President Zuma Advises Museveni to Rename Lake Victoria

President Zuma Advises Museveni to Rename Lake Victoria

hii kitu ilikuwa inaniumiza sana kichwa, na nikiwa primary niliwahi muuliza mwalimu wangu kwanini lisiitwe jina la kwetu badala ya kuitwa victoria, huyu victoria ni nani, kwa kweli alinipa jibu ambalo sikuridhika nalo, sasa viongozi wetu hata 1 hakuwahi kuwa na wazo hili, leo hii zuma kaamua kusema, hata mie naungana nae, wacha tuone, mara asiyepangiwa anaweza akagoma kwai hapangiwi
nyanza waweza liita hivo
 
Naunga mkono hoja,hakuna sababu ya kutumia jina la Malkia wa Uingereza kwenye ziwa kubwa kuliko yote Afrika.
 
Hata jua na mwezi vitabadilishwa majina sasa.
Hebu tuachane na wanasiasa
ambao fikara zao zimefikia ukomo.
 
Nadhani Zuma kwa elimu yake ya Grede 4 anajua ndivyo inavyokuwa kwa maziwa yaliyo shared kati ya nchi - kama alivyoona Malawi ziwa wanaliita Lake Malawi kwao na kwetu ni Lake Nyasa. Sijui Msumbiji wanaliitaje, Nyasa au Malawi?

Msumbiji wanaliita NIASSA
 
🙂 🙂 yeye amebadilisha majina kama cape town, Johannesburg au nyani analiona la mwenzake!?
Hakika mkuu huyu mzee anataka kutuchonganisha tu!
[emoji4] [emoji4]
 
Kwani ziwa lipo tu Uganda? Au Uganda ndo mmiliki wa ziwa? Inamaana nchi za Tanzania na Kenya hazina mamlaka?

Yeye mwenyewe jina "JACOB" ni la kizungu basi nalo alibadilishe
 
Napendekeza liitwe LAKE JULIUS KAMBARAGE NYERERE kwa heshima ya Baba wa Taifa.
"Julius" ni jina la Kizungu vile vile!!
Mimi namshauri aanze kubadilisha jina lake la JACOB kwanza! Akiwa kama MBANTU wa kweli
 
I support Zuma. Lake Nyanza is much better kuliko that Victoria CRAP!
 
Back
Top Bottom