President Trump has been Impeached after the House of Representatives voted in favour of charging him with abuse of power and obstruction of Congress

President Trump has been Impeached after the House of Representatives voted in favour of charging him with abuse of power and obstruction of Congress

Unahisi kule hua wanapelekwa bila sababu na ndio hua kuna takiwa ushahidi kamili
Brother! Humu ndani watu wanakupinga bure tu Ila upo sahihi! Na kilichotokea jana Dems wamepata aibu sana! Dems wamemzushia Trump mazingaombwe kibao wakiambiwa walete ushahidi wanaleta ushahidi wakupikwa ambao mwisho wa siku wanafeli.

Ndiyo maana jana Trump kawaambia hata kama wakimu' impeach atakuwa ni rais wa kwanza kufanyiwa impeachment pasipo kuwa na crime ya aina yoyote.
Anavyosema hata kama wakimu impich atakua anaonewa ana maana gani ama ndio anatafta huruma za raia[emoji16]

Jamaa anawexa akapita sababu kuna baraza moja anaongoza kwa majority ya wanachama wake

Ila kimsingi jamaa anamakosa hata kama sio yote ila ni MINGI tu Miongoni mwa Aliyohusishwa Nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unahisi kule hua wanapelekwa bila sababu na ndio hua kuna takiwa ushahidi kamiliAnavyosema hata kama wakimu impich atakua anaonewa ana maana gani ama ndio anatafta huruma za raia[emoji16]

Jamaa anawexa akapita sababu kuna baraza moja anaongoza kwa majority ya wanachama wake

Ila kimsingi jamaa anamakosa hata kama sio yote ila ni MINGI tu Miongoni mwa Aliyohusishwa Nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kama yapi?
 
Trump is going NOWHERE, mark my words, hii ni chuki za kibinafsi, nilifuatilia mambo yote, mashahidi wote, na hamna lolote, ngoja muchuano uelekee senate, huko ndipo hii impeachment itakufa na kuzikwa
 
Trump unamjua au unamsikia?, ni Tanzania tuu ndio mtu akiwa rais ndio anajenga kwao!, masikini Nyerere hadi anaacha urais hakujenga kwao akafanya kujengewa na JKT!.

Trump ni tajiri mkubwa, kujenga kwao in nothing, I wish rais Magufuli awe tajiri kama Trump na ndio maana mimi na support maendeleo ya Chato, charity begins at home

P
Si kwa kutumia pesa za serikali tena zisizo na bajeti huo ni ukwapuaji.
 
Hili ni bandiko la Trump, za Mlimani City tukutanie kule, tujifunze kuheshimu mabandiko ya watu kwa kujadili mada iliyo mezani, mada hapa ni bunge la wenzetu linatimiza role yake ya kuisimamia serikali kwa kutaka kumuwajibisha rais, swali hapa jee Bunge letu hili la Ndugai lingeweza?,

mfano mzuri kabisa ni katiba imeruhusu mikutano ya siasa nchi nzima, rais Magufuli kazuia mikutano hiyo kinyume cha katiba, chama makini cha upinzani Chadema kipo bungeni, lenye uwezo wa kulishughulikia hili, kule kwenye bungeni kwenye uwezo, hawashughuliki, Chadema walitaka kulishughulikia kwa kufanya mikutano na maandamano nchi nzima as if uvunjivu wa katiba unashughulikiwa kwa mikutano na maandamano!, juzi hapa siku ya Uhuru, Mwenyekiti Mbowe, anapiga magoti kwa Magufuli kumuomba suluhu ya mazungumzo wakae mezani wazungumze!, haki ni right sio favour, haiombwi na hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa na ikibidi inapiganiwa!. kuhusu hili

Somo hili la Trump ni somo kubwa kwa Bunge letu na wabunge wetu wakiwemo wabunge mahiri na machachari kama Zitto na umachachari wa kwenye twitter lakini mule Bungeni kwenye the right forum yuko kimya!.

