Preview ya Black Panther Wakanda Forever 2022

Preview ya Black Panther Wakanda Forever 2022

Iv kati ya Marvel na Disney nani anakimbiza sasa hivi?
Kwa nijavyojua hawa marvel ni tawi la Disney yani Disney alishanunua hiyo kampuni zipo chini yake, yeye ni kutow tu mkwanja kwenye movie wanazoandaa
 
Iv kati ya Marvel na Disney nani anakimbiza sasa hivi?
Unazungumzia disney ipi???
Maana Walt Disney Company LLC ndio inamiliki Marvel. Iliinunua mwaka 2009. . Disney inamiliki makampuni kadhaa ya kutengeneza muvi kama vile Marvel Studio, Lucas Film/Star Wars, 20th Century Fox, Pixar Animation Studio, Walt Disney Pictures na Walt Disney animations

Weka vizuri swali lako upewe uchambuzi
 
Kwa nijavyojua hawa marvel ni tawi la Disney yani Disney alishanunua hiyo kampuni zipo chini yake, yeye ni kutow tu mkwanja kwenye movie wanazoandaa
Yeaah Marvel Studio ipo chini ya Kevin as President ila nae yupo chini ya director wa Walt Disney Bob igler. Wao wanatoa pesa tu na kutoa final say kipi kitengenezwe kipi kisitengenezwe hata ushoga, femmenism hutoka huko huko disney
 
Hivi wale watu wa yts wanapata faida gani kutoa movies free kwa watu na hali ukifatilia movie moja kwa nchi za watu ni gharama sana kuitazama!?
 
Hivi wale watu wa yts wanapata faida gani kutoa movies free kwa watu na hali ukifatilia movie moja kwa nchi za watu ni gharama sana kuitazama!?
Hua kuna matangazo kwenye site zao ndio wanachopata. Ila kwa hizi muvi watasubiri sana hua hazipatikani kirahisi
 
FB_IMG_16684273289191142.jpg
 
View attachment 2401378
Kuna watu unajikuta unawapenda bila sababu yoyote/unconditionally yaani unamkubali tu, basi upande wangu kuna orodha ndefu ya watu wengi ninaowakubali sana kama vile 2Pac, Mohamed Ali, T. Sankara, P. Lumumba, Kit Harington, Charlie Cox, Nyerere, fidel Castro, Luck Dube,JPM, Jidenna, Runtown, Ckay, Putin, nk. Mwingine niliyekua namkubali ni Chadwick Boseman aliyefariki 28.August 2020 kwa kansa ya utumbu mkubwa. So I’m writting this as a tribute to him and to all Black Panther fans.

Ulishawahi kujiuliza kwanini muvi nyngi za kizungu ambazo hua zinazungumzia tamaduni za afrika mashariki mara nyingi sana hua hawagusii kabisa kuhusu Tanzania. Unakuta labda kitu Fulani asili yake ipo Tanzania laki wazungu wanasema kipo Kenya mfano kiswahli, maasai, Kilimanjaro nk wazungu wanajua kabisa asili ya vitu hivyo ni Tanzania ila wanaamua kusema ni Kenya pengne hua ni mara chache sana kukuta nchi yetu hii kua imetajwa au kuonyeshwa kwenye muvi za wazungu, hata kama muvi imeigiziwa kwenye baadhi ya location za hapa Tanzania basi watasema ni Kenya au Uganda.

