Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
B
Baba yangu mzazi alioa mtu na mdogo wake toka nitoke.
ahahahahahahaaaaaaa_mimi mzima sana bhana,...ukienda Yaeda juu salimia Preta na Valleynakusubiri wewe maana inakwenda kizazi hadi cha 4 hahahahaha mzima lakini
ahahahahahahaaaaaaa_mimi mzima sana bhana,...ukienda Yaeda juu salimia Preta na Valley
Yeah,...nilienda ukweni kwahiyo sikuwa na ka-muda sana hapo mjini bhana.salam zimefika nasikia ulipita juzi kati hujatafuta wadau
Kwa raha zake, wanasema kwenye udhia penyeza rupia.
Nina mashaka na jina la mke wa kwanza wa Mobutu ,linafanana kabisa na jina la mke wa aliyekuwa mfalme wa Ufaransa Francis wa pili aliyehudumu wakati wa Reconaicence!!!
Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Duuu miaka 36 watoto 14!.... Jamaa alikuwa hatariMke wa kwanza Anmarie alikufariki akiwa na umri wa mika 36 na alimzalia mzee watoto 14.
Kwa waganda ni kitu ya kawaida hiyo.Do na familia ya mama yako walikubali kabisa.
Kila siku alimuona mpyaInaelekea alimpenda sana, hakua anacheza nae mbali.
Da! Ww Wa ajabu Sana kwani hujui maana ya historiaTupe funzo kwa hii massage, acha ujanja janja
Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga alikuwa kiongozi wa kijeshi dikteta huko Zaire. Mke wake wa kwanza Marie-Antoinette Mobutu, alifariki kwa ugonjwa wa moyo mwaka 22 October 1977 Genolier, Switzerland akiwa na umri wa miaka 36.![]()
1 May 1980, alimuoa Bobi Ladawa pamoja na pacha mwenzake Kosia, Bobi na Kosia ni identical twins na mzee aliamua kuoa wote wawili.
![]()
![]()
Bobi Ladawa was Mobutu Sese Seko’s wife. She shared her marriage with her twin sister Kosia. Bobi gave birth to two sons and two daughters while Kosia had three daughters.
Mobutu alitoka kabila la Ngbandi na alizaliwa Lisala Congo, mama yake Mobutu Marie Madeleine Yemo, alikua mhudumu wa hoteli aliekimbia kijijini kwao Lisala kwa vitisho vya chifu wa kijiji. Alikutana na baba yake Mobutu Alberic Gvemani ambae alikua mpishi wa jaji wa Kibelgiji. Jina la Mobutu alipewa na mjomba wake, baba yake Mobutu alifariki akimwacha na umri wa miaka nane. Mke wa jaji alihuzunishwa sana na kifo hicho na alijenga mapenzi makubwa kwa kijana Mobutu, alianza kumfundisha kuongea, kusoma na kuandika Kifaransa hatimae Mobutu alikuwa na uwezo mzuri sana wa lugha hiyo.
Yemo aliishi kwa kutegemea msaada wa ndugu na jamaa hali iliyomlazimu kuhama kila mara ili kukidhi mahitaji ya watoto wanne alioachiwa.
Elimu ya kwanza ya Mobutu ilikua Leopoldville, lakini mama yake alimhamishia kwa mjomba Coguilhaville, ambako alijiunga na shule ya Christian Brothers School, hii ilikua shule ya boda chini ya kanisa katoliki. Kutokana na umbo lake alikua maarufu katika michezo, alikua na uwezo mzuri kimasomo pia. Pamoja na haya alikua mhariri wa gazeti la darasa.
Mobutu pia alijulikana kwa kuiga kwa kubeza, wanafunzi wenzake wanakumbuka alivyokua anambeza padre wa Kibelgiji ambae lugha yake ya kwanza ilikuwa Kiholanzi alipoongea Kifaransa kwa makosa. 1949 Mobutu alitoroka shule kwenda Leopoldville kukutana na girlfriend. Mapadre waligundua hilo, walimkamata wiki chache baadae. Mwaka wa shule ulipokwisha Mobutu alipewa adhabu ya kutumikia jeshi kwa kosa la kutoroka shule hii ilikuwa adhabu wa wanafunzi watukutu.
