Pre-primary education/chekechea imeleta impact yoyote katika elimu ya Tanzania au ni upotevu wa pesa tu?

Pre-primary education/chekechea imeleta impact yoyote katika elimu ya Tanzania au ni upotevu wa pesa tu?

Hizo shule ni kwa ajili ya watoto waliozaliwa kwenye Familia zisizo na akili!

Nakaribisha maswali.
 
Kwa upande mwingine wanasema ukichagua kufanya mambo bila hekima then jiandae kulipa gharama kubwa.

Hili la kulipia watoto baby class kwa gharama kubwa ni matokeo ya wazazi wasio na utashi wa kulea watoto wao wenyewe kuwaachia wengine jambo ambalo si la hekima. Mtoto kuanzia 0 hadi uzee analelewa na baba na mama yake na katika miaka hiyo ya awali ya kati ya 0 hadi 18 mtoto anatakiwa kuwa karibu zaidi na baba na mama yake kwenye malezi kwa
 
Ukiacha kujifunza "what is your name"Kama ulivyosema lkn pia mtoto anajifunza kusocialize na watoto wenzie pia michezo mbalimbali. Maana huwezi kuwa na kila kitu anachohitaji mtoto nyumbani.
Halafu walimu ni professional katika kufundisha watoto lkn sio kila mzazi ni mwalimu.
Tatizo watu wanachukulia early childhood development kimzaha, kumbe ndio makuzi ya mtoto huanzia huko. Kindergarten sio kujifunza kusoma na kuandika tu la, kuna mambo mengi ya kujifunza huko.
 
Watafiti tusaidieni hi miaka mitatu ya baby prep 1 prep 2 inao tumika na shule nyingi za mjini hususani private zenye gharama kubwa mpaka 1m kwa mtoto kuanzia 3- 6yrs kuanzia miaka ya 90s imeleta matokeo chanya katika makuzi na malezi ya watoto wetu ukiangalia performance ya hao watoto au ni kuongeza mzigo na umasikini kwa mzazi?

Kuanzia miaka ya 80s kurudi nyuma hayo madarasa ya prep hayakuepo mtoto alivokua na miaka 5 au sita alianza darasa la kwanza, au akianza kung"oa meno ya mbele au kushika sikio lake kwa kupitisha mkono, alianzishwa shule, kwa sasa hao wengi ndo wana siasa wetu na watumushi wa ummah walio wengi.

Suali langu je ukili nganisha utendaji wao hao ambao hawakusoma chekechea na hawa wahitimu wa miaka kuanzia 2000 kuna tofauti? Yupi ni imara zaidi?

Nisihukumiwe vibaya kwamba madarasa ya chekechea hayana umuhimu ila yanachosha wazazi kusomesha nakutumia pesa nyingi kama haina mchango bora mtoto anze darasa la kwanza moja kwa moja hizo pesa ununue kiwanja uanze maisha mdogo mdogo kuliko kipanga nyumba ya 1.2m kwa mwaka na ada ya chekechea ni 1 2m kwa mwaka wastage of resources.
Kijijini nilipo mtoto chekechea mwaka mmoja, lifuatalo ni darasa la kwanza mambo yanasonga. Na watoto mpaka la kwanza linaisha anajua kusoma na kuandika
 
Ki vip tupe msaada wa hayo madarasa kwa jamii yetu ya Tanzania isije ikawa kwamba boda boda au madalali walio shamiri wengi wasasa ni wahitimu wa hayo madarasa na hazi yao kwa sasa ndo hiyo
Ila, wengi mijini wanalazimika kupeleka watoto shule mapema pia sababu ya changamoto za malezi. Baba na mama..au kama ilivyo siku hizi mama(single) wapo busy anaona bora tu mtoto aende shule kwaajili ya company, mtoto asikae tu nyumbani na mdada wa kazi na tv
 
Umenikumbusha 200 ya noti
Tulikua tunalipa 200 kila wiki kwa ajiri ya uji na karo
 
Tatizo watu wanachukulia early childhood development kimzaha, kumbe ndio makuzi ya mtoto huanzia huko. Kindergarten sio kujifunza kusoma na kuandika tu la, kuna mambo mengi ya kujifunza huko.
Kabisa yaani. Yaani mtoto uwe nae ww tu ndani, si atakuwa wa hovyoo
 
Mimi nilifundishwa kusoma, kuandika, kuhesabu nyumbani nikiwa na Miaka mitano tuu nilikuwa nimeshajua kusoma na kuandika na kuhesabu.

Alafu kufundisha Mtoto haichukui hata Lisaa limoja. Ukitenga kîla Siku Lisaa limoja la kumfundisha, Kwa Ratiba maalumu Mtoto anakuwa Vizuri.

Binafsi nitafundisha Watoto wàngu mwenyewe hasa zile basic knowledge.

