John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Vigogo wa Afrika, Al Ahly wamepoteza mchezo wa nusu fainali ya Klabu Bingwa Dunia kwa kufungwa mabao 2-0 na Palmeiras ya Brazil, usiku wa kuamkia leo.
Kwa maana hiyo AL Ahly sasa wanasubiri kucheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Al Hilal ya Saudi Arabia au Chelsea ya England ambazo zitacheza leo katika nusu fainali nyingine ya michuano hiyo.
Katika mchezo huo waliopoteza Al Ahly, winga wao, LUIS MIQUISSONE alikuwa benchi na hakutumika.
Kutotumika kwa staa huyo kumetokana na kutokuwa na mwendelezo mzuri uwanjani tangu amesajiliwa na timu hiyo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Simba na inaelezwa kuwa hana furaha kwa kuwa hana uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza.
Presha imezidi kuwa kubwa kwa MIQUISSONE kutoka kwa wachambuzi, mashabiki na wadau wa klabu yake hiyo wakishutumu kuwa alisajiliwa kwa dau kubwa lakini hajaonyesha kile ambacho kilitegemewa.
Mwenzake, Clatous Chama ambaye awaliodoka Pamoja lakini wakienda timu tofauti, amerejea Simba na ameshaanza kuitumikia timu hiyo ambapo naye hakuwa na wakati mzuri uwanjani alipokuwa amesajiliwa na RS Berkane ya Morocco.
Tayari maoni ya mashabiki hawa wa Tanzania wanaamini kuwa ni bora arejee Simba kwani akiendelea kubaki huko atanenepa kwa ajili ya kukaa benchi.