Siku nimekutana na Zitto mahali, nilimpa za uso kuhusu hili by telling him to his face
P.
Kwa hiyo kwa kutumia bunge ambalo wapinzani ni minority unategemea muujiza gani utokee wapinzani wa m-empeach Magufuli hebu tueleze hapa maana lawama zingine kwa wapinzani si sahihi hata wakienda mahakamani mahakama ziko mfukoni mwa Magu,huo ndio ukweli watapenyea wapi,Magu aheshimu katiba aliyoapa vyama vya upinzani vipo kwa mujibu wa katiba marekebisho ya 1992 anza na Msukuma mwenzio kwanza.
 
Kwa hiyo kwa kutumia bunge ambalo wapinzani ni minority unategemea muujiza gani utokee wapinzani wa m-empeach Magufuli hebu tueleze hapa maana lawama zingine kwa wapinzani si sahihi hata wakienda mahakamani mahakama ziko mfukoni mwa Magu,huo ndio ukweli watapenyea wapi,Magu aheshimu katiba aliyoapa vyama vya upinzani vipo kwa mujibu wa katiba marekebisho ya 1992 anza na Msukuma mwenzio kwanza.
Mkuu Vonix, impeachment is a process, maadam vyama vingi vipo kwa mujibu wa katiba na sheria, na katiba na sheria imeweka utaratibu wa kushughulikia uvunjifu wa katiba, mtu yoyote au chama chochote makini, kitakacho lalamikia uvunjifu wa katiba, kitu cha kwanza kabla ya kulalamika ni kifuate taratibu, sheria na kanuni, kisiposikilizwa ndipo kilalamike.

Hatua ya kwanza ya jambo lolote lenye utata wa kisheria, ni kwenda mahakamani, sio kushitaki bali kuomba ufafanuzi wa kisheria. Tasisi pekee yenye mamlaka ya kutamka kama katiba imevunjwa au la ni mahakama kuu, Katiba imeruhusu mikutano, Magufuli amezuia mikutano kinyume cha katiba, nani amekwenda kuomba tafsiri ya mahakama?, mahakama ikiishatamka kuwa ni kweli Magufuli amevunja katiba, ndipo mbunge yoyote angeweza ku initiate hiyo process ya kibunge.

Chadema kinajiita chama makini, badala ya kufuata taratibu za kikatiba, kisheria, kikanuni na kiutaratibu ku deal na hili, chenyewe kilitaka kufanya a non stop maandamano na mikutano nchi nzima!, kwanza tuliwaeleza wazi humu kuwa uvunjifu wa katiba, haupingwi kwa maandamano na mikutano ya hadhara

Pili hiyo hoja kuwa mahakama ziko mfukoni kwa Magu, hazina mashiko kwasababu ni Chadema hao hao, huwa wanakimbilia mahakamani kwa mambo madodogo madogo mengine ni ya kijinga kabisa!, lakini mambo makubwa kama uvunjifu wa katiba, unaohitaji umahiri wa sheria, wao ndio wanapinga kwa maandamano na mikutano.

Mimi kama kawaida yangu, sio mwanasiasa, ni mwandishi tuu na kazi yangu siku zote ni kuuliza tuu, kutangaza na kuandika, nilipoalikwa Ikulu, suala hili nililiuliza kwa Magufuli mwenyewe

Siku nimekutana na Zitto, suala hili nilimuuliza Zitto mwenyewe

P
 
Pole sana ndugu yangu; je ulikuwa mtumishi hewa au ulikuwa na vyeti visivyotambulika? Nadhani watumishi hewa ni wale waliokuwa kwenye payroll, lakini hapatikana kwenye roll call. Kama ulikuwa kwenye roll call na bado wakakutema, tafuta mwanasheria mzuri akusaidie kupata haki yako kwani kesi hiyo ni rahisi sana. Ila kama ulikuwa kwenye kazi kwa kutumia cheki kisicho halali kesi yake ni ngumu kidogo, lakini bado ni vizuri kujaribu kuipeleka mbele ya vyombo vya sheria.
Mkuu naomba link ya uzi wako unaofundisha kuhusu muziki
 
