Premier League: Man United yaibamiza Liverpool 2-1, Agosti 22, 2022

Premier League: Man United yaibamiza Liverpool 2-1, Agosti 22, 2022

Baada ya kuanza msimu vibaya kwa kupoteza mechi mbili mfululizo, Manchester United imeamka na kuipa Liverpool kipigo cha magoli 2-1 katika mtanange wa Premier League kwenye Uwanja wa Old Trafford.

United haikupewa nafasi kubwa ya kushinda katika mchezo huo, ilipata magoli yake kupitia kwa Jadon Sancho na Marcus Rashford dakika ya 16 na 53 huku goli la Liverpool likifungwa na Mohamed Salah dakika ya 81.

Kocha wa Man United, Erik ten Hag aliwaweka benchi Cristiano Ronaldo na Harry Maguire katika mchezo huo.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Liverpool kucheza mechi tatu bila ushindi wowote msimu huu.
Derby haina fundi
 
Liverpool bado sana hapo hawajakutana na Arsenal msimu huu atagombania top 4 siyo ubingwa.
 
Kwendaa ,,
Una stress za kuchaniwa mkeka na united wewe sio bure
Huoni kama stress unazo wewe sasa maana ungepigwa Jana sijui ungekuwa na hali gani leo ungetuahribia zoezi la sensa ila hongera kuwa kunywa supu ya jogoo
 
Kloop ananiboa sana kwa kukumbatia uhafidhina kwenye mpira wa miguu

Bila shaka ni mwalimu ninayemhusudu sana lkn akishamwamini mchezaji namba atapewa tu

Pia usajili wa kuchechemea kwa epl anaweza asichukue ubingwa tena
 
Back
Top Bottom