Maisha ya Jeshini.
Mobutu alikutana na nidhamu katika maisha ya jeshini, pamoja na mfano wa baba alivyokuwa Sagent Joseph Bobozo kwake. Mobutu alifanya yote aliyotakiwa kufanya kwa nidhamu pia alianza kuazima magezeti kutoka kwa maofisa wa Kibelgiji na vitabu kila alikoweza na alipenda kusoma kila alipopata nafasi. Katika vitu alivyopenda kusoma ni mada za raisi wa Ufaransa waka huo Raisi Charles de Gaulle, Wazieri Mkuu wa Uingereza Winston Churchil na mwana philosopha Muitaliano Niccolo Machiavelli. Baada ya kumaliza na kufaulu masomo yake ya uhasibu, alianza kufanya kazi kama mwandishi wa habari. Bado alikuwa na hasira na mapadre wa shule waliompa adhabu ya kwenda jeshini, alimaua hataoa kanisani. Mchango wake katika harusi ulikua sanduku la bia, hii ndio mshahara wake ulichomudu.
![]()
Akiwa askari, Mobutu aliandika kwa kutumia jina bandia (kama ID za JF) mambo yanayoendelea katika siasa katika gazeti jipya lilianzishwa na wakoloni wa Kibelgiji Actulites Africaines. Mnamo mwaka 1965, aliacha jeshi na kuwa mwandishi wa habari, akiliandikia gazeti la Leopoldiville daily L'Avenier. Miaka miwili baadae alikwenda Ubelgiji kuchukua habari juu ya 1958 World Exposition, alibakia huko kupata mafunzo ya uandishi wa habari. Muda huu Mobutu alishakutana na vijana wengi wa Kikongo wasomi ambao walipinga utawala wa kikoloni. Alianza urafiki na Patrice Lumumba na alijiunga na chama cha Lumumba cha Mouvement National Congolais (MNC). Mobutu hatimae alikua msaidizi maalum wa Lumumba ingawa watu walishaanza minong'no kuwa Mobutu anafanya kazi na shirika la ujasusi la Ubelgiji.
Kipindi cha mwaka 1960 mazungumzo mjini Brussels juu ya uhuru wa Congo yaliendelea, ubalozi wa Marekani ulihodhi mazungumzo ambayo yaliazimia kupata picha kamili ya uwakilishi wa Congo. Wafanyakazi kila mmoja walikabidhiwa majina ya wageni wa kuwapokea na kuongea nao, balozi aligundua jina moja lina jirudia, lakini hakuwa kwenye list kwakua hakua mmoja wa wageni, alikuwa katibu wa Lumumba. Lakini kila mtu alikubali kuwa mtu huyu alikuwa na akili sana, bado kijana lakini atafika mbali.
Mvutano wa Congo.
Kufuatia ahadi ya uhuru hapo tarehe 30 June, 1960, serikali ya mseto iliundwa, iliongozwa na Waziri Mkuu Patrice Lumumba na Raisi Joseph Kasa-Vubu. Taifa jipya haraka lilianza kuona matatizo wakati jeshi lilipoanza kukaidi maofisa wa jeshi wa Kibelgiji. Lumumba alimpa cheo Mobutu kama Katibu Mkuu Kiongozi wa Jeshi la Wananchi wa Congo na Victor Lundula alikua Mkuu wa Majeshi. Katika nafasi hiyo Mobutu alitembea nchi nzima kuhimiza wanajeshi warudi kambini. Jitihada zilifanywa na serikali ya Ubelgiji kulinda mashimo ya madini ya kusini mwa Congo walileta jeshi la Umoja wa Mataifa.
