Pre GE2025 PPR News Analysis : Kurejeshwa kwa Makamba ina maana kuna watu wamepwaya! Bado Nepi na Konda Boy!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ww ndio unajua sio chawa, lakini sifa zote za uchawa unazo.
 
Kwanini tunaogopa kuusema ukweli? Hivi sasa CCM haina wanasiasa imeishiwa, siku hizi CCM haijengi wanasiasa inategemea sana machawa na manyangarakasha yasiyo na faida za muda mrefu, turejee kisa cha kumteua Wasira! Hana tofauti na Biden, pamoja na usemi jungu kuu halikosi ukoko lakini jungu hili liliungulia dona kwa chai halifai.
 
Kale "kakofi" alikopigwa kalisababishwa na nini?
Tukikajua tutatoa mchango mzuri zaidi,badala ya kupapasa papasa
 
Hakuna kupwaya ni kila mtu ana aina yake ya utendaji, CCM kama wanavyofikiria kumrejesha humphrey polepole Lumumba, na Kama sio kanali Ngemera lubinga au Dr. Bashiru sababu wanajua hao ndio watu wanaweza ku counter propaganda za Upinzani.
Mzee Wasira ni lazima apate attacking midfielder wenye viwango na wametumia ujanja kumtia kambani Dr Slaa maana Wakutane Slaa, Lissu, Heche hayo mawe yatakayorushwa inabidi kuwe na opposite fair reaction kutoka ccm.

Juzi Heche kaanza na episode ya ubadhirifu wa SGR part gazzete wanaita uswahilini, CCM kama alivyosema Musiba wanahitaji vichwa kama Polepole na Bashiru ku counter propaganda za chadema.

It was a matter of time kwa January kurudi na nadhani alitolewa kwa majungu tuu maana january ana nyota ya odinga sio watu wote wanamuelewa ila wenye akili huwa wanamuelewa sana. Ila Nape hana kitu cha maana sana wala asirudishwe apambane na Steve Membe jimboni.
 
Hakuna kupwaya ni kila mtu ana aina yake ya utendaji,
Una maana kupwaya wewe hujakuona?, kumetokea mgogoro kwa jirani waasi wameshika usukani, nchi yako inapewa fursa ku host mazungumzo kutafuta suluhisho, mtaitana wakubwa watupu, kuzungumzia amani ya eneo hilo huku hao waasi wenye eneo kibindoni, mmewaacha!. Hili dogo?. Huku sio kupwaya?.
CCM kama wanavyofikiria kumrejesha humphrey polepole Lumumba, na Kama sio kanali Ngemera lubinga au Dr. Bashiru sababu wanajua hao ndio watu wanaweza ku counter propaganda za Upinzani.
Japo mimi ni kada, kuna mambo ya ndani siyajui, Polepole is the best kwenye sera na kuandaa ilani, wananchi wa kawaida wa hali ya chini, hawahitaji ilani, wanahitaji amsha amsha, Konda Boy is the best kwenye eneo hilo!.
Mzee Wasira ni lazima apate attacking midfielder wenye viwango
Mzee Kijana Wasira is good
na wametumia ujanja kumtia kambani Dr Slaa maana Wakutane Slaa, Lissu, Heche hayo mawe yatakayorushwa inabidi kuwe na opposite fair reaction kutoka ccm.
I just don't believe this,
Juzi Heche kaanza na episode ya ubadhirifu wa SGR part gazzete wanaita uswahilini, CCM kama alivyosema Musiba wanahitaji vichwa kama Polepole na Bashiru ku counter propaganda za chadema.
CCM ina hazina kubwa.
It was a matter of time kwa January kurudi na nadhani alitolewa kwa majungu tuu maana january ana nyota ya odinga sio watu wote wanamuelewa ila wenye akili huwa wanamuelewa sana.
Naunga mkono hoja
Ila Nape hana kitu cha maana sana wala asirudishwe apambane na Steve Membe jimboni.
Itakuwa hujui Nape ndie mfungaji wa bao la mkono!.
P
 
Hivi kwenye chess /Draft SI hakuna option ya kuingiza kete za nje?

Ila hii siyo Chess Wala draft siyo ...

Grand Master
 
Safi, mwalimu wa sayansi ya siasa. Uchambuzi makini lakini wanasiasa wanapaswa kuteua watu makini ili wasiwabadilishe Hawa wasaidizi wao kila mara. Maana kuwabadili kila mara ni kama vile hawaaminiki vile, na Tena ufanisi wao ni mdogo pale kiongozi anapopata uzoefu katika wizara,halafu umpeleke wizara nyingine, matokeo hakuna ufanisi.
 
Nje ya mada, hivi hakunaga viongozi wapya huko ccm hadi kurudishwa wale walee tu wakati walishakosea tena zaidi ya mara 1...hii nini maana yake?!.
Ni mwendo wa kubebana na ukikataa unatishiwa kurogwa 😄
Kuna familia wamo tangu Uhuru na wajukuu ni wabunge na mawaziri watarajiwa
 
Kaka yangu Mayalla majuzi umenikoea sana , maandiko yako nimeanza kuyachukia mkuu
 
Waziri wa FA wa sasa amejaaliwa.utendaji.wake kwa.maarifa mungu aliyompa na akifuata policy yetu pia. Yaani.uwezo.wake ndio.umeishia hapo.

Kuandaa mkutano wa kusaka suluhu ya eastern congo bila kuwaalika M23. Sidhani kama ni uamuzi wake binafsi. All in all Makamba anahitajika whether watu wanapenda au hawapendi.
 
Mimi sijui ni nini cha kumpongeza mama isipokuwa kumlaumu kwa kutokuwa na principles za kufanya maamuzi na kujikuta unateua, unatengua, halafu unateua tena na kutangua tena. Haya mambo sio ya kupongezwa kwa mtu yeyote aliye na ukweli katika matendo yake. Tunapaswa kumlaani mama kwa udhaifu huu mkubwa. Waandishi "nguli" kama nyie mlipaswa kuwaelewesha watu vizuri na pia kulisemea kwa kweli yake, ila badala yake mnatumia ujinga juu wa rais kumpongeza na kujipendekeza kwake. Trump yupo sahihi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…