Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Baada ya utata wa muda mrefu wa mahali alipo kiongozi wa kikundi cha askari wa kukodiwa cha Wagner leo ameonekana hadharani nchini Belarus alikohamishia shughuli zake baada ya jaribio la kutaka kuipindua serikali ya Urusi kuzimwa.
Katika video iliyomuonesha akisalimiana na askari wake aliwaambia askari hao kwamba wamepigana kishujaa sana nchini Ukraine na kwamba kwa sasa hawatapigana tena Ukraine bali wajitayarisha katika vita kama hivyo barani Afrika.