Prigozhin asema hataki tena kupigana Ukraine, anakuja Afrika

International paid mercenaries
 
Jeshi letu unaamini litakuwa na drones huku linamiliki ndege za miaka 40 iliopita 😀😀😀
Mambo ya kivita yamebadilika sana.Nadhani majeshi yote ya Afrika yana vifaa vilivyopitwa na wakati ukiondoa bunduki za rashasha.
 
Acha kuwaongopea watu wewe Wagner ni Urusi na hata yeye mwenyewe awezi kupinga ilo.Prigozhin mwenyewe kasema Urusi ndo nchi mama na popote walipo Wagner uwezi kukosa bendera ya Urusi.
 
Mambo ya kivita yamebadilika sana.Nadhani majeshi yote ya Afrika yana vifaa vilivyopitwa na wakati ukiondoa bunduki za rashasha.
Kwa bunduki huenda zikawepo za kisasa hilo sina shaka nalo ila mahanjumati kama drones na tactical missile hakuna.
 
Kwa bunduki huenda zikawepo za kisasa hilo sina shaka nalo ila mahanjumati kama drones na tactical missile hakuna.
Vita bila drones sasa huwezi kushinda. Vifaru vinakuwa kama keki mbele kijidroni kidogo tu kinachodowea angani na kuona kila kona kutoka angani hata rada za kizamani hawazioni.
Droni ikiona shabaha yake inashuka mpaka chini kama mwewe na kudondosha bomu.
 
Hahahah sasa vita vya kutumia bunduki tu si mtaisha wote 🤣🤣🤣 sijui hata kama bongo wanafanyaga drills na mataifa kama russia au us
 
Hahahah sasa vita vya kutumia bunduki tu si mtaisha wote 🤣🤣🤣 sijui hata kama bongo wanafanyaga drills na mataifa kama russia au us
Kama tunataka Rwanda baada ya kuichukua DP world asije ichukua na bandari yetu basi lazima tuanze kufanya mazoezi ya kivita na mataifa makubwa ili tujuwe namna ya kutumia drones. Kagame nasikia ana jeshi dogo lakini si la kawaida,linapiga kama Wagner.Wanaweza kukatisha kutoka kigoma mpaka Dar es salaam kwa masaa 24 tu.
 
Hahahah hizo story tu mkuu, Kagame anakalishwa mapema mno. Sema nina hisia kuwa anaitaman sana Tanzania. Kwa ujinga unaoendelea atakuja ajimegee kama Ukraine
 
Hahahah hizo story tu mkuu, Kagame anakalishwa mapema mno. Sema nina hisia kuwa anaitaman sana Tanzania. Kwa ujinga unaoendelea atakuja ajimegee kama Ukraine
Sisi tuna faida tuko wengi, lakini nahofia tuwaoga kidogo.Hivyo akitokea mbabe akatupiga tukafa wengi anaweza akajimegea ardhi halafu akakacha kuondoka miaka nenda miaka rudi tukabaki kulalamika UN kama wapalestina. "Mwambie Rwanda aondoke Kagera,pale ni nchi yetu"
 
Furahien ujio wa majeshi ya kigeni ukifika muda mtalia na kusaga magego , yaan unategemea waje kumaliza matatizo yetu ili warudi kwao ? Ili wakaendelee kujibizana na jeshi la Putin na Lukashenko ? mnakaribisha matatizo bila kujua
Ko kuna tatizo ambalo mpaka sasa hatujakutana nalo hapa Africa....!?
 
Sisi Afrika ni bure kabisa.
 
Ushuzi mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…