Labda itokee Dharura kama Kifo au Mama zào wawanyang'anye Kutoka kwangu Kwa maana pia siwezi kung'ang'ania Mtoto na Mwanamke aliyezaa Kwa uchungu
 
Zamani nani alikua analea watoto wao, hizi shule za chekechea hata vijijini mawilayani zipo ambao hamna haja ya kulea watoto.
Ilikuwa kinyume cha haki za mtoto hasa huko.vijijini

Wanaenda shamba toka asubuhi hadi jioni kitoto kiko kimekaa Juani au kukaa tu chini ya miti au kinazagaa tu nyumbani

Shule za chekechea zimewapa kitu cha kufanya productive cha kuongeza kitu kwenye akili yao badala ya vyenyewe kubaki tu empty kama vibwege majumbani wazazi wakiwa kazini au shambani
 
Ukiacha kujifunza "what is your name"Kama ulivyosema lkn pia mtoto anajifunza kusocialize na watoto wenzie pia michezo mbalimbali. Maana huwezi kuwa na kila kitu anachohitaji mtoto nyumbani.
Halafu walimu ni professional katika kufundisha watoto lkn sio kila mzazi ni mwalimu.
Kwani nyumbani hakuna watu wa ku socialize nao, socialisation haina mwisho popote mtoto ana socialise hata kwenye public parks social function sehemu za ibaada sherehe za nyumbani, kwanini nilipie 1.2m kwa socializong tu.
 
Kwa upande mwingine wanasema ukichagua kufanya mambo bila hekima then jiandae kulipa gharama kubwa.

Hili la kulipia watoto baby class kwa gharama kubwa ni matokeo ya wazazi wasio na utashi wa kulea watoto wao wenyewe kuwaachia wengine jambo ambalo si la hekima. Mtoto kuanzia 0 hadi uzee analelewa na baba na mama yake na katika miaka hiyo ya awali ya kati ya 0 hadi 18 mtoto anatakiwa kuwa karibu zaidi na baba na mama yake kwenye malezi kwa
Na hao watoto ambao wamelelewa na wazazi mama na baba, wakianza shule ni more guineas kuliko hao wa baby class atakiakili za kupamnana na maisha ni wazuri kuliko hawa wa whats your names.....
 
Tatizo watu wanachukulia early childhood development kimzaha, kumbe ndio makuzi ya mtoto huanzia huko. Kindergarten sio kujifunza kusoma na kuandika tu la, kuna mambo mengi ya kujifunza huko.
Yapi hao ambao nyumbani hayapatikani?
 
Ila, wengi mijini wanalazimika kupeleka watoto shule mapema pia sababu ya changamoto za malezi. Baba na mama..au kama ilivyo siku hizi mama(single) wapo busy anaona bora tu mtoto aende shule kwaajili ya company, mtoto asikae tu nyumbani na mdada wa kazi na tv
Unataka kusema pre primary ni kwa ajili ya ma singo maza kupata company kwa watoto wao?
 
Mimi nilifundishwa kusoma, kuandika, kuhesabu nyumbani nikiwa na Miaka mitano tuu nilikuwa nimeshajua kusoma na kuandika na kuhesabu.

Alafu kufundisha Mtoto haichukui hata Lisaa limoja. Ukitenga kîla Siku Lisaa limoja la kumfundisha, Kwa Ratiba maalumu Mtoto anakuwa Vizuri.

Binafsi nitafundisha Watoto wàngu mwenyewe hasa zile basic knowledge.

Labda itokee Dharura kama Kifo au Mama zào wawanyang'anye Kutoka kwangu Kwa maana pia siwezi kung'ang'ania Mtoto na Mwanamke aliyezaa Kwa uchungu
Wakwangu wanafundishwa nyumbani na mama yao mpaka miaka 5 ndo wana enda shule bahati nzuri mke wangu ana ujuzi wa ualimu ila sotaki ajiliwe kwahiyo mda wake yeye na watoto wake, nafanya saving kubwa, gharama ya pre- primary sio rafiki kwa wage earners.
 
Unataka kusema pre primary ni kwa ajili ya ma singo maza kupata company kwa watoto wao?
😂 usinichonganishe, ila watoto wengi wa wazazi mmoja wasio na support ya ndugu (wazazi, ndugu wengine) na mzazi huyu huyo ndio anaweka mkate mezani, hupeleka watoto wao shule mapema zaidi kuliko watoto wa wazazi wawili

Ningesema kitu kingine ila mtanichoma moto na mifano kedekede to prove me wrong. Niishie hapa.
 
[emoji23] usinichonganishe, ila watoto wengi wa wazazi mmoja wasio na support ya ndugu (wazazi, ndugu wengine) na mzazi huyu huyo ndio anaweka mkate mezani, hupeleka watoto wao shule mapema zaidi kuliko watoto wa wazazi wawili

Ningesema kitu kingine ila mtanichoma moto na mifano kedekede to prove me wrong. Niishie hapa.
Tumekuelewa mimi watoto wangu wana mama wa nyumbani graduate tena katika fani ya ualimu siwezi kupoteza 1m kwa ajili ya baby class, wakati sio singo maza wanao tafuta kapani ya watoto wengine, teaching/learning aid zote zipo nyumbani kuna extra reading room hufanya kama class room.
 
Now days people are very busy
Ukilijua hili utajua kuhusu hiyo inaitwa Vidudu.

Mtoto anayepelekwa shule at 2 yrs nyuma yake ni kuwa wazazi hawana muda wa kulea.
 
Now days people are very busy
Ukilijua hili utajua kuhusu hiyo inaitwa Vidudu.

Mtoto anayepelekwa shule at 2 yrs nyuma yake ni kuwa wazazi hawana muda wa kulea.
Hawana mda kulea na pesa hawana bado wansishi kwenye nyumba za kupanga nyumba, kwahiyo ubizy wao hauna faida.
 
Back
Top Bottom