Laiti tungewafahamu waingereza vizuri, na msala zaidi uwe una asili ya weusi hata kwa mbali then ukaoa au ukaolewa nao hapo ndo utajua nini maana ya Racism! Achilia mbali Royal family, hawa wa kawaida tu ni kwikwi je hao wanaotunza ufalme? Harry ni kama tunamuona amemsikiliza sana mke wake au wengine tunahisi kama amekosea sana kutemana na mambo ya kifalme but hizo familia hazina tofauti na gereza lenye pesa!
Mkuu, wakati mwingine tujifunze kubakiza akiba ya maneno - wewe unajua bibi yake Queen Victoria alikuwa mwenye asili ya bara gani?
Angalia picha ya Queen Victoria alipo kuwa kwenye umri wa uzee ie kabla hajafariki in 1901, je, inakupa impression gani - kwamba ni mzungu by 100%? hana vinasaba vya watu weusi!!
Aliwahi kuletewa binti kutoka aidha Benin au Nigeria sikumbuki vizuri akakubali kumlea na kuishi nae kwenye kasri ya Kifalme Burkingham Palace kaudumiwa kama mwanae wa kumzaa, licha ya Queen Victoria kuwa na watoto wake chungu mzima - licha ya binti huyo kupewa kila kitu Mumewe Queen Victoria alimwambia mkewe kwamba binti huyo anaonekana kama kuna kitu anaki-miss hivyo wakakata shauri kumrudisha Nigeria akasome kwenye shule za bweni za mission, baadae Queen Victoria kawatuma watu kwenda kumfuata binti huyo kutoka Nigeria na kumrudisha kwenye Kasri ya Queen Victoria Uingereza, kaendelea kumsomesha binti aliopofikisha umri wa kuolewa Queen Victoria kamtafutia nchumba huko huko Uingereza ambaye alikuwa ni mfanya biashara na tajiri mwenye asili ya Nigeria akaolewa kwa kufanya harusi yao chini ya usimamizi wa Q.V. , baadae kabisa binti huyo kufariki kutokana na Ugonjwa wa TB.
Kama unafikiri Queen Victoria aliwapenda watu wenye asili ya bara la Afrika bila sababu you better think twice - kuna kitu alikuwa anakumbuka katika family tree yake ya miaka mingi ya nyuma. Kwenye Royal family ya Uingereza mtu mwenye tatizo kubwa la kuendekeza ubaguzi wa rangi na majivuno ni mumewe Queen Elizabeth, yuko very colourful uwezi kujua anaweza kusema nini mbele za wageni/public hatumiagi busara hata kidogo ,unlike Queen Beth.
Back to the main point: Queen Victoria aliwahi vile vile kuwa na mauhusiano ya karibu na mfanya kazi wake kutoka Bara la India - wazungu wabaguzi wa rangi walinchukia sana kijana huyo wa kihindi, Q Victoria alipo pendekeza apewe u knighthood mawaziri na bunge wakamkatalia, Queen Victoria alipo fariki Muhindi huyo alifukuzwa kutoka kwenye kasri ya Kifalme siku hiyo hiyo akapakizwa kwenye meli kurudi India.
Nimalizie kwa kuwahoji tena - mnafikiri ni kitu gani ambacho kilimfanya Queen Victoria hasiwe na ubaguzi wa rangi - wakati wa enzi zake ndio ubaguzi wa rangi ulikuwa ni mkubwa sana huko Uingereza na Merikani.