Akiwa na wasiwasi kuhusu uwepo wa majeshi ya Umoja wa Mataifa si kwa kutuliza amani bali ni kwa lengo la kuligawa taifa, Lumumba aliwaendea Umoja wa Soviet kwa msaada, alipewa msaada mkubwa wa silaha na askari wa Kisoviet kama 1,000 kwa msaada wa kiufundi kwa wiki sita. Serikali ya Marekani iliona jitihada za Umoja wa Soviet ni njia ya kueneza ujamaa Afrika ya kati. Kasa-Vubu alihamasishwa na Wamarekani na Wabelgiji kuanzisha mpango wa kuchukua madaraka kijeshi na kumuondoa Lumumba. Lumumba alipogundua hilo haraka alimtoa Kasa-Vumba madarakani. Wote wawili Lumumba na Kasa-Vubu walimpa maelekezo Mobutu ya kumweka ndani mwenzake. Akiwa Katibu Mkuu wa Majeshi Mobutu alikuwa katikati ya msukumo kutoka sehemu mbali mbali. Balozi za Magharibi ambazo zililipa mishahara ya askari, pia Kasa-Vuba na wanajeshi wa chini hawakupenda uwepo wa majeshi ya Umoja wa Soviet.
Mobutu alimlaumu Lumumba kwa kutafuta huruma ya Umoja wa Soviet sasa wamejenga mgongano na Wamarekani, Lumumba aliamua kwenda Staneyville, ambako alipanga serikali yake. Umoja wa Soviet tena walimpatika msaada wa silaha na aliweza kupigania nafasi yake. Baadae mwaka 1960, Lumumba alikamatwa na kupelekwa Katanga. Motubu bado alimuona Lumumba ni tishio kwahiyo aliamrisha akamatwe na apigwe hadharani hiyo ilikua 17 January, 1961. Baada ya hapo alitoweka kwenye macho ya watu na hakusikika tena. Baadae ilifahamika aliuwawa siku ile ile na majeshi maalum ya Moise Tshombe baada ya kuigeuka serikali ya Mobutu na mabishano na Wabelgiji. Wamarekani walimuona Lumumba ni kiongozi hatari na masilahi yao yangekuwa hatarini kama angebaki madarakani.
23 January 1961 Kasa-Vubu alimpandisha cheo Mobutu kuwa Mkuu wa Majeshi, De Witte anasema hii ilikua ni kwa sababu za kisiasa zaidi kwa nia ya kulipa jeshi nguvu kubwa zaidi, alikua mtu ambae raisi alimwamini zaidi pia umuhimu wake katika jeshi.
1964 Pierre Mulele aliongoza wafuasi wa vyama vingine katika mapinduzi. Kwa haraka walishikilia 2/3 ya eneo la Congo lakini jeshi la Congo likiongozwa na Mobutu waliweza kuchukua eneo lililotekwa lote ilipofika 1965.
Jaribio la pili la kupindua serikali.
Waziri Mkuu Moise Tshombe ambae ndiye aliyekuwa kiongozi wa Congolese National convetnion alishinda uchaguzi kwa kura nyingi katika uchaguzi wa March 1965, lakini Kasa-Vubu alimtunuku kiongozi wa upinzani Evariste Kimba kuwa waziri mkuu, hata hivyo Bunge lilipinga uteuzi huo. Kufikia hapo serikali ilikua inayumba na Mobutu alichukua nafasi hiyo kufanya mapinduzi ya kijeshi 25 November 1965. Hii ni mara tu yakufikisha umri wa miaka 35.
Chini ya utawala wa dharura Mobutu alifikiri atapata nguvu kamili ya uongozi ndani ya miaka mitano. Hotuba yake ya kwanza baada ya kuchukua madaraka, Mobutu aliuambia umati wa watu mjini Leopoldville katika uwanja wa mkuu kuwa tangu wanasiasa waharibu nchi basi kwa miaka mitano hatutakuwa na chama cha siasa wala shughuli za kisiasa. Nguvu za bunge zilibaki kuwa ni mhuri tu kabla ya kufutwa kabisa lakini baadae zilirudishwa. Idadi ya majimbo ilipunguzwa na ushawishi wa majimbo ulidhoofishwa. Hii ilileta utawala wa amri kutoka kwa rais.
