Preta njoo nikutongoze, wengine tulieni mjifunze

Uwanja wa tungo, he he he kigezo ingekuwa mistari wengine tungeishia kupepesa macho tu.
 
Safi kabisa aya mashairi yatasaidia ktk harakati za kumtafuna nifah
 
Safi kabisa aya mashairi yatasaidia ktk harakati za kumtafuna nifah

Huu mtongozo haumuhusu Nifah, waungwana tulieni mtuwache,
Huyo Nifah sio mashallah, Moto na Sooth twamwona mkweche,
Labda dili kwake Abdallah, Vampire hashobokei vicheche,
Preta amenichagua mimi,tangia akiwa binti kigori,

Tangia akiwa binti kigori, Moto posa niliipeleka,
Wamepoke yangu mahari, wazazi walostarabika,
Hawa kutaka zangu dinari, kwa binti aliyeumbika,

Watu8 mtani katu usinyamaze, king'asti mshenga toa tamko,
Arushaone njoo uzungumze, Sooth imwishie mihemko,
Dada FP njoo upige zeze, tulikamilishe la kwetu tambiko,
Preta wangu mwandani, milele nitakupenda
 
Einstein umekula hongo, moto nimekushitukia,
Alama watoa fyongo, Sooth kumpendelea,
Hakika takuwanga magongo, ka Jecha nitakubutua,
Preta ajua mi ndiye wake mume, Einstein acha ulozi.

Einstein acha ulozi, kwa umrio hilo sio dili,
Umeuanza uchokozi, Preta wangu kumjadili
Nahisi wewe ni mdokozi, wallah ntasoma Albadili,
Einstein wewe ni dalali, hilo nimeng'amua.

Einstein umekubuhu kwa udalali, moto leo ninakuumbua
vampire sio rijali, katu hatonipindua.
Sooth hana lolote dili, tungo zake zamuumbua.
Muniwache na wangu Preta, wapambe nyie nuksi
 
Preta nipe kaz ya urefa na umeneja nikuendeshee zoez.
kwanza itabidi watume chapaa za kuendea sokoni. shopping huko tutaanza mchujo wa awali
 
Teh teh teh.
Huu uzi chiboko!

Mpambano mkali kati ya vampire_hunter007
Sooth
moto2012


Matokeo ya awali
Sooth;40%

vampire_hunter007;35%

moto2012;25%

Endeleeni watoto wa S.Robert.
Mmoja wenu atampata tu Preta

Shukrani kwa kutambua, uzito wa hoja zangu
Wamekosa kitumbua, moyoni wana uchungu
Japo wanifukuzia, wanaona tu ukungu
2025 NEC nakukabidhi maana wewe mtu wa haki

Jecha amepata somo, hakika wewe ni Shule
Yeye kwako mbilikimo, pembeni akae kule
Lubuva memzidi kimo, we kucha wao upele
Akili yako ni jumla ya Newton na Einstein

Ungekuwa huko zenji, singeharibika neno
Umetosha mpaka chenji, umepiga yao meno
Kama Yanga wewe Manji, wewe ni kama msumeno
Wewe mtu adilifu, endelea hivyo hivyo

Machoni hawatapenda, moyoni wana amani
Moto nae anaponda, mwepesi kama majani
Japo wote tunapenda, niachieni maini
Moto wewe bado mchanga, nyonya kwanza
 

Aliyeamua refa, meniweka kwenye sofa
Ongezea maarifa, haya marefu masafa
Nipo juu ya ghorofa, kiwango changu taifa
Wewe bado mchanga, endelea kuzichanga

Uwezo wako tarafa, hunipati kwa kafara
Soma hii taarifa, usifanye masihara
Hoja zako zina ufa, huzizibi kwa mshahara
Kiwango chako cha tarafa, taifa umefuata nini?

Preta tafadhari njoo, huu mzizi ung'oe
Nitulize langu koo, sitakuja nikuboe
Mimi cha kwako kioo, peke yao wazogoe
Preta wewe Hakimu, maliza hii kesi

Wewe mzuri ka waridi, kwangu wewe ni zawadi
Umbo lako maridadi, wanipandisha midadi
Naomba japo miadi, tuifukuze baridi
Preta mimi nina kiu, wewe una maji.

