokea wahitaji nenda kwa mwanasheria ili ampe ushauri stahiki.

2. Power of Attorney inampa mtu ama kumkamisimisha mamlaka kamili kama vile mhusika mkuu wa jambo fulani la kisheria, hivyo maamuzi ya mwisho juu ya jambo alilokasimishwa mamlaka ni yake.

3. Sio lazma mtu anayepewa nguvu ya wakili awe mtaalamu wa sheria, anaweza kuwa mtu yoyete tu ambaye tunasema kiujumla he/she is not disqualified from any other law. Sana sana awe mtu mzima, mwenye wakili timamu na ambaye mkasimisha mamlaka amemuamini kwa niaba yake.

4. Umuhimu wa power of attorney ni mkubwa kijumla humpa 'locus standing/locus' yaani maslahi ya kisheria kusimama badala ya mtu mwingine ambaye mara nyingi anakuwa nje ya nje nchi.
 
Power of attorneys(nguvu ya uwakilishi) ni nyaraka inayokasimisha Mamlaka ya kisheria kwa mtu aliyechaguliwa na mkasimishaji ili watende matendo yote yenye kuhusiana na ukasimishaji huo kwa niaba ya ukasimishaji.
Mambo ya kuzingatia;

1. Nyaraka hii ni ya kisheria hivyo ni lazima izingatie matakwa ya kisheria ikiwa ni pamoja na umri wa wahusika, uelewa wa Jambo husika, utayari,

2. Nyaraka hii ni lazima iwe na kiapo cha cha wahusika kilichofanyika mbele ya kamishina wa viapo yaani Hakimu au wakili.

3. Nyaraka hii ni lazima usajiliwe kwa msajili wa nyaraka ili ipate uhalali kisheria

4. Pia ni muhimu kuweka stamp duty

5. ifahamike kuwa kila atakalofanya aliyekasimishwa Mamlaka kupitia nguvu ya uwakili litahesabika kuwa na matendo halali ya mkasimishaji ikiwa tu haliko nje ya nguvu ya uwakili
 
Power of attorney inaweza tumika katika issue ya mkataba

Na je haito athiri privity to contract?
 
Power of attorney inaweza tumika katika issue ya mkataba

Na je haito athiri privity to contract?
kimsingi baada ya kupata PO.O.A uuk
Power of attorney inaweza tumika katika issue ya mkataba

Na je haito athiri privity to contract?
Kimsingi baada ya kupata Power of attorney ni ikiwa kuingia ktk mikataba ni mojawapo ya Mamlaka aliyopewa mhusika basi kila atakachofanya maadamu kiwe within the given Power bs ni halali kisheria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…