LGE2024 Preemptive Move Kuisaidia Chadema Ahead of Press Conference ya Mwenyekiti Mbowe Leo, Chadema Wasifanye Kosa la Kurudia Kosa Kususia Uchaguzi wa SM

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
leo kuna press conference muhimu ya Chadema。

hili ni bandiko la kitu kinachoitwa preemptive move ya kuisaidia Chadema ahead of Press Conference hii muhimu ya Mwenyekiti wa Chadema leo,ili kuisaidia Chadema wasifanye kosa la kurudia kosa la kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa!。

Anzia hapa Je, wajua Vyama vya Siasa TZ ni Public Parties? Maamuzi yake lazima yazingatie Public Interest na siyo kufuata ujinga na ubinafsi wa viongozi insane!
Asante sana kwa taarifa hii, ushauri wangu ni atangaze chochote na alalamike vyovyote kuhusu hizi figisu figisu za uchaguzi wa serikali za mitaa, ila hala hala ,Chadema wasifanye kosa kama lile la mwaka 2019 kususia uchaguzi wa serikali za mitaa,hivyo uchaguzi mkuu wa 2020 waliambulia jimbo moja tuu la ngama!,wakasusia kuutambua uchaguzi,na kuuita ni uchafuzi, lakini baada ya maridhiano wakautambua na kuyatambua matokeo!。

Kufanya kosa sii kosa,kosa kurudia kosa, Chadema walifanya kosa kususia uchaguzi ule,uchaguzi huu wasirudie makosa,wasijitoe kwa kususia uchaguzi wa seikali za mitaa!。

Paskali
update
Press Conference Imeisha, Chadema haitajitoa。

Pongezi Chadema kutorudia makosa。
Mungu Ibariki Chadema
Mungu Ibariki Tanzania
P。
 
Wakisusa wenzao wala,

Mpaka sasa CHADEMA imepoteza legitimacy ya kujiita chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Uroho wa madaraka baina yao
Kukosa oneness kwenye misimamo yao
Kukosa agenda ya kitaifa
 
Wakisusa wenzao wala,

Mpaka sasa CHADEMA imepoteza legitimacy ya kujiita chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Uroho wa madaraka baina yao
Kukosa oneness kwenye misimamo yao
Kukosa agenda ya kitaifa

Sema kweli japo inauma
Kwanini mnawakata wagombea wao wote mnabakisha wetu ccm? Unadhani hio ni haki?
 

Ili wauhalalishe huu uchaguzi?
 
1. La kususia halipo. Na labda umesahau kuwa, kwa kanuni za uchaguzi huu wa mwaka huu, hakuna mgombea kupita bila kupingwa. Kama yuko pekee yake basi kuna kura ya NDIYO au HAPANA. Hii ni fursa pia kwa vyama kumpigia kampeni ya "HAPANA" mgombea asiyetokana na wananchi. Ni fursa ya chama pia kujitangaza...

2. PC ya leo likely itahusu mambo mawili au matatu

➡Msimamo wa CHADEMA kuhusu kasoro na uchafuzi wa mchakato wote wa uchaguzi wa vijiji, mitaa na vitongoji 2024 kuanzia uandikishaji wapiga kura, uchukuaji fomu za kugombea, urejeshaji wa fomu hizo, uteuzi wa wagombea na ukataji wa rufaa na maamuzi ya rufaa hizo..

➡Response ya serikali juu ya janga la kuanguka kwa ghorofa Kariakoo na kuua watu kadhaa. Na huku watu wakijiokoa na kuomboleza, Rais Samia Suluhu Hassan yeye akakwea pipa kwenda Brazil kwenye mwaliko wa mkutano wa nchi wanachama wa G20..

➡Kelele za mgogoro ndani ya chama hususani yeye na Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wake. Na kwa hili bila shaka Tundu Lissu atakuwepo kwenye Press Conference hiyo na pengine akawa mmoja wa wasemaji wakuu. Asipokuwepo itakuwa ni dosari kubwa na litakuwa kosa kubwa la kisiasa CHADEMA kulifanya..

Ni mtazamo na maoni yangu tu..
 
