President Zuma Advises Museveni to Rename Lake Victoria

Nasapoti hoja kwa asilimia mia..si bora tuliite Kalekansungu tu.
 
Napendekeza liitwe LAKE JULIUS KAMBARAGE NYERERE kwa heshima ya Baba wa Taifa.
 
Kwa tuliosoma zamani, hilo ziwa hata kwenye atlas za Kiswahili huitwa Ziwa Nyanza. Na ukijibu hivyo kwenye mtihani unapewa alama kamili.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Napendekeza liitwe LAKE JULIUS KAMBARAGE NYERERE kwa heshima ya Baba wa Taifa.
Khaaaa, hapana kwa kweli, kwani kabla ya kuitwa hilo victoria, wenyeji walikua wanaliitaje???

Nadhani jina la mwanzo ndio lingerudi.
 
...na jina Jacob je, linamhusu? nafikiri angeanza na hilo kwanza.
Halafu jina lake Jacob alipewa na mzungu aliyembatiza. Mbona hajabadili? Bora Joseph alianza yeye kujiita Mobutu ndo akawaambia na wenzake wabadili.
 
Waludishe jina lake la mwanzo.maana zamani lilikua linafahamika kama ziwa nyanza
But wakitaka kulibadili jina waliite ziwa
1bashite
2magufuli
3zuma
 
Rais Zuma ataka Ziwa Victoria libadilishwe jina

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo.

Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo.

Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria.

Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema Ziwa hilo kuendelea kuitwa Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao.

“Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma.

Wachana nae huyo Mzee wa scandali, kwanza M7 anamiliki sehemu ndogo sana ya ziwa hilo na pili mbona kule kwake hajabadilisha jina la Durban au Cape town? Hata Pretoria walijaribu kuibadilisha iitwe Tshwane, limegoma bado global identity imebakia kuwa.Pretoria! Na yeye bado anaitwa Jacob kwa nini?
 
Bora libadilishwe na lile jiwe nalo libadilishwe
 
Ni sawa! Hata sisi tulishalibadilisha jina huku Tanzania. Linaitwa ziwa NYANZA! Yaani Lake NYANZA! Uganda Nao sehemu yao wanaweza lake Matoke!
 
Huyo jamaa sio mzima...hata kwake south ametumia gharama kubwa sna kubadilisha MAJINA ya MITAA..kutoka kwenye majina ya KIZUNGU kuweka ya WATU WEUSI...mfano JACOB MALEY...VANDAR WART..hayo ni mfano wa majina ya KIKABURU..yeye ameweka ya KIZULU..mfano ALBET SISULU..nk..hata AIRPORT ya JOBERG zamani iliitwa JAN SMATS airport.. akaibadili nakuwa OLIVER TAMBO...imesababisha USUMBUFU MKUBWA SN..yeye hana anachokijuwa zaidi ya KUCHEZA NGOMA na WANAWAKE...tu.. basi..kaharibu sana ile INCHI..
 
Back
Top Bottom