Mkuu
Ndalilo,
Nilisahau jambo moja la msingi kabisa!!
Umedai, hata nikushawishi vipi KATU, huwezi kukubali kwamba JK alikuwa analinda maliasili za taifa kwa maslahi ya taifa! Nami nikakujibu kwamba HAKUNA popote niliposema JK alikuwa analinda maliasili zetu...
Lakini pamoja na hayo, ukataja marais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania ni Nyerere, Mkapa, na Magufuli. Aidha, marais wabovu kabisa kuwahi kutokea ni Mwinyi, Kikwete, na bila shaka kwenye orodha hii utamwigiza Samia!!
Huyo JPM tumwache manake tumemjadili sana!!! Hata hivyo, hebu nijuze jambo moja! Hivi huu ubora umeipima kwa kutumia vigezo gani? Unaweza akueleza kinaga ubaga?!
Nauliza hivyo coz', last time I checked, kashfa nyingi za kutisha nchi hii zimetokea wakati wa Mkapa...
1. Kagoda Scandal... imetokea wakati wa Mkapa
2. Deep Green... imetokea wakati wa Mkapa
3. Meremeta scandal... imetokea wakati wa Mkapa!
4. EPA Scandal... imetokea wakati wa Mkapa!
5. Huu mjadala umepamba moto kwa sababu ya Tony Blair aliyehusika kutuuzia radar kwa bei ya kutisha!! Lakini tunajisahaulisha kwamba, hiyo radar na yenyewe (Radar Scandal) iltokea wakati wa Mkapa
6. Msingi wa mikataba mibovu ya madini, umetokea wakati wa Mkapa!
7. Uuzaji holela wa mashirika ya umma (ule haukuwa ubinafsishaji), na wenyewe umetokea wakati wa Mkapa!
8. IPTL ingawaje ilianzia wakati wa Mwinyi, lakini aliyekuja kuuvuruga mkataba wa IPTL hadi kulazimika kuwapa miaka 20, tena alifanya hivyo kabla mkataba wa awali hujaisha... nalo ni wakati wa Mkapa!
9. Roho ya bandari ni Container Terminal. Aliyebinafsisha Container Terminal kwa TICTS, hapo pia ni Mkapa! Na kama ambavyo alifanya kwa IPTL... kwa mara ya kwanza aliwapa mkataba wa miaka 10, lakini alipoona anakaribia kuondoka madarani... akawaongezea miaka mingine 10! And FYI, TICTS wali-break even in less than 3 years!
Again, ulipanga ubora wako kwa kutumia vigezo gani?
Halafu ulihoji ikiwa hivi sasa ndo rasmi namtetea Kikwete!!! Man, mbona unachukulia haya mambo too personal?! Nimtetee KIkwete ili iweje?!
Watu mnasema GAS YOTE IMEUZWA, kwa sababu ndivyo Magufuli alivyowaambia... mimi nawaambia habari za kugesi kuuzwa hazina ukweli wowote!!
Mnasema sheria yenyewe ya gas ni mbovu kweli kweli ndo maana JPM kaibadilisha ... mimi nikawataka muweke hiyo sheria mbovu au hiyo sheria mpya ya JPM, mara zote naongea with confidence kwa sababu najua hata sheria zenyewe hamjawahi hata hkuzitupia macho let alone kuzisoma!! Pamoja na hayo, sheria hamziweki!
Sasa kama huko ni kumtetea na/au kumsafisha JK, basi sawa, ndo namsafisha rasmi lakini busara iendelee kujikita kwenye hoja!!
Na ningekuwa hapa kutetea watu, uliposema suala la Riziwani kukamatwa na dawa za kulevya, basi ningemtetea kwa kukuwekea link kabisa ya wapi habari hizo zilianzia siku ya September 07,2012. Na kwavile aliyeanzisha alikuwa ni mwana-JF maarufu sana kipindi kile, habari zikatoka kwenye source, zihamia JF!
Pamoja na kujua source ya habari yenyewe lakini nimeamua kupuuza kwa sababu sipo hapa kutetea yeyote bali nipo hapa kueleza mambo yenye maslahi kwa taifa!!Maelezo yangu yamejikita kwenye issues za gas!
Na kwa wanaonifuatilia, mimi ni mfuasi wa masuala ya Uchumi na Uwekezaji, kwahiyo hata hayo mambo ya gesi nimeyajadili sana, tena sana na nitaendelea kuyajadili!!