Prefect wa darasa la 6B mbona hata wewe unatajwa

Prefect wa darasa la 6B mbona hata wewe unatajwa

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1541237463319.jpeg


Ni pale prefect wa shule ya Dodo alipoomba majina ya wanafunzi wote wanaoachia hewa chafu darasani. Anasema amechoshwa na tabia ya wachache wanao haribu hali ya hewa darasani.

Kuna wengi hasa wale ambao wanaomba mwalimu atoke waendelee kucheza. Wao shuleni wanakuja ku social ndiyo hao walikuwa front line kumpa prefect majina. Prefect anasema hata mwenyewe yamemshangaza ma confi waliyokuja nayo jamaa.

Huku nyuma tuna list yetu, hawa ni watu wanaokaa na prefect upande mmoja. Wanasema mbona prefect pia huwa anachafua hali ya hewa? Sasa nani atamfunga paka kengele? Hii list yetu tuipeleke wapi?
 
Tunampelekeaje prefect hii list yetu? Wengine wanasema tutume barua kwa Shule ya Msingi Dodo, SLP...
Bado haitasaidia maana shule ya msingi Dodo ndiyo wamemwamini prefect.
Hapo mtihani upo. Au labda tujaribu kutuma barua ila sina uhakika kwamba itasaidia.
 
Hata prefect akiandikwa unafikiri mkuu wa shule atakubali kumfukuza shule ama kumpa adhabu?
 
Back
Top Bottom