Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Safi kabisa aya mashairi yatasaidia ktk harakati za kumtafuna nifah
Watu na fani zaoDah! Shaaban Robert kafufuka nn maana mnapanga vina balaaa
Einstein umekula hongo, moto nimekushitukia,Sijawahi kukutana na uzi mtam kama huu.
Hii ndiyo raha ya JF ya bhana.
Mpambano mkali kati ya vampire_hunter007
Sooth
moto2012
Matokeo ya awali
Sooth;40%
vampire_hunter007;35%
moto2012;25%
Endeleeni watoto wa S.Robert.
Mmoja wenu atampata tu Preta
Teh teh teh.
Huu uzi chiboko!
Mpambano mkali kati ya vampire_hunter007
Sooth
moto2012
Matokeo ya awali
Sooth;40%
vampire_hunter007;35%
moto2012;25%
Endeleeni watoto wa S.Robert.
Mmoja wenu atampata tu Preta
Einstein umekula hongo, moto nimekushitukia,
Alama watoa fyongo, Sooth kumpendelea,
Hakika takuwanga magongo, ka Jecha nitakubutua,
Preta ajua mi ndiye wake mume, Einstein acha ulozi.
Einstein acha ulozi, kwa umrio hilo sio dili,
Umeuanza uchokozi, Preta wangu kumjadili
Nahisi wewe ni mdokozi, wallah ntasoma Albadili,
Einstein wewe ni dalali, hilo nimeng'amua.
Einstein umekubuhu kwa udalali, moto leo ninakuumbua
vampire sio rijali, katu hatonipindua.
Sooth hana lolote dili, tungo zake zamuumbua.
Muniwache na wangu Preta, wapambe nyie nuksi
mseminari mdogo,Kuandika si shahiri,
kutunga uwe mahiri,
Tuandike kimistari,
Tusiwe wakukariri,
Ushairi si upori,
Tutunge kama stori,
Vipangeni vina vyenu, mizani haitimii.
Beti zenu sio nzuri,
Vina ni kama kaburi,
Vimejawa na kiburi,
Umalenga ni saburi,
Guni yenu mashairi,
Mabaya kama sifuri,
Vipangeni vina vyenu, mizani haitimii
Nimewaona malenga,
Wanajua kujipanga,
Tungo zao huzijenga,
Hawajui kusimanga,
Hoja zao kokomanga,
Hasira zao kibanga,
Vipangeni vina vyenu, mizani haitimii
Tumieni tafsida,
Sije leta zenu shida,
Kukariri Kuna mda,
Kwanini kuwa kimada,
Preta siyo mziwanda,
Wala yeye si kiwanda,
Chagua umpendaye,
Mimi simo shindanoni.
Kaditama kituoni,
Tungo naiweka poni,
Malenga sipo tanzini,
Preta watoe kundini,
Wajifunze kwa kughani,
Tulifundishwa jandoni,
Preta jipatie wako,
Aghani tumsifu.
Kukaa kimya si dawa,Mwenyewe Mali nimejikalia kimyaaaaa
Kutunga hakika fani,Watu na fani zao