Trump is going NOWHERE, mark my words, hii ni chuki za kibinafsi, nilifuatilia mambo yote, mashahidi wote, na hamna lolote, ngoja muchuano uelekee senate, huko ndipo hii impeachment itakufa na kuzikwa
Impeachment huwa haimwondoi rais madarakani; hata Nixon alijiuzulu mwenyewe kwa sababu hakutaka kwenda njia hiyo ingawa bado huenda asingeondolewa madarakani. Maraisi wa Marekani wote waliowahi kuwa impeached walimaliza vipindi vyao ila walikuwa na bahati kuwa hayo yalitokea mwishoni mwa utawala wao. Impeachment ya Congress hulenga kumwadabaisha rais kuwa hayuko juu ya kila kitu. Amini kuwa kipindi cha pili cha Trump iwapo atafanikiwa na Congress ikabaki kwa Democrats, basi atakuwa na adabu ya kufanya nao kazi kama serikali moja. Washauri wake wazuri wameshambia wazi kuwa tatizo lake ni lile la kujimwambafy kuwa mimi ni Rais sitishwi na yeyote. General Kelly alimwambia usifanye hivyo, na sasa hivi atakuwa anakumbuka maneno hayo. Viongozi hutaka kubaki na legacy nzuri, siyo hiyo kuwa jamaa alikuwa chaotic hadi akawa impeached!!.
 
Mkuu naomba link ya uzi wako unaofundisha kuhusu muziki
Noja nikutafutie kwani ninategemea kuaihudimia tena kwa wiki mbili zijazo baada ya krismas, andika chochote pale kusudi baadaye niwe nakutag kwa kila post nitakayoweka baada ha hapo.
 
1. Wakimchmoa itakuwa muujiza! Two third votes kumpinga so rahisi kufikiwa.
2. In any way, mission ya Democtratics imefanikiwa: kupunguza spidi ya Trump mwakani, kutahadharisha raia na mamlaka mbalimbali juu ya tahadhari na hatari ktk uchaguzi ujao.
3. Uchaguzi wa mwakani ni mgumu. Rep. watakuwa wanawaza kwa kina namna ya kumvisha 'the tweet master'
Ndio kwanza wamempa nguvu, Americans are not controlled by the media or celebrities, pitia mitandao mbali mbali soma comments za watu ndio utajua kwamba jamaa wasio mkubali ni hoolywood na democrats, ila raia wanamkubali vibaya mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu naomba link ya uzi wako unaofundisha kuhusu muziki
Sawa ni hii hapa
 
Ndio kwanza wamempa nguvu, Americans are not controlled by the media or celebrities, pitia mitandao mbali mbali soma comments za watu ndio utajua kwamba jamaa wasio mkubali ni hoolywood na democrats, ila raia wanamkubali vibaya mno

Sent using Jamii Forums mobile app

Waamerika wamegawanyika katika makundi matatu ambayo roughly ni kama: 40% Republicans ambao wengi wao ni watu weupe na wa vijijini , 40% democrats ambao ni mchangayiko wa magrupu ya race mbalimbali na wengi wao wako mijini, na 20% Independents ambao wengi wao ni wasomi ambao pia wako mijini. Kwa hiyo hizo websites unazosoma inategema ni za watu wa mlengo gani kati ya hayo magrupu makubwa ya demokrats na Republicans. Independents wengi huwa huwa hawaandiki maoni yao mitandanoni, na vile vile sehemu kubwa ya democrats wenye rangi, yaani weusi, latino na waasia pia huwa hawaandiki maoni yao mitandani. Kwa hiyo iwapo unasoma maoni mengi ya republican siyo kweli kuwa hayo ndiyo maoni ya waamerika wengi.
 
Back
Top Bottom