Mfano mzuri ni muvi ya The Lion King, mazngira ya muvi hii ni Serengeti, hata majina ya character ni Kiswahili ila walifanya asil yake ionekane ni Kenya. Niliwahi kuona mara moja tu kwenye series ya Blacklist nchi yetu ikitajwa, sio sisi tu hata Ghana ni hivyo hivyo pia mara nyingi hua inaonyeshawa Nigeria…hata kama kitu asili yake ni Ghana basi hubadirishiwa Nigeria.
View attachment 2401451
Well, sababu kuu hua ni ajili ya Ukomunisti wetu ambao nyerere aliutoa Urus na China. Baada ya vita ya pili ya dunia adui mkubwa wa US na EU aliyeibuka ni Russia akiwa na Communism as model of production, huku US ikiwa na Capitalism as a model of production….Kipindi hicho sasa ndio vichwa vya wasomi wa kiafrika vilikua vimecharuka kudai uhuru wao na kimbilio lao wengi waliona Model ya Russia ndio ingeweza kuwasaidia kuwaondoa wakoloni ukizingatia USSR haikutawala afrika…..Hapo US akiwa kama kilanja wa dunia hakupendezwa na model hiyo ya urusi kwani ingemfanya ashindwe kutekeleza mbinu yake mpya ya ukoloni mambo leo ipasavyo hivyo alichukulia Russia na Communism ni adui yake na chi zote zitakazofuata Communism basi ni adui yake.

Nyerere kama tunavyomjua alikua mjamaa asiyejilimbikizia mali, alifuata model ya Communism kama njia ya kuongoza taifa letu so US katuweka kwenye kundi la adui wake ndio maana kamwe huwezi kuta nyerere katajwa au kuonyeshwa kwenye muvi za Hollywood….Nyerere hakuwapa wazungu kile "walichokua wanakita" toka kwetu ndio maana hua hatajwi popote japokua ana mchango mkubwa katika mataifa ya mengi ya Afrika. Lakini Mandela,Gandhi, Kenyatta nk hawa watu waliwapa wazungu kile walichokihitaji ndio maana kuna muvi nyingi sana Gandhi na Mandela wametajwa na kusifiwa zingine wametengenezewa kama Documentary huko Hollywood.
View attachment 2401453
……
Hii inahusiana vipi na muvi hii?

Wakati Stan Lee anatengeneza nchi ya kufikirika ya Wakanda mwaka 1966 alitaka wakanda iwe Tanzania(Tanganyika kwa kipindi hicho) kutokana na upekee, uzuri na asili ya tafa letu. Chunguzi za kisayansi na kihistoria zinaonyesha kwamba asili ya mwanadamu ni Afrika kumbuka pia inasemekana Eden pia ilikua Tanzania(Olduvai George) kwa mujibu wa uchunguzi wa kihistoria. Lakini stan lee alishindwa kufanya hvyo maana Tanzania ilikua ipo kwenye ukomunisti na kipindi hicho urusi na marekani walikua kwenye vita baridi akaamua kuihamishia nchi ya wakanda iwe Rwanda na sio Tanzania.

Deeping Deeper….

Wakanda ni nchi iliyopo afrika mashariki kaskazin kidogo mwa Tanzania ambapo ndio Rwanda ilipo wakazi wa nchi hii ya kufikirika wanaongea lugha ya Xhosa, Yoruba na English wanamuabudu mungu wao aitwae Bast, bast ni mungu ambae ana kichwa cha paka kutoka katika taifa la misri ya zamani ambae huko huitwa Bastet. Miaka mingi iliyopita kimondo chenye element ya Vibranium kilianguka katika nch ya wakanda, kimondo hicho kilisababisha mionzi ambayo ilibadirisha mimea ambapo ilitokea mmea unaoitwa Heart shaped Herb 💜 ambayo ilitumiwa na familia pekee ya kifalme, mmea huo uliwasaida kuwaongezea nguvu pia walitumia madinii kuendeleza teknolojia yao. Wakanda ikawa taifa tajiri zaidi na lenye tekneloja kubwa zaidi duniani kwa kuogopa teknolijia na madini yao kuibiwa na kutumiwa na mataifa mengne waliamua kujificha kwa kutumia teknolojia yao.
View attachment 2401776
[Letitia Wright/Shuri akiwa kakaa pozi alilofanya Chad 2018]

Sitapenda kuhadithia sana maana naamini wengi wameitazama hii muvi.
Black panther ni jina analopewa mtawala wa nchi ya wakanda, kuna huyu mfalme alikua anaitwa T’chaka alioa mwanamke aitwae N’ymi akamzalia mtoto mmoja bahati mbaya alifariki wakati anajifungua na kumuacha mtoto wa kiume aliyeitwa T’challa. Mfalme T’chaka alioa mwanamke mwingine kutoka south Africa ambae aliitwa Ramonda, ramonda alizaa mtoto wa kike Shurii. Tchalla alitokea kumpenda binti mmoja yatima aitwae Ororo Monroe ambae hutambulika kama storm kwenye muvi za X-Men, kwenye Comics Storm ni mke wa Tchala. Japo yeye storm ni mzawa wa Egypt

Walikutanaje?