Wakisusa wenzao wala,

Mpaka sasa CHADEMA imepoteza legitimacy ya kujiita chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Uroho wa madaraka baina yao
Kukosa oneness kwenye misimamo yao
Kukosa agenda ya kitaifa
Actualy bado hawajapoteza, currently ndio chama kikuu cha upinzani despite ya rafu zote zinazofanywa against them.
Kuna chama kingine chenye upinzani mkubwa zaidi yao?
Yes wana madudu yao, but je hayo madudu ccm hayapo?
I dont think kuna chama perfect
 
Kushiriki kwenye Uchaguzi siyo njia sahihi kwao, lakini pia hata kususia uchaguzi siyo njia sahihi kwao ya kufanya Siasa sahihi kwa hapa Tanzania hivi sasa.

Aidha, Inavyoonekana Kuna mvurugano ndani ya Chadema. Kiini cha kuwepo kwa mvurugano huu huko Chadema kwa maoni yangu ni kutokana na namna Mwenyekiti wa Chama chao hicho Freeman Mbowe kukosa misimamo inayoeleweka kuhusiana na Siasa za nchi hii kwa sasa. Siyo siri hata kidogo, Mbowe akiwa Kama Kiongozi wa Chama Chao hicho, amekuwa ni mtu ambaye Hana msimamo unaoeleweka hali hii imesababisha mkwamo na kuyumba kwa Wanachama wa chama hicho.

Mbowe amekuwa ni mtu asiyeaminika tena kwa sasa ndani ya Chama Chao hicho, watu wengi kwanza wanamchukulia kama ni Mamluki wa Chama tawala ambaye amejipachika kwenye Vyama vya upinzani kwa 'kazi maalumu ya kuvuruga vyama vya upinzani' ili kukinufaisha chama tawala.

'Engine' ya treni ikiharibika mabehewa yote ya treni nayo huyumba na kusimama!

THE WAY FORWARD:
Njia iliyo sahihi zaidi ya kufanya Siasa sahihi kwa hapa Tanzania kwa Sasa ni Moja tu: nayo ni KUDAI NA KUPIGANIA UPATIKANAJI WA KATIBA MPYA ILIYO NZURI.
Kupatikana kwa Katiba Mpya iliyo nzuri ndio itajenga Msingi Bora na ulio imara kabisa wa kufanikisha Mambo mengine yote kabisa yaliyo mazuri.

NB: Hakuna Jambo lolote lile lililo zuri ambalo linaweza kufanikiwa kwa Sasa hapa Tanzania bila ya kupatikana kwa Katiba mpya iliyo nzuri kwanza, never!
 
Unaielekeza CDM au unamuelekeza Mkt Mbowe Cha kufanya?

Je akusikize wewe na Si maamuzi ya vikao vya chama?

Je Kuna uchaguzi?
 
Mbowe anaenda kuongelea maafa ya Kariakoo na kuwapa faraja watanzania maana aliyetakiwa kufanya hivyo kaenda Brazil kufanya makeup
 
Kama timu za mpira zilivyo, kadri unavyoshiriki ligi na kupoteza ndivyo unavyopoteza mashabiki na kinyume chake ndio kweli.

CHADEMA kushiriki hizi chaguzi ambazo haziko fair kwao, na wao kutojipanga kunapunguzia kuaminika kwa jamii.

Ni bora kugoma kushiriki huku jamii ikijua ikielewa kwa upana hizo sababu.
 
Wakifanya hivyo watakuwa wasaliti Sana maana mtaani wanasubiri hata iwekwe CCM Na Kuku Ni Bora wachague sura ya Kuku kuliko Chama hiki.

Vipi ukiweka CCM Na sura nyingine ya mwanadamu mwenzao? It's much better of
 
Wakisusa wenzao wala,

Mpaka sasa CHADEMA imepoteza legitimacy ya kujiita chama kikuu cha upinzani Tanzania.

Uroho wa madaraka baina yao
Kukosa oneness kwenye misimamo yao
Kukosa agenda ya kitaifa
Sasa ni kosa hilo au ahueni kwenu CCM..? Jifariji..endelea kungojea kuona bendera za CHADEMA mtaani..!Kilishavuka huko
 
Wanabodi,

Kufanya kosa sii kosa,kosa kurudia kosa, Chadema walifanya kosa kususia uchaguzi ule,uchaguzi huu wasirudie makosa,wasijitoe kwa kususia uchaguzi wa seikali za mitaa!。

Paskali
Pongezi Chadema kutorudia makosa。
Mungu Ibariki Chadema
Mungu Ibariki Tanzania
P。
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…