Penzi lako japo tone, ni tamu kama senene
Waachie wapambane, hata walale sanane
Utamu wasiuone, hilo tueleweshane
Wewe ndiye utamu wangu, tafadhali nipe raha
 
Wapi Vampire's hunter?,Sooth unatisha
Ila moto2012 kaza buti

CC;Preta

Mi nipo sijakata tamaa, Preta ntampata bila uchawi wala chapaa
Mwisho wa hili pambano mi ndo nitakayeng'aa
Ntawaacha kina Sooth na moto wakishangaa

Natamani Preta aje akate mzizi wa fitna,
Sjui kwa nini haamini ka mi nampenda sana,
Maisha bila Preta kila siku bora ya jana,
Nikimpata sitamwacha na wala tutogombana

Maisha bila Preta kwangu ni sawa na giza,
Mtoto ana nyota ya Lowassa kila kona anakimbiza,
Iyo siku ntompata moyo wangu atautuliza,
Maisha yangu yatapata nuru na wala sitomliza

Natamani sana nikuimbie hello kama adele,
Ili moyo wako uridhike tuweze kusonga mbele,
Sooth aweze kujua tofauti ya jipu na kipele
Ajue mi ni mfalme wa rymz nlempiku afande sele

Maisha nyewe mafupi Preta acha kudelay,
We ndo wangu akadumba so yule wa mitego ney,
Nshakubembeleza sana kukataliwa spendelei,
Mana naweza kufa akyanani skuongopei.

Please njoo useme neno au nini nikufanyie? ,
Sema unachopenda baby ili nikupatie,
Kisha tusogee private yani wewe na mie,
Ili wambeya wote waumie na walie....

PREEEEEEEEEEEEEETAAAAAAAAAA


PREEEEEEEEE TATATATATATATA
 
Kuandika si shahiri,
kutunga uwe mahiri,
Tuandike kimistari,
Tusiwe wakukariri,
Ushairi si upori,
Tutunge kama stori,
Vipangeni vina vyenu, mizani haitimii.

Beti zenu sio nzuri,
Vina ni kama kaburi,
Vimejawa na kiburi,
Umalenga ni saburi,
Guni yenu mashairi,
Mabaya kama sifuri,
Vipangeni vina vyenu, mizani haitimii

Nimewaona malenga,
Wanajua kujipanga,
Tungo zao huzijenga,
Hawajui kusimanga,
Hoja zao kokomanga,
Hasira zao kibanga,
Vipangeni vina vyenu, mizani haitimii

Tumieni tafsida,
Sije leta zenu shida,
Kukariri Kuna mda,
Kwanini kuwa kimada,
Preta siyo mziwanda,
Wala yeye si kiwanda,
Chagua umpendaye,
Mimi simo shindanoni.


Kaditama kituoni,
Tungo naiweka poni,
Malenga sipo tanzini,
Preta watoe kundini,
Wajifunze kwa kughani,
Tulifundishwa jandoni,
Preta jipatie wako,
Aghani tumsifu.
 
mseminari mdogo,
mapenzi siyo udogo,
wache wao na mipango,
preta kumtongoza.

kutongoza si mchezo,
maneno siyo uwezo,
vina isiwe kikwazo,
preta kumtongoza.

umetoa ushauri,
na wala si umahiri,
mimi sikuja kwa shari,
twasubiria mshindi.

vampire alianza,
sooth naye katongoza,
moto naye kafukuza,
preta kumtongoza.

preta utoe jibu,
neno lako ni muhibu,
uondoe maswahibu,
mshindi apatikane.

uchague kwa mapenzi,
wala si kufata tenzi,
na mshindi umuenzi,
afurahie mapenzi.

mshindi akubalike,
apewe heshima yake,
na hatamu aishike,
matunzo kwa mke wake.

mkubali matokeo,
mtoe uelekeo,
hayo ndiyo mapokeo,
ya wowote ushindani.

kaditama ninafika,
preta wasubirika,
mdada wakubalika,
mekanika mbobezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…