J. Mushuku
Member
- Jun 1, 2015
- 17
- 4
Bodi ya premier league ya UK imetoa taarifa juu ya mgawanyo wa mapato kwa timu 20 zilishoshiriki ligi hiyo kwa msimu wa 2014/2015. Jumla ya £1.6 bn ziligawanywa kwa timu hizo ambapo Chelsea ndiyo ilipata pesa nyingi zaidi
Katika mgawanyo huo Chelsea ndiyo iliyoongoza kwa kupata £98,999,554 ikijumuisha mapato ya televisheni, merit money (kulingana na nafasi ya kwenye msimamo wa ligi) na malipo mengine mbalimbali. Timu ya QPR ambayo ilimaliza katika nafasi ya 20 ndiyo iliyopata kiasi kidogo ambacho ni £64,886,028.
Timu ya Man city ilikuwa ya pili (£98,501,832) ikifuatiwa na Man Utd (£96,759,212). Nafasi ya nne ilichukuliwa na arsenal ambayo ilivuna £96,509,758 pamoja na kwamba ilimaliza katika ligi katika nafasi ya tatu juu ya Man Utd ambayo ilimaliza nafasi ya nne.
Katika mgawanyo huo, kila timu ilipata mgawo sawa wa television money, regardless ya mechi ngapi za timu husika zilikuwa broadcasted. Kila timu ilipata £21,968,793 kutokana na domestic broadcasts, na £27,757,371 kutokana na overseas broadcasts.
Pia kila timu ilipata gawio la £4,392,630 kutokana na sponsors wa epl, kama vile Barclays, Samsung etc.
Vilevile kila timu ilipata gawio la £8,775,160 kwa ajili ya kuboresha filming facilities katika viwanja vyao. Hiki kiwango kilikuwa sawa kwa kila timu, hata kama timu hiyo haikufikisha mechi 10 zilizorushwa live kwenye televisheni. Kwa kila timu iliyozidi mechi 10 live, imelipwa £747,176. Katika category hii Man Utd ndiyo imepata fedha nyingi Zaidi kwakuwa na mechi nyingi zilizorushwa live kwenye tv huko uingereza (mechi 27) na hii ndio sababu ya Man Utd kuizidi arsenal kwa mapato, ambapo ni mechi 25 za arsenal zilizorushwa live.
Finally kila timu ilipata £ 1,244,896 kama merit money, kulingana na nafac iliyomaliza kwenye ligi, ambapo Chelsea ndiyo iliyopata kiasi kikubwa kwa kumaliza wa kwanza.
Changamoto: Hapa bongo, azam ndio walipata haki ya kurusha broadcast za mechi mbalimbali za ligi. Je mgawanyo wa mapato kwa timu umewekwa wazi?