PPPC kuvuta mitaji ya $9bn

PPPC kuvuta mitaji ya $9bn

Tanzania tunahitaji watu makini sio Rasilimali kwani Rasilimali tunazo, karibu zote,
Mkapa alikuja na sera hii ya ubinafshaji tuliona matokeo yake
Nataka kujua hii PPP inatofauti gani na ile ya Mkapa?
Abood pale Morogoro anamajengo yetu yeye anafugia Mbuzi wakati kile kilikuwa ni kiwanda
Ndiyo maana wanakimbilia kuwa wabunge ili wasikamatwe, nchi inanuka rushwa tupu
 
Sina mgogoro na PPP,ILA ninataka kujua ni kwa muda gani hawa watu wanapewa kuendesha hii miradi?

Hii mikataba isizidi miaka 10
HIlo la miaka 10 halitawezekana. Fikiria kampuni ijenge barabara ya kulipia kutoka Chalinze mpaka Kibaha, hao watumiaji watakuwa wanalipia kiasi gani kila wakipita, kiasi kwamba hela ya hiyo kamapuni itakayojenga irudi na hiyo kampuni ipate faida ndani ya miaka 10?

Kwa vyovyote hii miradi itakuwa ya ubia kwa miaka siyo chini ya 90, kama lilivyo jengo la Mlimani City.
 
Hiyo ppp imebuniwa na wazungu na bado imewashinda! Ni unyonyaji wa kistaarabu furani!
Nimekaa paleee!
 
Mkuu Mia770

Mkapa alifanya Ubinafsishaji lakini Samia anafanya Ubia,
Tofauti ya Ubia na ubinafsi ni kwamba,

Ubinafsishaji umiliki unabadilika
Ubia umiliki haubadiliki
Mkapa alifanya kazi kubwa lazima tumuenzi lakini tuepuka yale yaliyomfelisha
 
View attachment 3152750

Kituo cha Ubia nchini kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PPPC) kimeendesha Mafunzo maalumu kwa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa( TAMISEMI )

Mafunzo hayo ya siku moja yalilenga kuwajengea uwezo Wahesimiwa Wabunge hao wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano ili kutoa picha pana juu ya muundo na majukumu ya PPP - Cetre hapa Tanzania.

Mambo mengine muhimu ambayo yamejadiliwa katika semina hiyo ni pamoja na umuhimu wa kutumia PPP katika kutekeleza Mipango mbalimbali ya Taifa ya Maendeleo ya nchi, muundo wa kisheria na Kitaasisi katika utekelezaji wa mipango ya PPP Tanzania.

Mambo mengine ambayo yalijadiliwa ni pamoja na dhana ya PPP na Orodha ya miradi ya mbalimbali PPP iliyoandaliwa chini ya Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini.

Mkurugenzi wa PPPC Tanzania Bw. David Kafulila ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa PPPC inatarajia kuvuta mitaji toka sekta binafsi yenye thamani ya US$9 billion au TZS25 trillioni kwaajili ya Utekelezaji wa miradi midogo ya kati na miradi mikubwa kwa manufaa ya Taifa.

Kwasasa, Tanzania inatekeleza zaidi ya miradi 84 kupitia PPP kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo miundombinu , Umeme wa maji pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo endelevu.

David Kafulila ameiambia kamati hiyo ya Bunge kuwa miradi iliyo kwenye mtiririko wa PPP iko katika hatua mbalimbali za kiutekelezaji kama Upembuzi yakinifu, hatua ya kuandaa mikataba, mingine iko katika tathimini, Manunuzi na mingine iko katika hatua ya uandaaji wa maandiko ya miradi.

“Miradi muhimu kama barabara za kulipia toka Kibaha-Chalinze US$340millioni sawa na TZS 888bn pamoja na Ujenzi wa barabara za mzunguko kwa Jiji la Dar es salaam ambazo zitafuta kabisa foleni wenye thamani ya US$1 billioni karibu TZS 2.7trilioni,
Miradi hii yote inaendelea vizuri" alisema Mkurugenzi huyo wa PPP Bw David Kafulila.

Faida kuu kwà PPP ni kuifanya Serikali ya nchi husika iweze kutekeleza miradi yake mbalimbali ya maendeleo kwa faida ya Wananchi wake lakini pasina kutumia Kodi wala tozo toka kwa wananchi wake hivyo kupunguza maumivu ya Kodi na kuisaidia Serikali hiyo iweze kutekeleza miradi mbalimbali ambayo tu haiwezi kuvuta au kuvutia wabia wa PPP.

View attachment 3152755
Kazi ni nzuri
 
Hongera sana Rais SAMIA
 
HIlo la miaka 10 halitawezekana. Fikiria kampuni ijenge barabara ya kulipia kutoka Chalinze mpaka Kibaha, hao watumiaji watakuwa wanalipia kiasi gani kila wakipita, kiasi kwamba hela ya hiyo kamapuni itakayojenga irudi na hiyo kampuni ipate faida ndani ya miaka 10?

Kwa vyovyote hii miradi itakuwa ya ubia kwa miaka siyo chini ya 90, kama lilivyo jengo la Mlimani City.
Mkuu Sheria ya PPP MAX TERMS ni 25YRS

#MAMA SAMIA YUKO MAKINI SANA
 
Back
Top Bottom