majibu hajayatoa,
wengi wanasubiria,
mshindi kushangilia,
preta akikubali.
kwanza mshenga ni nani?
kwenye huu ushindani,
preta haonekani,
majibu kuja kutoa.
preta toa utata,
washindani wanatweta,
viroho vinafukuta,
watoe kwenye utata.
Mie nimechagua King'asti, posa yangu kuipeleka,
Wala hakupoteza wakati, kwa haraka alichakarika,
Ilikamilika mikakati, kabla Sooth hajafika,
Preta ni wangu laazizi, Mseminari kaa pembeni,
Mizani kupanga tatizo, Mseminari upo sahihi,
Utamu uwe kibwagizo, Mizani isiwe kebehi,
Preta ni langu tulizo, hata ka Mizani sio sahihi,
Mseminari kaa pembeni, uniache na wangu Preta.
Vina mpangie Valentina, huyo ndiye lako chaguo,
Sooth ametulizana, beti zimeisha kwa mkupuo,
Preta wangu tumeshibana, Vampire sio lake chaguo,
Moto natangaza bila kificho, Preta ni wangu kitambo.
Preta ni wangu kitambo, Mseminari acha chokoo,
Sooth acha zako tambo, mwishowe utakausha koo,
Vampire komesha majigambo, hapa sio kariakoo,
Preta baki mafichoni, tule zetu raha.
Mahaba yako nigaragaze, Preta ndiwe langu tunda,
Sauti yako sawia zeze, milele moto nitakupenda,
Mdumange tuucheze, wapambe waendelee kukonda,
Preta ni wangu kitambo, Mseminari rudi konventini
Mseminari unatamani, Moto nimeng'amua,
Ndugu Karibia kilingeni, Mizani acha kusingizia,
Umeipanga sawia Mizani, ila Preta hutompatia,
Jaribu ingine gia, Moto nimekushtukia