Press za John John Mnyika mwezi huu zinafikirisha sana

Press za John John Mnyika mwezi huu zinafikirisha sana

Wiki iliyopita Katibu mkuu wa CHADEMA J J Mnyika aliitisha kikao cha waandishi wa habari na kuhoji alipo Rais Magufuli na kama yupo salama. Waziri mkuu mh Majaliwa alijibu siku hiyo hiyo akiwa mkoani Njombe kikazi.

Jana J J Mnyika alitangaza kikao kingine cha waandishi wa habari ambacho kingefanyika leo lakini usiku wa jana alikiahirisha kufuatia tangazo la msiba wa Rais Magufuli lililotolewa na makamu wa Rais mama Samia.

Huyu J J Mnyika anaonekana kuanza kukomaa kisiasa.

Maendeleo hayana vyama!
Mkuu kwani kuna kipi cha ajabu hapo?
Mnyika ni Mtanzania na anajitambua na kapewa madaraka na chama chake kuuliza mswali magumu ambayo wana CCM hawakudirik kuyauliza.

Siyo siri hali ya Rais Magufuli ilikuwa inafuatiliwa zaidi kule Twitani kuliko matamko ya akina Chalamila na Majaliwa.

Ni aibu kwa serikali maana hata leo CNN imponda tamko la msiba kuwa halielezi kiini cha kifo.
Mficha ficha maradhi kifo kinamuumbua
Zile sera za mheshimiwa Mkapa , sera za Ukweli na Uwazi, ziliishia wapi?
Serikali lazima ijitambue kuwa huwezi kuishi kwa kumanipulate News , hasa nzito.
 
Bahati mbaya ccm ni wale wale siku zote, wala tusitalajie jipya lolote!!
Mama Samia bahati nzuri sio mgeni tumemuona na tunamjua,toka bunge la katiba tuliona sura yake vizuri,kipindi cha kampeini za urais, tulisikia matamshi yake haliyo yatoa uko Mbeya!! Sio Kiongozi anaependa kufata sheria na utaratibu, watanzania tuna kazi kubwa ya kufanya kama kweli tuna nia ya kutoka kwenye huu mkwamo!! Lakini kusema eti kuwa CCM italeta mabadiliko hizo ni ndoto za mchana
 
JF wajuaji ni wengi, wanachambua mambo magumu na kudhani ni kitu rahisi sana. kuliongoza taifa lolote si kitu kidogo, nje na vifungu vya sheria tunavyovijua nadhani kuna mengine makubwa zaidi hatuyajui. kwaio tupunguze mihemko, Mr. President ametangulia na sisi twafata, sababu hakuna atakae ikosa haki ya kifo
 
Siungi mkono pupa ya kutekeleza miradi aliyoanzisha JPM kama alivyokuwa anafanya yeye maana inaharibu uchumi,miradi itekelezwe lakini kwa awamu.Kuna baadhi ya miradimilikuwa ianze kama mabwawa ya umeme wa maji ya Njombe,hiyo ipigwe chini maana haina tija kwa sasa.

Haiingii akilini eti 2/3 ya bajeti ya nishati inaenda kulipia bwawa la nyerere au stiglaz,it doent make sense.Tuwe selective kwenye vipaombele maana uchumi uliumia sana kwa sera zake na hautatengamaa leo au kesho inaweza pita miaka 5 zaidi.
Hold on please. A new era in offing.
 
Yaani kila nikifikiria miradi ya JPM nashikwa na huzuni. Sijui nani anaweza kuiendeleza. Maana mwisho wa siku ni kodi zetu.

Maana yote ilikuwa inafanyika kwa utashi wa mtu mmoja!

Ndio maana guru wa miradi walikua wanahoji juu ya affordability, sustainability na kama ndio priority zetu. haya maswali hayakua na jibu! Ila goma lilikua linakwenda mpelampela kwa one mans show!
 
Yaani kila nikifikiria miradi ya JPM nashikwa na huzuni. Sijui nani anaweza kuiendeleza. Maana mwisho wa siku ni kodi zetu.

Maana yote ilikuwa inafanyika kwa utashi wa mtu mmoja!
Miradi ya JPM ni ipi iyo?
 
Yaani kila nikifikiria miradi ya JPM nashikwa na huzuni. Sijui nani anaweza kuiendeleza. Maana mwisho wa siku ni kodi zetu.

Maana yote ilikuwa inafanyika kwa utashi wa mtu mmoja!
Nikiufikiria uwanja wa ndege wa Chato nashikwa na huzuni kubwa, utafanya kazi gani ule uwanja jamani
 
Back
Top Bottom