Press za John John Mnyika mwezi huu zinafikirisha sana

Press za John John Mnyika mwezi huu zinafikirisha sana

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wiki iliyopita Katibu mkuu wa CHADEMA J J Mnyika aliitisha kikao cha waandishi wa habari na kuhoji alipo Rais Magufuli na kama yupo salama. Waziri mkuu mh Majaliwa alijibu siku hiyo hiyo akiwa mkoani Njombe kikazi.

Jana J J Mnyika alitangaza kikao kingine cha waandishi wa habari ambacho kingefanyika leo lakini usiku wa jana alikiahirisha kufuatia tangazo la msiba wa Rais Magufuli lililotolewa na makamu wa Rais Mama Samia.

Huyu J J Mnyika anaonekana kuanza kukomaa kisiasa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hakika ni msiba mzito sana. Kwa nini lakini ulitangazwa usiku??
 
Yaani kila nikifikiria miradi ya JPM nashikwa na huzuni. Sijui nani anaweza kuiendeleza. Maana mwisho wa siku ni kodi zetu.

Maana yote ilikuwa inafanyika kwa utashi wa mtu mmoja!
Siungi mkono pupa ya kutekeleza miradi aliyoanzisha JPM kama alivyokuwa anafanya yeye maana inaharibu uchumi,miradi itekelezwe lakini kwa awamu.Kuna baadhi ya miradimilikuwa ianze kama mabwawa ya umeme wa maji ya Njombe,hiyo ipigwe chini maana haina tija kwa sasa.

Haiingii akilini eti 2/3 ya bajeti ya nishati inaenda kulipia bwawa la nyerere au stiglaz,it doent make sense.Tuwe selective kwenye vipaombele maana uchumi uliumia sana kwa sera zake na hautatengamaa leo au kesho inaweza pita miaka 5 zaidi.
 
Yaani kila nikifikiria miradi ya JPM nashikwa na huzuni. Sijui nani anaweza kuiendeleza. Maana mwisho wa siku ni kodi zetu.

Maana yote ilikuwa inafanyika kwa utashi wa mtu mmoja!
Aisee walipe kwanza pesa zao wastaafu,wana hali ngumu sana huku mtaani.
 
Back
Top Bottom