Lara moja kweli waru, tena sana mtandaoni
Mkali ka mtoza ushuru, tuli awapo nyumbani
Katu sitoe udhuru, akufaa kitandani
Lala 1 saizi yako, muache wangu Preta
Simba akiwa kimya, huyo mzee kibogoyo
Waweza hata kumfinya, amebakia poyoyo
Hathubutu kumung'unya, japo tamani kwa moyo
Simba ninaemjua, ana sauti nzito haendi kimyakimya
Sasa kura na ipigwe, sera zifike tamati
Heshima na irejeshwe, bila tumia manati
Preta piga hawa mawe, ikibidi kiberiti
Preta chagua wako mwandani, kura yako naitaka
Asije tokea Jecha, walahi sitakubali
Hapa pote patachacha, eleweni tafadhali
Nasubiri usiku kucha, matokeo ya halali
Preta piga kura sasa, ufukuze mamluki
Lara 1 waru waru, hakuna asojua.
Mtanie auto baru, ngebe zitakuishia.
Preta Fundi subaru, moto nimejipatia.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Ndoa sio bomani, hili neno shika.
Ndoa sio Kanisani, Bali Moyoni hushika.
Moyo huwa shakani, mke wa mtu ukishika.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Acha kujikweza Mlowezi, yatakushinda mbeleni.
Preta wangu humwezi, utashushwa kulingeni
Preta mali ya mkwezi, Mlowezi taishia kutamani.
Simba mwenda kimya, nyama ninaifaidi.
Kuna wajinga wamevamia, huu uzi bila kujua
Preta mi ndo ananizimia, moyoni kwake nimetulia
Anasubiri kunivulia, penzi aweze npatia
Nampa vitu mpaka analia, dozi inamuingia
Naomba wanoko mpotee, uzi mniachie
Preta hapendi wazee, kama mlivyo nyie
Preta ni wangu yo mazee, muda mwingine mfikirie
Mwacheni sasa achekelee, mume amejipatia
Lara moja hana utu, staki ata kumsikia
Wacha auze wake za watu, mapenzi atayasikia tu
Mi napendaga story zake tu, huwa znanivutia
Moyo wangu upo kwa preta tu, naye anipenda pia
Preta naomba unikubalie, usiogope ilo jina langu
Please njoo nkukumbatie, uweze kufeel joto langu
Penzi nono nkupatie, hiyo ndo hobby yangu
Moyo wangu uushikilie, we ndo mboni ya jicho langu
Achana na Sooth ni muongo, hilo nalitambua
moto2012 ana longolongo, najua anakusumbua
Mashairi yote ni fyongo, mi ndo nakulilia
Hakuna ka preta apa bongo, hata na majuu pia
Pretaaaa oooh preeetaaaaaaa we ni wangu mamaaaaa