PPPTZ: Bil 948.5TZS kukarabati Uwanja wa Sabasaba Dar es salaam sasa biashara ni 24|7 sio kusubiri tena msimu wa SabaSaba, Heko PPPC

PPPTZ: Bil 948.5TZS kukarabati Uwanja wa Sabasaba Dar es salaam sasa biashara ni 24|7 sio kusubiri tena msimu wa SabaSaba, Heko PPPC

H

Hebu tufundishe mkuu maana ya trade Fair

kwa kiswahili tunaita maonyesho ya sabasaba, maana yake ni kwamba kampuni mbali mbali huja na kuonyesha bidhaa zao, teknolojia zao mpya na kuzitangaza kwa wateja, sasa kama unaona nchi haioni umuhimu wa tradefair maana yake ni kwamba hawana cha kuonyesha, hivyo inarudi nyuma haiendi mbele …
 
nani amekudanganya, ni kwamba hamuelewi maana yake tatizo liko hapo, mnaona tu eneo basi udenda unawatoka …
Hayo yanayofanyika hapo mtoni yote yanafanyika kwa smartphone yako meku 24/7 😂😂😂✔️
 
kwa kiswahili tunaita maonyesho ya sabasaba, maana yake ni kwamba kampuni mbali mbali huja na kuonyesha bidhaa zao, teknolojia zao mpya na kuzitangaza kwa wateja, sasa kama unaona nchi haioni umuhimu wa tradefair maana yake ni kwamba hawana cha kuonyesha, hivyo inarudi nyuma haiendi mbele …
😁✔️🇹🇿
 
View attachment 3376595
==
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) inatarajia kuanza utekelezaji wa mradi mkubwa wa uboreshaji wa Uwanja wa Maonyesho wa Mwalimu Julius Nyerere, maarufu kama Viwanja vya Sabasaba kwa njia ya Ubia PPP.

Uwanja huo wa kisasa Ukanda Mzima wa Africa Mashariki unatarajiwa kutumia US$322M karibu sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 948.5bn ambazo zitatoka kwa wawekezaji wa Ubia baina ya Serikali (TanTrade) na Sekta binafsi.

Kwa ujumla wake Mradi huu una lengo la kuboresha viwanja hivyo vya Maonyesho ili kuvifanya kuwa kitovu cha biashara Africa ili kuendana na viwango na matakwa ya biashara za kimataifa na hadhi ya Tanzania kwa sasa.

Baada ya ukarabati na Ujenzi huo uwanja huu badala ya kutumika kwa kipindi flani maalumu katika mwaka sasa utatumika masaa 24|7 kwa ajili ya biashara jambo ambalo litaongeza Kodi na mzunguko wa pesa hasa Kwa Mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bi. Latifa Khamis, amesema mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia na sekta binafsi, kama sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuvutia mitaji, Teknolojia na Ujuzi pamoja na uwekezaji kutoka mataifa mbalimbali, watu binafsi au makampuni binafsi.

“Mradi huu utahusisha ujenzi wa miundombinu ya kisasa inayojumuisha kumbi za kimataifa za maonesho, maeneo ya biashara, huduma za kidijitali na maeneo ya burudani, malezi na hoteli. Lengo ni kuhakikisha uwanja wa Sabasaba unakuwa kitovu cha maonesho na biashara kwa Ukanda Mzima wa Afrika Mashariki,” alisema Bi. Latifa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Center), Bw. David Kafulila, alisema uwekezaji huo una umuhimu mkubwa katika kukuza Sekta ya bidhaa na huduma nchini, ambayo ni moja ya nguzo kuu za ukuaji wa uchumi wa Taifa la Tanzania.

“Mradi huu ni mfano bora wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na Sekta binafsi hapa nchini.

Mradi huu utasaidia kuongeza mchango wa sekta ya huduma katika pato la taifa sambamba na kuipunguzia Serikali mzigo wa kifedha kwa kuwezesha utekelezaji wa miradi mingine ya kimkakati,” alisema Kafulila.

Mradi huu unatarajiwa kubadili kabisa taswira ya uwanja wa Sabasaba na kuongeza ushindani wa Tanzania katika sekta ya biashara ya maonesho kimataifa.

Hata hivyo Rais Samia baada ya kumteua Bwana David Kafulila kama mkurugenzi wa kwanza wa PPPC tukumbuke pia kati ya nchi 195 dunia ni nchi 26 tu ikiwemo Tanzania ndio zina vituo kamili vya uwekezaji Kwa Ubia PPPC na huu ni utaishi alionao Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na ndio maana katika hotuba zake 34 za maswala ya kiuchumi 50% au nusu ya hotuba hizo alizungumzia Ubia na PPPC.

Hata hivyo PPPC pamoja na mradi huu Miradi mingine mingi imeanza kutekelezwa katika hatua mbalimbali hasa Ile iliyofuata Sheria ya PPP, Kwamfano mpaka sasa tayari miradi minne (4) ya mabasi ya mwendokasi Dar es salaam DART imesainiwa yenye jumla ya thamani ya zaidi ya TZS 600bn pamoja na Ile ya DDC business complex , Ubungo east Africa Complex , Bandari et el,

Hongera PPPC, Hongera TanTrade
Soma pia Govt unveils Sh948.5bn PPP plan to turn Sabasaba into economic hub

===
Kariakoo haitoshi? So wachina wanahamia huko kuendeleza uchuuzi?
 
Kila sehemu mnataka kuweka Machinga, hadi pori la Mabwepande. Hawa viongozi wetu wanaishi dunia ya pekeyao kabisa.
Taifa la Wachuuzi, Dar yenyewe imejaa Frame hadi Jeshini na wanaona haitoshi wanapeleka hadi Sabasaba?
 
Hii ni ku atract uchuuzi, huwezi kuwa na Trade fair mwaka mzima, haiko kokote kule, ni ushamba na ujinga.

hapo wameona eneo, wanalitaka kuuzia imports zao ktk china na kuendelea kuua bidhaa zinazotengenezwa tanzagiza …
 
hapi wameona eneo, wanalitaka kuuzia imports zao ktk china na kuendelea kuuwa bidhaa zinazozalishwa tanzagiza …
ndio lengo kuu, ile kariakooo yenyewe ni kituo cha kuua viwanda vya ndani na kama haitoshi bado wanapeleka hadi Sabasaba na bado kina ile ya Ubungo, hakuna Idea za kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hasa kwa ajili ya ku export
 
Umeongea point to note, Mchina asipewe ruhusa ya kuuza bidhaa zake au namna gani?
ndio lengo kuu, ile kariakooo yenyewe ni kituo cha kuua viwanda vya ndani na kama haitoshi bado wanapeleka hadi Sabasaba na bado kina ile ya Ubungo, hakuna Idea za kujenga viwanda vya kuzalisha bidhaa hasa kwa ajili ya ku export
,
 
Kariakoo na ile ya Ubungo hazitoshi kuwa vituoa vya uchuuzi? yaani badi na vuwanja vya Sabasaba tena wanapeleka wachuzi? yaanu waanenda kusidaia China kukuza uchumi wao, hizi ni akili za kijinga sana
 
Back
Top Bottom