Kuna matatizo kadhaa yaliyomtokea storm akakimbilia mkoa wa Mara Tanzania akawa anakaa kwenye moja ya kijiji kilichopo karibu na hifadhi ya Serengeti akawa anawasaidia wanakijiji katika shughuli mbalimbali kwa kutumia nguvu zake, siku moja Tchala akatoka wakanda akaja kutalii katika mbuga ya Serengeti. Huko Serengeti ndipo walipokutana na Storm wakapendana na kuoana. Ngoja niishie hapo nisielezee zaidi kama unataka kujua zaidi tafuta comics usome maana What happened in Comics stays in Comics.
View attachment 2401424
[Pisi kali Halle Berry aliyeigiza kama Storm]

Black Panther: Wakanda Forever

Japo alikua ameshaanza mazoezi na lishe maalumu ya kuongeza mwili ,Wiki mbili kabla ya chadwick kufariki alipungua mwili na kua mwembamba sana ajili ya ugonjwa aliokua anaumwa. Bahati mbaya hakua amemwambia mtu yoyote juu ya ugonjwa aliokua anaumwa tofauti na familia yake hivyo basi wakati Director Ryan Coogler anaandaa script alikua ameitengeneza maalumu ajili ya Chad so baada ya kifo cha Chad ilibidi wabadirishe Script nzima na kumfanya Shuri awe mrithi wa ufalme, well hata kwenye comics Tchala alikufa shuri ndio akashika ufalme.
View attachment 2401421
[Chadwick Boseman Akiwa kakonda wiki kadhaa kabla kifo chake]

CEO wa Marvel Kevin Feige alisema kwamba hawatamchukua mwigizaji mwingine kucheza kama Tchala sababu haitakua vyema kwa mashabiki pia anataka historia ibaki hivyo kua Chad ndio pekee aliyeicheza character ya Black Panther. Wakati muigizaji Paul walker amefariki mdogo wake alimalizia kucheza vipande vilivyobaki as Standing-In na kutumia CGI kuweka sura ya paul waker….so ilitegemewa kwamba na kwenye BP2 itatumika teknolojia hiyo ila walikataa so inawezekana hatutaiona tena Character ya Tchalla kwenye muvi labda kwenye animated series kama What If..? Coz anyone can do voice acting.
View attachment 2401434
Kwenye muvi ya BP2018 tuliona kwamba Killmonger baada ya kumshinda tchalla na kuchukua ufalme alichoma moto ile mimea ya Heart Shaped Herb 💜ambayo ilikua inawajalia nguvu na kuwaungansiha na wafalme waliokufa /waliopita. So unaweza kujiuliza Shuri atakuwaje the next Black Panther na kupata nguvu bila kutumia ule mmea? Nguvu atazitoa wapi? Well Shuri is a tech genius atatumia technology kujipatia nguvu zake.

Kama mtakumbuka mwisho wa muvi ya BP 2018 Tchalla alinunua majengo kadhaa marekani akasema itakua ni kituo cha kushea techonolgy waliyonayo kwa dunia, pia in Post credit scene akaenda kwenye mkutano wa UN kusema yupo tayari kushirikiana na dunia na kutoa msaada pindi inapohitajika (kuna mtu alimuuliza nchi ya wakulima ina kipi cha maana itakochoichangia dunia?? Wafrika tunazalauliwa asiee)

