President Zuma Advises Museveni to Rename Lake Victoria

nyanza waweza liita hivo
 
Naunga mkono hoja,hakuna sababu ya kutumia jina la Malkia wa Uingereza kwenye ziwa kubwa kuliko yote Afrika.
 
Hata jua na mwezi vitabadilishwa majina sasa.
Hebu tuachane na wanasiasa
ambao fikara zao zimefikia ukomo.
 
Nadhani Zuma kwa elimu yake ya Grede 4 anajua ndivyo inavyokuwa kwa maziwa yaliyo shared kati ya nchi - kama alivyoona Malawi ziwa wanaliita Lake Malawi kwao na kwetu ni Lake Nyasa. Sijui Msumbiji wanaliitaje, Nyasa au Malawi?

Msumbiji wanaliita NIASSA
 
πŸ™‚ πŸ™‚ yeye amebadilisha majina kama cape town, Johannesburg au nyani analiona la mwenzake!?
Hakika mkuu huyu mzee anataka kutuchonganisha tu!
[emoji4] [emoji4]
 
Kwani ziwa lipo tu Uganda? Au Uganda ndo mmiliki wa ziwa? Inamaana nchi za Tanzania na Kenya hazina mamlaka?

Yeye mwenyewe jina "JACOB" ni la kizungu basi nalo alibadilishe
 
Napendekeza liitwe LAKE JULIUS KAMBARAGE NYERERE kwa heshima ya Baba wa Taifa.
"Julius" ni jina la Kizungu vile vile!!
Mimi namshauri aanze kubadilisha jina lake la JACOB kwanza! Akiwa kama MBANTU wa kweli
 
wazo la kubadirisha jina ni zuri ila kwa ukilaza wake anafikiri hilo ziwa lipo Uganda tu
 
I support Zuma. Lake Nyanza is much better kuliko that Victoria CRAP!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…