Point. Ruto anataka kurudisha pesa aliyowalipa wale jamaa wa IT wa Bulgaria kuchezea mitambo ya IEBC hataki mambo ya nusu-mkate watajua Siri zake
Kila upande una watu wa kurudishia pesa, kama unaelewa siasa unapaswa ujue wagombea wakuu wote huwa na wafadhili nyuma yao ambao huwakopesha kwamba ukishinda aidha utalipa fadhila kwa dili za kiserikali au unipe hela yangu na riba juu.
Hilo lipo kwa wote, iwe wa upinzani au serikalini, sasa utata huja pale umeshindwa kwenye uchaguzi na uliwaaminisha wafadhili lazima utashinda, hivyo kwa kifupi inapaswa aidha urejeshe hela ya watu au uingie kwenye makubaliano kimya kimya na aliyechukua uongozi, unampa masharti ili niache kukusumbua naomba uwape hawa mikataba na dili za kiserikali maana wananipumulia.
Hivyo mara nyingi unaposikia viongozi wamekutana kuridhiana, nyuma ya pazia hayo ndio huwa wanayajadili.
Ruto anayafahamu sema anashupaza shingo tu, labda na yeye ana wengi sana wa kuwalipa fadhila kiasi kwamba hawezi kubeba wa Raila kwa sasa, labda amemuambia nipe miaka miwili niwalipe wa kwangu kabla kuchukua madeni yako, ila yamkini Raila naye anapumuliwa sana na wa kwake kiasi kwamba anaona bora uwachukue mapema la sivyo nitaliamsha hutatawala.
Ninaamini hiki ndicho Uhuru na Raila waliwekana sawa kipindi chao na wakagawana kimya kimya na hali ikatulia.
Unapo waona viongozi wa upinzani ikulu ujue nyuma ya pazia kuna mengi huwa hayawekwi bayana kwetu sisi.
Kuna mafia huwa wanafadhili viongozi, unaskia mtu katokea sijui Urusi au wapi huko mataifa ya kimafia mafia, kaja na mikoba yenye mabilioni kwa yeyote anayetaka hela na yupo radhi kulipa riba.