Kumbuka kwamba kipindi chote hicho nchi ya wakanda ilikua imejificha wazungu wanajua ni nchi maskini yaani kama vile wazungu wakija TZ wanafikia Bukoba huko huko kwenye mapori ila Arusha mji ulioendelea tumeuficha kwa tekolojia……Sasa kitendo cha Tchalla kwenda UN kujitangaza na kutaka kushea Technology lilikua kosa kubwa. Kuna jamii nyingine ya watu ilikua inaishi chini ya Maji (Tolokan) na yenyewe ilikua haitaki kufahamika kama ipo duniani sasa Tchala kufanya vile ile jamii ikaona watafahamika walipo..kumbuka eneo lolote lenye amani akikanyaga mzungu tu basi amani hupotea. Sasa hapo ndio ikaanza vita kati ya watu wa Ardhini (Wakanda) na Waishio ndani ya Maji(Tolokan) muvi ndio inahusu ugomvi huu….Well, kama kawaida yao Hollywood wana agenda zao wanazozipromote za LGBT na Feminism na muvi hii itakua na lesbians + Feminism.

Tukutane November 11 kuinjoi muvi yetu pendwa kwa wapenzi wa muvi najua hata wasiokua wapenzi wa muvi hua wanaitazama hii muvi. Hasa kwa sisi weusi maana inaonyesha Black Supremacy.
-Criston Cole.
View attachment 2401430
Naomba link nidownload
 
Nawapaga Challenge fans wa Marvel Studio waulize swali lolote kuhusu MCU sijapata challenge kubwa niitakayo!
So if you have any Qns regarding MCU or GOT unaweza uliza. mate!
Okay


1)Nebula ni binadamu au nani hasa kwanini wanaitana dada na Gomora na iweje awe anamtumikia Ronan na Thanos??

2)Chard Wick(Actor wa Black Panther) amekufa kiukweli in real life lakini kule kwenye Movie ya BP ya kwanza hakufa Sasa kwanini kwenye BP hii ya 2022 tunaoneshwa amekufa na hatujaona amekufaje na wapi ??

3)....
 
Okay


1)Nebula ni binadamu au nani hasa kwanini wanaitana dada na Gomora na iweje awe anamtumikia Ronan na Thanos??
Nebula si binaadamu. Kiukweli bado sijajua race yake ni ipi ila kutokana na rangi ya ngozi yake naweza kusema ni Kree. Maana kree ndio wana rangi ya blue.
So Nebula alikua adopted na Thanos kama ilivyokua kwa Gamora baada ya wazazi wao kuuawa. So walikua pamoja kama mkubwa na mdogo ila Thanos alikua anaona kwamba Nebula sio prefect kama Gamora so kila alipokua anaona udhaifu kwa nebula basi aliondoa kiungo na kuweka technology/vyuma kama robot. Ndio maana yupo kama robot baadhi ya viungo vyake.

Kwa mtazamo wangu nahisi Korath the Parsuer ndio alikua anamtengemeza maana jama alikua mwanasayansi. Kama sio Korath basi atakua High revolutionary ndio alimtengeneza. Tutamuona Kwenye Guardian of the Galaxy vol 3.

Ronan alipewa kazi ya kutafuta Power stone ampelekee Thanos, nebula na Gamora wakawa wasaidizi katika mission hiyo japo Gamora aliasi na kuoeleka power stone kwa Tineleer Tivvan (The Collector)
2)Chard Wick(Actor wa Black Panther) amekufa kiukweli in real life lakini kule kwenye Movie ya BP ya kwanza hakufa Sasa kwanini kwenye BP hii ya 2022 tunaoneshwa amekufa na hatujaona amekufaje na wapi ??
Je umesoma mada yote??
Ok. Chad alikufa ila kabla ya kufa tayari muvi ilikua ishaandaliwa bado kushoot tu so alivyokufa ilibidi Ryan Coogler abadirishe script nzima ya muvi na kuifanya kwamba Chad alikufa kwenye muvi. Lakini kwenye muvi walieleza sababu ya kufa kwake wasingeweza kuonyesha alivyokufa maa a Mwigizaji alikua kafa in real life na hawakutaka kumRecast mtu mwingine kucheza kama T'chala
 
Back
Top Bottom