Precision Air versus FastJet, Nani zaidi

Precision Air versus FastJet, Nani zaidi

If this happens I will be preaching first and second service in Dar and third at around 1600hrs in Isamilo Mwanza and then will board the last flight at around 1900hrs. But yangu macho ndugu zangu, you are Blessed!!!
 
Yaani hapo ni kujipiga na kiporo au Mihogo ya kuchoma kisha unashushia na maji ndani ya fast jet!
 
wakuu

Kweli ujio wa fastjet unaweza kuua si precision air tu, hata biashara za mabasi, mathalan uwanja wa songwe Mbeya ukikamilika mwezi ujao na wao wakaanza kuleta dege lao huku nani atahangaika na mabasi[nauli 30000 hadi 45000] safari masaa kumi.
 
Kiboko ya ushindani, Precision air wamepunguza kwa kiasi kikubwa nauli ya dar-mwanza-dar
 
Kiuchumi, serikali makini haiwezi kufanya hivyo. Wanaopanda ndege ni asilimia ndogo sana ya watanzania. Kodi inayokusanywa kwenye mafuta ya ndege ikitumika vizuri inafaidisha watanzania wengi zaidi kuliko hawa wanaotumia usafiri wa ndege. Kuondoa kodi kwenye mafuta ya ndege ni sawa na kuondoa ziwa mdomoni mwa kichanga na kumpa baba yake.
Wale wale!. mbona unafikiria karibu sana we mangi?. Hivi bei ya mafuta ikiwa chini na kuwezesha usafiri wa ndege kuwa say chini ya Tshs 50,000 kwende popote TZ , nani atapanda haya mabasi mikangafu? Kodi yetu inayoishia Uswisi na jersey ndiyo unayoililia?
 
Mi napenda competition kama hiz tunakaribisha makampuni mengine yaweze kuja ili usafiri wa anga uwe wa kawaida.wasi wasi wangu ni long last ya fast jet je atweza kumantain status yake hasa huduma binafsi nimesafiri sana na precision mpka nje ya nchi huduma zao ni nzuri ukiachilia mbali changamoto ndogo ndogo za kibinadamu ingawa pia bei yao kubwa so mi nawatakia kila la heri fast jet wadumu,ingawa pia nasikiaeti ni sister company na fly 540 ambao nao ni kama wamekufa maana flight zao zilikuwa hazielweki nimesafiri kama mara 4 from MZA-KIA-ZBAR-DAR huduma zao mbovu.Pia nasikia hawa fast jet wnatoza mbaya kwenye mizigo wale wenzangu na mimi tukisafiri tunabeba mafurushi huku itawacost mana nypesi zinasema wanachaji elfu 8 kwa kilo labda kama wana jf nyie mmepata hizi nyepesi mni update.
 
FastJet inaleta changamoto kubwa kwa Precision air na hii ni nzuri lakini ni hatari sana kwa usafiri wa anga Tanzania kwa sababu FastJet hawawezi kwenda routes nyinginezo ukiacha ya Dar-Mwz na Dar-KIA. Dege lao kubwa vile kwanza haliwezi kutua mfano Mtwara na hakuna abiria wa kutosha kwenda kwenye destinations nyingine zaidi ya Mwz na KIA. Sasa kama Precision air ikifa hii fastjet itaweza kutoa huduma mikoa mingi kama precision wafanyavyo kwa sasa? kwa maneno hayo nisingependa Precision air ife!!

Precision air wajifunze kwamba competition is stiff and many more new entrants in the market are there to come. Waboreshe huduma ili abiria wasiwakimbie. Kuna watu kulipa laki 4 sio tatizo kwao bora tu huduma iwe nzuri. All in all competition in the service industry is a good thing. So Viva FastJet

HAWA WATU WAMEINGIA NA UJANJA MWINGI KWELI KUTANGAZA KUWA BEI NI NDOGO LEO HII NIMETOKA KUKATA TIKETI YA KWENDA Dar na kurudi nimelipa TZS 150,000/= ya tarehe 10.12.2012. bado hakuna laguage allowance ukikamata kinywaji unalipia cheaper things are not always cheaper air precision isife ushindani ndio utakao tuokoa na bei za ajabu.
 
Inaonesha kweli jamaa wamejipanga kibiashara ,wasiwasi wangu wasije hujumiwa kama community air line. Lakini nilipata moyo baada ya kumsikia mtaalamu mmoja wa aviation alipokuwa akisema kuwa ,low cost airline wanajipanga rasmi kufanya biashara africa, na moja ya vikwazo alivyokuwa anazungumzia ni hujuma . Inawezekana Fast jet ikawa ni mkombozi.
 