Kwakifupi serikali ya Mobutu ilikua madhubuti na pia siasa haikutakiwa kabisa. Neno siasa lilikua ni sawa na uhaini na mwanasiasa alimaanishwa ni mtu mpenda rushwa, tapeli na mhaini. Hata hivyo mnamo 1966 kulianza msukumo wa vikundi vya vijana vya kujitolea vilianza mikakati ya kumuondoa Mobutu ambae alijiita "Shujaa wa Pili wa Nchi"baada ya Lumumba. Kwa nguvu zote alijipa cheo cha mtu aliefuata nyayo za Lumumba na moja ya mambo aliyoazimia ni kuwa na serikali halali ndani ya Congo.
![]()
Mwaka 1967 kilizaliwa chama cha Popular Movement of the Revolution (MPR) ambacho mpaka 1990 kilikua chama pekee cha kisiasa kilichoruhusiwa. Kwa lugha nyingine kilikua chama kilichoruhusiwa kisheria kuendesha shughuli za kisiasa nchi nzima katika imani moja. Serikali ilikuwa ni njia ya kuenzeza chama. Kila raia alikua mwanachma wa MPR tangia kuzaliwa. Policy kubwa ya chama iliyojulikana kama N'Sele, ilikua na lengo la kuleta mapinduzi, uongozi wa vitendo ndani ya chama, hali hii ilionekana kama ni mchanyiko wa siasa za ujamaa na ubepari. Usome mashuhuri wa MPR ulikua "Hatuko mwengo wa Kulia wala wa Kushoto". na wenyewe waliongezea "Hatuko hata katikati" miaka ya baadae. Chama cha MPR kilifanya uchaguzi kila baada ya miaka saba na mshindi kuwa raisi wa Jamhuri. Kila mwaka Mobutu alikua anapendekezwa kama mgombea pekee na jina lilipitishwa na uongozi mkuu wa chama ambao walikua na orodha ya wagombea nafasi za uongozi ndani ya chama.
Bunge lilirudi kila baada ya miaka mitano kama chombo cha kutunga sheria na kilimpa rais wa chama nguvu zote za kuendesha serikali.
Mwaka huo huo vyama vyote vya kutetea haki za wafanyakazi viliunganishwa na kua chama kimoja National Union of Zairian Workers, chama hiki kiliendeshwa moja kwa moja kwa amri kutoka serikalini. Kwa matakwa ya Mobutu mwenyewe chama hiki kilikua chombo cha kuhakikisha agenda za serikali zinatekelezwa makazini iwe kwa sheria, nguvu au kwa ubishi. Vyama vingine vya kutetea haki za wafanyakazi havikuruhusiwa mpaka 1991.
Akikabiliwa na upinzani mwanzoni mwa utawala, Mobutu aliweza kuwanyamazisha aliweza kuwafanya wapinzani wake wengi wamkubali kwa kutumia mbinu mbalimbali na mbinu hizo zikishindwa, nguvu ilitumika. Mwaka 1966 mawaziri wanne waliwekwa ndani kwa kilichoaminika kuwa jaribio la kupindua serikali. Walishiatakiwa katika mahakama ya jeshi na walinyongwa hadharani, watu 50,000 wakishuhudia. Jeshi la Katanga liliteketezwa na mipango mingine iliyopangwa na jeshi la wazungu mwaka 1967 haikufanikiwa. Mwaka 1970 karibia kila aliekua tishio katika utawala wake alimalizwa and sheria za chama na serikali zilifikishwa karibu katika kila kona ya nchi. Mwaka huu unaweza kuelezewa kuwa mwaka uliofikisha kileleni utawala wa Mobutu wa kisheria na nguvu. Mfalme Baudouin wa Ubelgiji alifanya ziara ya kiserikali iliyokuwa na mafanikio makubwa na mwaka huo huo uchaguzi wa bunge na rais ulifanyika. Chama cha MPR pekee ndio kilishiriki uchaguzi ingawa kwa kisheria ilitakiwa vyama viwili vya kisiasa vishiriki uchaguzi. Kulingana na matokeo ya uchaguzi huo kwa mashaka MPR kilipata ushindi wa asilimia 98.33% ya wapiga kura wote. Katika uchaguzi wa raisi Mobutu alikua mgombea pekee, wapiga kura walipewa karatasi mbili wachague kati ya kijani kukubali au nyekundu kukataa. Mobutu alishinda kwa kuta 10.131.699 mpaka 157.
