Premier league watoa taarifa ya mgawanyo wa mapato kwa timu msimu wa 2014/2015

Premier league watoa taarifa ya mgawanyo wa mapato kwa timu msimu wa 2014/2015

J. Mushuku

Member
Joined
Jun 1, 2015
Posts
17
Reaction score
4
Bodi ya premier league ya UK imetoa taarifa juu ya mgawanyo wa mapato kwa timu 20 zilishoshiriki ligi hiyo kwa msimu wa 2014/2015. Jumla ya £1.6 bn ziligawanywa kwa timu hizo ambapo Chelsea ndiyo ilipata pesa nyingi zaidi
Katika mgawanyo huo Chelsea ndiyo iliyoongoza kwa kupata £98,999,554 ikijumuisha mapato ya televisheni, merit money (kulingana na nafasi ya kwenye msimamo wa ligi) na malipo mengine mbalimbali. Timu ya QPR ambayo ilimaliza katika nafasi ya 20 ndiyo iliyopata kiasi kidogo ambacho ni £64,886,028.
Timu ya Man city ilikuwa ya pili (£98,501,832) ikifuatiwa na Man Utd (£96,759,212). Nafasi ya nne ilichukuliwa na arsenal ambayo ilivuna £96,509,758 pamoja na kwamba ilimaliza katika ligi katika nafasi ya tatu juu ya Man Utd ambayo ilimaliza nafasi ya nne.
Katika mgawanyo huo, kila timu ilipata mgawo sawa wa television money, regardless ya mechi ngapi za timu husika zilikuwa broadcasted. Kila timu ilipata £21,968,793 kutokana na domestic broadcasts, na £27,757,371 kutokana na overseas broadcasts.
Pia kila timu ilipata gawio la £4,392,630 kutokana na sponsors wa epl, kama vile Barclays, Samsung etc.
Vilevile kila timu ilipata gawio la £8,775,160 kwa ajili ya kuboresha filming facilities katika viwanja vyao. Hiki kiwango kilikuwa sawa kwa kila timu, hata kama timu hiyo haikufikisha mechi 10 zilizorushwa live kwenye televisheni. Kwa kila timu iliyozidi mechi 10 live, imelipwa £747,176. Katika category hii Man Utd ndiyo imepata fedha nyingi Zaidi kwakuwa na mechi nyingi zilizorushwa live kwenye tv huko uingereza (mechi 27) na hii ndio sababu ya Man Utd kuizidi arsenal kwa mapato, ambapo ni mechi 25 za arsenal zilizorushwa live.
Finally kila timu ilipata £ 1,244,896 kama ‘merit money’, kulingana na nafac iliyomaliza kwenye ligi, ambapo Chelsea ndiyo iliyopata kiasi kikubwa kwa kumaliza wa kwanza.

Changamoto: Hapa bongo, azam ndio walipata haki ya kurusha broadcast za mechi mbalimbali za ligi. Je mgawanyo wa mapato kwa timu umewekwa wazi?
 
Attachments

  • epl prize money.png
    epl prize money.png
    38.5 KB · Views: 563
siyo hapa kwetu yanga na simba wanapewa mgawo wa voda sawa na stand utd
 
siyo hapa kwetu yanga na simba wanapewa mgawo wa voda sawa na stand utd

Hahahahaa, sijui lini tutawakaribia hawa jamaa hata robo tu!
Labda kizazi chetu hiki kitakua hakipo tena.
 
Inasisimua kiukweli km Qpr kashuka daraja kapata fedha ambazo ni sawa na mara ishirin kwa bingwa wa Tz.
Jamal malinzi alione hili km tatizo,sio kuwaza kubadilisha rangi za jez tu
 
Hahahahaa, sijui lini tutawakaribia hawa jamaa hata robo tu!
Labda kizazi chetu hiki kitakua hakipo tena.

Wenzenu wana ushirikiano ktk kudai haki zao nifah, halafu viongozi wao wa soka ni professionals, sasa huku kwetu viongozi wengi hasa wa mtaa wa pili mbumbumbu balaa. Yanga si walijaribu kupushi ili mgawo uwe fair lakini wa mtaa la pili kwa umbumbumbu wao wakavuruga move ya Yanga
 
Uandishi wako umeandika kiushabiki na lengo halikua kufikisha ujumbe wa huo mgao bali ni kuonyesha Ushindani kati ya Arsenal na Man U

Na iko wazi ww ni mshabiki wa MAN U
 
Uandishi wako umeandika kiushabiki na lengo halikua kufikisha ujumbe wa huo mgao bali ni kuonyesha Ushindani kati ya Arsenal na Man U

Na iko wazi ww ni mshabiki wa MAN U
Hapana mkuu, umehisi vibaya tu. Nimeelezea kuhusu arsenal na man u, kwa sababu kwa namna mgawanyo ulivyokuwa arsenal alitakiwa kuapa zaidi ya man u. Lakini sio maneno yangu mkuu, hii habari nimeitoa kwenye website ya mirror...for reference jaribu kuchek Premier League prize money: QPR earn £2m per point, Man United finish below Arsenal but earn more - Mirror Online
 
Wenzenu wana ushirikiano ktk kudai haki zao nifah, halafu viongozi wao wa soka ni professionals, sasa huku kwetu viongozi wengi hasa wa mtaa wa pili mbumbumbu balaa. Yanga si walijaribu kupushi ili mgawo uwe fair lakini wa mtaa la pili kwa umbumbumbu wao wakavuruga move ya Yanga

harafu majuzi juzi wakaanza kulalamika kuwa hawapati mapato makubwa kutokana na mpira kuoneshwa LIVE! Vilaza sana hivi.
 
harafu majuzi juzi wakaanza kulalamika kuwa hawapati mapato makubwa kutokana na mpira kuoneshwa LIVE! Vilaza sana hivi.

Wanatia hasira sana yaani
 
Back
Top Bottom