mseminari mdogo
JF-Expert Member
- Aug 18, 2011
- 228
- 146
Kuchomoka ni busara,Kwa haya mashairi Preta unapakuchomokea kweli?
Heee....Kuchomoka ni busara,
Vale hupati hasara,
Kichwa chako si kipara,
Tulia acha papara,
Preta hataki mkwara,
Hujipanga kila Mara,
Kisha Pima zao tenzi,
Majibu kawapatia
Wewe wawachonganisha,Teh teh teh.
Huu uzi chiboko!
Mpambano mkali kati ya vampire_hunter007
Sooth
moto2012
Matokeo ya awali
Sooth;40%
vampire_hunter007;35%
moto2012;25%
Endeleeni watoto wa S.Robert.
Mmoja wenu atampata tu Preta
majibu hajayatoa,Kuchomoka ni busara,
Vale hupati hasara,
Kichwa chako si kipara,
Tulia acha papara,
Preta hataki mkwara,
Hujipanga kila Mara,
Kisha Pima zao tenzi,
Majibu kawapatia
Mie nimechagua King'asti, posa yangu kuipeleka,majibu hajayatoa,
wengi wanasubiria,
mshindi kushangilia,
preta akikubali.
kwanza mshenga ni nani?
kwenye huu ushindani,
preta haonekani,
majibu kuja kutoa.
preta toa utata,
washindani wanatweta,
viroho vinafukuta,
watoe kwenye utata.
preta uwahi kuja,Mie nimechagua King'asti, posa yangu kuipeleka,
Wala hakupoteza wakati, kwa haraka alichakarika,
Ilikamilika mikakati, kabla Sooth hajafika,
Preta ni wangu laazizi, Mseminari kaa pembeni,
Mizani kupanga tatizo, Mseminari upo sahihi,
Utamu uwe kibwagizo, Mizani isiwe kebehi,
Preta ni langu tulizo, hata ka Mizani sio sahihi,
Mseminari kaa pembeni, uniache na wangu Preta.
Vina mpangie Valentina, huyo ndiye lako chaguo,
Sooth ametulizana, beti zimeisha kwa mkupuo,
Preta wangu tumeshibana, Vampire sio lake chaguo,
Moto natangaza bila kificho, Preta ni wangu kitambo.
Preta ni wangu kitambo, Mseminari acha chokoo,
Sooth acha zako tambo, mwishowe utakausha koo,
Vampire komesha majigambo, hapa sio kariakoo,
Preta baki mafichoni, tule zetu raha.
Mahaba yako nigaragaze, Preta ndiwe langu tunda,
Sauti yako sawia zeze, milele moto nitakupenda,
Mdumange tuucheze, wapambe waendelee kukonda,
Preta ni wangu kitambo, Mseminari rudi konventini
Mseminari unatamani, Moto nimeng'amua,
Ndugu Karibia kilingeni, Mizani acha kusingizia,
Umeipanga sawia Mizani, ila Preta hutompatia,
Jaribu ingine gia, Moto nimekushtukia
Ushindani siuwezi,Mie nimechagua King'asti, posa yangu kuipeleka,

Vampire ndiye tajiua, Nsereko ninakujuza,preta uwahi kuja,
washindani wanangoja,
uje umalize hoja,
mshindi kutupatia.
au tumia kanuni,
wa mwisho ndiyo kawini,
uupime umakini,
mshindi kutupatia.
mapenzi unayajua,
wapinzani watambua,
wasije wakajiua,
kulikosa lako pendo.
Misa kwangu ni lazima,Vampire ndiye tajiua, Nsereko ninakujuza,
Sooth alishakimbia, jukwaani hawezi jitokeza,
Mseminari anaugulia, Preta amemgaragaza,
Moto ndimi wake mume, Preta moyoni Karidhia,
Preta moyoni Karidhia, hahitaji kupigiwa debe,
Kimya zake kajikalia, timu bazazi kawakata ngebe,
Amezichoka zenu kadhia, amejichimbia kule entebe,
Nsereko Kula zangu Mia, jukwaa kulisimamia.
Preta ni wangu wa ujana, kumuenzi ni wangu wajibu,
Penzi letu si la juzi wala jana, hahitaji mtu kumjibu,
Kwangu Preta katulizana, hayataki yenu mjaribu,
Preta ndiye wangu Muhibu, mapenziye yamenipagamu.
Mapenziye yamenipagamu, kwake yamini nimekula,
Miaka kenda timamu, penzi halijawa dharula,
Haijaniishia yake hamu, hapa hakuna kulala
Preta ni wangu mwandani, Mseminari kasome misa
naomba usikimbie,Ushindani siuwezi,
Moto hofia pumzi,
Wito wangu si mapenzi,
Nilishatoa kitanzi,
Usikate langu pozi,
Preta ni kikohozi,
Jipange sawa sawa,
Sooth yupo kwenye Kasi.
Sijazoea kunyata,
Kujificha ni utata,
Moto wataka kunata,
Eti Preta shampata?
Wapo walio na data,
Huyo kazua utata,
Jipange sawa sawa,
Preta hataki bughudha
Na mtungia shairi,
Kaacha kuwafikiri,
Anasoma takriri,
Hataki ya kukariri,
Anajua kuhariri,
Ya Pwani Naya bahari,
Preta sio size yako, jiondoe shindanoni
Cheki alivyotulia,
Kuwajibu kasusia,
Moto umezimikia,
Majivu umebakia,
Mseminari sijakimbia,
Konventi najirudia,
Nimeona mmepwaya,
Mizani haitimii.
Wajuze mshindanao,
Kwa Preta sio mwambao,
Ujue kulima mazao,
Tena utunze mafao,
Usijute kalimao,
Ukabakia kikao,
Nimewachia ulingo, narudia Abasia
Kukaa kimya si dawa,
Kwani wewe ni mtawa,
Onyesha chako kipawa,
Kwamba wewe unapawa,
Hukumuona Mkwawa,
Hakutaka tawaliwa,
Kukaa kimya ugonjwa,
Zungumza Mwana kwetu
hujaonyesha ukali,Mimi si mtawa japo changu kipawa
naona hei kunyamaa
kuliko kutwa kubwabwajaa
kwani mtoto katuwamaa
mapenzi kwangu yamejaa
yanini basi kulalama wakati mali najilia
mtoto hapa hana ujanja kwa hakika kazama
Preta achana na vimpire utampwaya... njoo kwangu nile hiyo tende yako mlimbwende. Acha kusonya nisije kunyosoa. Mie ndie mtenda, nikutenda utapenda,