![]()
Jinsi Mobutu alivyozidi kupata nguvu ndiyo alivyoimarisha jeshi kwa nia moja kubwa ya kumlinda yeye. Kulikuwa na Kikosi Maalum cha Raisi, Jeshi la Usalama, Jeshi Maalum la Upelelezi na Vitendo.
Mwendelezo wa Kampeni.
Kulianza kwa kile kilichoaminiwa mwendelezo wa jadi ya Mwafrika au uasilia. Mobutu alianza kubadilisha majina ya miji ya Congo kuanzia 1 June, 1966; Leopoldville kuwa Kinshasa, Elisabethville kuwa Lubumbashi na Stanleyville kuwa Kisangani. October 1971 alibadili jina la nchi kuwa Jamhuri ya Zaire. Watu waliamrishwa kuacha majina yao ya ki Kristu na majina yaliyotambuliwa yalikuwa ni ya jadi tu. Viongozi wa dini walipewa onyo kali kuwa atakaembatiza mtoto ki Zaire kwa jina la Kikristu atafungwa jela miaka mitano. Suti za Magharibi na nguo nyingine zilipigwa marufuku na wanaume walilazimishwa kuvaa style ya Mao iliyokuwa koti fupi mpaka juu kidogo ya magoti lenye mikono mifupi lilojulikana kama abacost kifupi cha (a bas le costume down with suit).
1972 Mobutu alibadilisha majina yake wenyewe na kujiita Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu Wa Za Banga ("Shujaa wa mashujaa mshindi ambae kwa ujasiri na kutokukuba kushindwa atashinda na kushinda na kuacha moto nyuma yake"). Huu ndio wakati Mobutu alikuwa na style yake ya mavazi ambayo ni abacost, miwani yenye frame nzito, fimbo ya kutembelea na kofia yenye ngozi ya chui.
Utawala wa mtu mmoja.
Mapema katika utawala wake Mobutu alijipatia nguvu kwa kupindua serikali, kunyonga wapinzani wake hadharani, kutesa na kuua wapinzani na utawala wa vitisho. Kwa mfano wengi walinyongwa mbele ya umati wa watu akiwemo aliekuwa Waziri Mkuu Evariste Kimba, ambae pamoja na mawaziri wengine watatu Jerome Anany (Waziri wa Ulinzi), Emmanuel Bamba (Waziri wa Fedha) na Alexandre Mahamba (Waziri wa Nishati na Madini) walihukumiwa May, 1966 na walipelekwa kunyongwa 30, May mbele ya watu 50,000. Wanaume hao waliuliwa kwa kuwa na mawasiliano na Colonel Alphonse Bangala na Meja Pierre Efomi, kwa mipango ya kupindua serikali. Mobutu alielezea kitendo hicho kama "Mmoja inabidi mmoja atoe adhabu ili iwe mfano kuweka utawala wenye nidhamu. Kamanda akichukua hatua ni mwisho wa maamuzi".
