PPPTZ: TANROADS yatangaza miradi 6 ya barabara za PPP zenye urefu wa km 969

Porojo tu.kuna Wachina walikuja na mahela ya kutaka jenga Barbara ya kwenda Dodoma 4 Lanes. Wamepigishwa kwata kisawasawa kwenye corridors za TANROADS awana hamu.Leo wanakuja na matangazo 😁😁
Hiyo sasa ndivyo sheria inataka tufanye. Wachina walikuja TANROADS na wazo/ proposal ya kujenga barabara. Hawapewi hivihivi lazima washindanishe. Madhumuni ya Public Procurement Act ni [Sura ya 410] ni kuweka mfumo thabiti wa uwazi, ushindani, na ufanisi katika matumizi ya fedha za serikali. Sheria inalenga kuhakikisha taasisi za umma zinapata thamani halisi ya fedha (value for money), kudhibiti rushwa, na kukuza ushiriki wa wazabuni wa ndani na wa nje
 
Porojoooooo tuuu hizooo hamna kituu
Tatizo linaanzia pale barabara ilikuwa ya umma unaibadilisha kwenda PPP inakuwa ya kulipia halafu bila kutengeneza mbadala wa barabara nyingine ya umma.

Matapeli wengi sana nchi hii
 
Kungekuwa na sheria wabadhirifu wa Mali za umma kunyongwa na wezi kufungwa Maisha Watz ni wakarimu sana wangechanga hiyo Tril. 2.9 ila sasa viongozi wetu ni wabinafsi sana.
Kabisa.
 
Haina ubaya
Ubaya upo PPP inatakiwa wajenge barabara nyingine siyo kubadili barabara ya umma kuingiza kwenye PPP.
Mfano ukibadili Morogoro Road ikaingia kwenye PPP maana yake watumiaji wote wa hiyo barabara unawalazimisha kulipia kwa sababu hawana chaguo jingine.
 
💩💩💩
 
Sweet talk. Watengeneze Barbara ya Singida Katesh.
 
Kwa kuwa swajatangaza Barabara ya Dar-Mbeya-Tdm basi hii Haina maana
 
Nzuri
 
Imetangaza wapi, kwenye website yao ya tanroads na pppc hakuna project iliyotangazwa.Mi sioni popote walipotangaza hebu nisaidieni nione
 
Sawa sawa
 
Kuna kesi kuhusu daraja la kigamboni, hapo wanatengeneza mgogoro mwingine sababu wananchi wamekuwa wakikatwa pesa kupitia tozo za mafuta, uagizaji bidhaa toka nje halafu leo uwaambie walipie barabara sio sahihi.
Cag akague zile pesa zinazokatwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara zinaenda wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…