Watu wanajali nini kunywa , kula. Mbona kwenye daladala unakaa masaa hata mawili hawatoi maji au chochote na joto kibao. Cha muhimu ni kufika, after all safari ya Dar/Mwz ni saa moja na nusu. Kwa raha twende Rock City, tukale samaki bana!!!
 
Biashara ya usafiri wa anga ni kama kamari hapa tz. nakumbuka rafiki yangu alinishawishi sana kununua hisa za precision nikakataa. Kwa kweli naona nilifunuliwa kutokununua! risk na uncertainty ni nyingi mno
 
fastjet ni ndugu moja na easyjet hivyo hawa jamaa wana uzoefu mkubwa ktk masuala ya uendeshaji wa cheap frights, mpinzani wao lazima awe makini
 
Wale wale!. mbona unafikiria karibu sana we mangi?. Hivi bei ya mafuta ikiwa chini na kuwezesha usafiri wa ndege kuwa say chini ya Tshs 50,000 kwende popote TZ , nani atapanda haya mabasi mikangafu? Kodi yetu inayoishia Uswisi na jersey ndiyo unayoililia?


Nikupongeze wewe kwa kufikiria mbali meku. Kwenye comment yangu ya kwanza niliweka tahadhari" ikitumika vizuri". Ninafahamu kuwa kuna mapungufu makubwa kwenye mfumo wetu wa kukusanya na kutumia kodi, lakini pia ninatambua kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa serikali kuongeza makusanyo ya kodi ili kuweza kutoa huduma kwa watanzania wengi zaidi. Hebu jiulize, ni watanzania wangapi watakaoweza kumudu hiyo nauli ya 50,000? Kuna maeneo ambayo serikali ikipunguza kodi itagusa maisha ya watanzania wengi zaidi kuliko huko kwenye mafuta ya ndege.
 
Huwezi kuoperate airbus kwa nauli ya 32k kwenda Mwanza!!!

I guess hiyo 32k ni offer ya ticket chache lets say 10% ya tickets for every flight, Marketing strategy
Mbona inawezekana sana? Hii hapo chini ni mifano tu na bei huwa zinapungua zaidi ya hizo:
ryanair.PNG
 
Mbona inawezekana sana? Hii hapo chini ni mifano tu na bei huwa zinapungua zaidi ya hizo:
View attachment 72859

Unapoweka hizo bei utuwekee na tozo za uwanja, kodi, bei ya mafuta ya ndege, ili tuweze kulinganisha na za huku kwetu...10% ya waziri, naibu, katibu mkuu, Ewura, TAA, and many other factors
 
Bado ATCL na Sky Aviation bei lazima zishuke kwa kasi mno tupate unafuu
 
kwa mtazamo wangu ni kwamba FAST JET wamekuja na aidea nzuri sana unajua makampuni ya ndege yameshakuwa mengi kama ilivyo kwa makampuni ya simu unapoona tigo wameshusha bei na voda watafuata au airtel na zantel pia ukishindwa utaondoka. ndivyo pia Fast jet ameleta changamoto nzuri kwenye makampuni ya ndege. haijalishi unatumia boiling au sijui nini kinachoitajika ni kuwa na wateja so kitendo cha fast jet kushusha bei hata presition nao watashusha pia. Ni hivi mimi ninavyoona upande wangu ni kwamba sikuzote technology inatitaji utake risk kwa unachokiitaji nikuwa na maana hii endapo wakiona fast jet kafanikiwa na anafanikiwa na wengine wote watafanya hivyo kama mtakumbuka Tigo ilikuwa kampuni ya kwanza kutangaza shilingimoja kwa sekunde na extreme baada ya yeye kujakutangaza mapato yake kwa wiki na mwezi ngio kampuni zingine zilipoanza kufuata hivyo fast jet ni kama HEBU ANZA TUONE KAMA INAWEZEKANA na ndio siku zote ilivyo so sitoshangaa kusikia PRESITION,KAMPALA,KENYA na zingine nyingi nazo zimeshusha bei
 
32,000/= Nadhani VAT na Insurance hazijawekwa hapo nina uhakika mwisho wa siku utalipa zaidi ya hiyo tsh 32,000/=
 
Naomba mie mnipe kazi ya marketing manager precision alafu mje muone kama shairika litafirisika..
 
huyu jamaa wa fast jet biashara anaifahamu kutokana na kuwa na uzoefu katika nchi nyingine pia hii ni short term plan kwamba wanaanza na nauli kdogo halafu wataongeza kulingana na mahitaji ya muda unavyokwenda na kusoma soko lilivyo namuona kama ni mshindani wa kweli kwa kampuni nyingine za usafiri wa anga hapa nchini na barabarani
 
Back
Top Bottom