1968 Pierre Mulele, aliekuwa Waziri wa Elimu wa Lumumba na kiongozi wa upinzani waka wa Upinzani wa Simba 1964, alishawishiwa kurudi kutoka ukimbizini Brazzaville kwa mategemeo kuwa atakua na kinga, lakini aliteswa na kuuwawa na askari wa Mobutu. Wakati Mulele alikua hai, macho yake yalitolewa na sehemu za siri kukatwa na miguu ilikatwa mmoja mmoja. Mobutu baadae alihama kutoka kutesa na kuuwa na akabadili mbinu, na kuanza kununua maadui wake wa siasa. Alitumia usemi "Weka marafiki zako karibu lakini maadui waweke karibu zaidi, akimaanisha mbinu ya kubadili mioyo ya maadui zake kwa kutumia hongo.
Mbinu Mobutu aliyoipendelea sana ni kucheza "mziki wa viti", kubadilisha mawaziri wake katika serikali na kuhakikisha kwamba hakuna atakae kuwa hatari kwa serikali yake. Mbinu nyingine ilikuwa kuwaweka ndani na kuwatesa wakaidi wa serikali, baadae aliwatoa kwa msamaha na kuwapandisha cheo. Mfano mzuri wa hili ni tukio ni Jean Nguza Karl-u-Bond, ambae alifukuzwa kama waziri wa mambo ya nchi za nje mwaka 1977, alihukumiwa kufa, na aliteswa. Baadae Mobutu alibadilsha hukumu yake kuwa kifungo cha maisha, alitolewa mwaka mmoja baadae na baadae alipewa uwaziri mkuu. Nguza alikimbia nchi mwaka 1981 na alirudi 1985, kwanza alipewa cheo cha balozi wa Zaire nchini Marekani na waziri wa mambo ya nje.
Faida alizojipatia binafsi katika utawala wake.
Mobutu alijichukulia fedha za nchi kwa mabillioni ya dola za ki Marekani. Inasemekana aliiba kati ya US$ billioni 4-5 lakini wengine wanasema inafika US$ billioni 15. Mkwe wa Mobutu Pierre Janssen aliemuoa binti yake Yaki Mobutu anasema, Mobutu hakujali gharama ya zawadi aliyotoa kwa marafiki na watu wake wa karibu. Wakati wa ndoa yao Janssen anasema bendi tatu zilitumbuiza na keki ya harusi pamoja na mapambo viligharimu US$ 65,000. Bibi harusi Yaki alivaa gauni la US70,000 na mapambo mengine kama mkufu na hereni yaligharimu US$ 3 million. Janssen anasema siku ya kawaida ya Mobutu iliambatana na vyakula na mivivyo ya gharama iliyoletwa kutoka Ufaransa na nchi nyingine.
![]()
Gbadolite ni moja ya majumba ya Mobutu linavyoonekana kutoka angani. Ujenzi wake uligharimu US$ million 100
![]()
Moja ya sherehe za kuapishwa kwa rais Mobutu ndani ya Gbadolite.
![]()
Mke wa kwanza wa Mobutu ambae alimpenda sana Marie Antoinette Mobutu. Chanzo cha uhakika kimenieleza mauti ya huyu mama yalisababishwa na kipigo alichokipata kutoka wa mume wake akiwa mja mzito. Pamoja na kuwa aliwahishwa hospitali nchini Switzerland lakini aliaga dunia, hiyo ilikuwa mwaka 1977.
Gbadolite ni mji katika nchi ya Congo na sio jumba au palace kama ulivyoandika,ni huko Mobutu alijenga uwanja wa ndege mkubwa kwa wakati huo wa kuweza kutua madege makubwa ilihali haukua mji unaostahili kuwa na kiwanja kikubwa hivyo,bali alifanya hivyo kwakua ni nyumbani kwao.Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga alikuwa kiongozi wa kijeshi dikteta huko Zaire. Mke wake wa kwanza Marie-Antoinette Mobutu, alifariki kwa ugonjwa wa moyo mwaka 22 October 1977 Genolier, Switzerland akiwa na umri wa miaka 36.![]()